SOMA KWA MAKINI SANA. By mr.Mende 2014.

SOMA KWA MAKINI SANA. By mr.Mende 2014.

mende 2014

JF-Expert Member
Joined
Apr 13, 2014
Posts
763
Reaction score
131
Hii ni story fupi yenye mafunzo. Nilipoingia katika mahusiano
naye nilimuamini, nikampa kila
kitu nilichoweza. Nakumbuka
enzi zile nyumbani tulikuwa tuna
ng’ombe, niliiba maziwa kila siku
na kumpelekea kwao.
Akanenepa!!
Penzi letu likawa huru alipoanza
maisha yake mwenyewe. Sikuwa
najua lolote kuhusu mapenzi.
Alinifundisha. Nikaegemeza
maisha yangu yote kwake.
Akanifanya nikawa mtumwa wa
ngono kila nikienda chumbani
kwake.
Kama haikutosha sasa akaanza
kunifundisha kunywa pombe.
Niliamini kuwa ndiye mume
wangu mtarajiwa, kwa nini
nikatae? Nilimkubalia kila kitu.
Alinilazimisha ngono hata
nilipokuwa katika siku zangu.
Kweli nilikuwa msomi na
niliyajua madhara ya kufanya
hivyo lakini sikutaka kumuudhi
huyo niliyeamini kuwa ni mume
wangu.
Nilipenda tututmie kinga lakini
aliipinga sana. Nikapata mimba
ya kwanza!! Hakuwa na pesa
lakini alinilazimisha niitoe.
Nikaiba pesa nyumbani
nikafanya alivyotaka. Kwa mara
ya kwanza nikatyoa mimba.
Haikuniuma sana!! Niliamini
kuwa ni yeye atakuja kunioa na
atanifichia aibu hii.
Nilitegemea sasa tutaanza
kutumia kinga. Lakini hapana
haikuwa hivyo. Aliendelea
kunilaghai. Tayari aliujua
udhaifu wangu. Alinishika hapa
na pale. Nikishtuka tayari
amefanya anavyojua.
Pombe kidogo na nyingine
kidogo. Nikazoea lakini nikawa
nawahi kulewa.
Akautumia udhaifu huu
kunifanyia jambo baya
lililonifanya niandike haya
kwako.
Akaniingilia kinyume na
maumbile. Alinilawiti!!
Nilishindwa kumshtaki popote.
Nikavumilia kwa kuwa alikuwa
mume wangu mtarajiwa. Mume
asiyejulikana hata kwa wazazi.
Mchezo ule ukaendelea.
Akajitetea eti hataki nipate
mimba tena, hivyo hiyo ni
mbinu mbadala. Najuta
kumuamini!! Lakini huyo alikuwa
mume wangu.
Miaka ikapita, ule urembo
wangu niliozoea kuuona katika
kioo ukatoweka, simu za mara
kwa mara kutoka kwake
zikatoweka, akawa mkali sana
kwangu. Hakutaka niende
kwake. Wakati huo nilikuwa
nasoma chuo.
Pesa ya mkopo ikitoka
ananitafuta na tunakuwa
marafiki tena. Anasema
ananipenda na atanioa.
Ananilewesha na kunitumia
kinyume na maumbile.
Pesa ikiisha na mapenzi
yanaisha nabaki mwenyewe
katika msoto. Sasa akaanza
kubadilisha wasichana waziwazi.
Ningesema nini mimi?
Ninajua alishindwa kusema
neno moja tu. Tuachane!!
Nilijua tayari ameniacha!!!
Afya yangu ikadolola sana,
nikalazimika kwenda kupima
hospitali.
Sikuwa na virusi. Nikapewa
ushauri nikautumia.
Siku zikasonga nikampata
mwanaume mwingine. Huyu
alikuwa ananijali sana. Nikaanza
kumsahau yule aliyenitenda.
Nilipomaliza chuo
akajitambulisha nyumbani na
alitaka kunioa.
Akanio kweli. Maisha yakaanza.
Mwaka wa kwanza, mwaka wa
pili na hadi wa tatu. Sikuwa
nabeba mimba.
Mume wangu alikuwa mvumilivu
sana, hakuwa hi kunilaumu.
Lakini niliumizwa na mawifi.
Nikaamua kwenda hospitali.
Nikaambiwa kizazi change
kiliharibiwa kwa kutoa mimba
mara kwa mara. Pia mapenzi ya
kinyume na maumbile
yamenivuruga kabisa.
Nililia sana huku nikimkumbuka
yule aliyeuleta uchungu huu
kwangu.
Dunia haikuwa mahali pangu
sahihi.
Nimekuandikia barua hii mdogo
wangu. Uisome mwenyewe!!
Lakini uwasimulie wengi baada
ya kifo changu.
Uwasimulie bila kuchoka
wasichana wa kileo
wanaodanganyika na kufanya
mambo magumu kuwaridhisha
wapenzi wao. Waambie watakufa
kwa mateso kama mimi.
Wasipokusikiliza usijisikie vibaya
maana hata mimi nilikuwa
siwasikilizi watu waliponambia
lolote kuhusu yule mume
mdanganyifu.
Sitajiua lakini nitakufa kabla ya
wakati!!!
Nimekuandikia wewe kwa kuwa
u mwandishi. Japo kwa sasa u
mtoto mdogo najua utaipata
nafasi siku moja ya kuwafikishia
wasichana hawa.
Usilie kwa sababu nitakufa. Lia
kwasababu mwanaume
mwenzako AMENITENDA HIVI!!!
TAFADHALI TAFAKARI
[Gonga "LIKE" kwa yeyote alie
toa Ushuhuda huu mimi Binafsi
nimeukubali na nimeamua
kuupost ili na wewe Uelimike ,
Click "SHARE" ili Watu zaidi
waelimike ,shukrani Zangu
zimfikie alie Muhusika kwa
kushare Pamoja.
 
Pole sana imeniuma sana. Ila ninakulaumu kitu kimoja tu kwamba ulifanya makosa pale alipokuingilia minyume na maumbile maana ukweli uliowazi ni kwamba mtu anayekupenda kwa dhati hawezi kufanya ujinga kama huo. So alipofanya hivyo tayari ilikudhihirishia kuwa hawezi kukuoa bali kujuchezea tu isipokuwa hukuweza kushutuka. Hata hivyo dalili alikuonyesha mapema kuwa hakupendi maana hata. pae alipokuwa anakuwa kando unapoishiwa pesa. Alionyesha kuwa anakupenda sababu ya pesa na bila pesa mapenzi hakuna. Kiujumla pole sana. Akina dada watakaosoma hii iwe ni fundisho kwao.
 
Kwa kweli akina dada wanatakiwa kuwa makini sana maana unapopendwa na wewe kukubali kupendwa ni sawa kabisa ila usikubli kujiachia full kama huyu dada alivyifanya maana ukijiachia hivyo utegemee moja kati ya mawili ambapo kuna kuolewa ama kuachwa. Jambo la pili pia sisi wanaume tujitahidi kuwa wastaarabu sio wakuwatenda mabinti wa watu and at longlast we escape. It's not fair.
 
Back
Top Bottom