Soma hii kwa usalama wako

Kuweni na subira.

Wewe ndiyo yule wa subira yavuta heri, pole. Subira inachelewesha maendeleo. Tumesubiri sana sasa ni miaka 50 ya Uhuru na wazee wa iliyokuwa Jumuiya ya Afrika Mashariki wasubiri tuu?, ila wengi ni marehemu jamani!!
 
Kwa kweli nampa hongera aliyechora katuni hii. Kwanza kasema UKWELI, pili kaonyesha uhalisi wa bei katika mahitaji muhimu kama mafuta, na vyakula kuwa bei juu wakati kipato ni kidogo. Wenye uwezo kifedha, ambao ni wachache ukilinganisha na wasio na uwezo, wao hawaoni uchungu sana kwa vile wanazo. Wanakula mpaka wanasaza. Hembu mwangalie mtu wa KCC (Kima cha chini) anaishije??? Kuna Kampuni ya usafi inawalipa wafanyakazi wake sh elfu 90 tu!!! kwa mwezi. Yenyewe imechukua tenda, inalipwa mapesa mengi sana kwa kila kichwa. Huyo wa 90 elfu ana mke na watoto, amepanga chumba, na anatakiwa alipie huduma zote muhimu kama matibabu, chakula, elimu, n.k. Mtu huyu anaishije??? TAFAKARINI JAMANI. Gadhafi alihakikisha raia wake wanapata kipato bora kuliko cha Mtanzania. Wamemuua. Sasa hivi wanakoma! Tufanyeje??? Hembu mtu wa katuni tuchoree na katuni nyingine ya SULUHISHO.
 
Kajamaa kamenuna baada ya kuulizwa kwanini hakakui! Eeeh Mwenyezi Mungu tusaidie huyu bwana mdogo Salary akue japo afikie nusu ya kimo cha rafiki zake, tunakufa
 
So vizuri kutishana bana, we unataka mishahara ipande kwani na vingine havitapanda? kwanza wafanyakazi wenyewe kazi hawafanyi wote wamekua wana SI HASA na washabiki wa mpira kutwa, Hamasisha watu wafanye kazi kwa bidii na Maarifa!
 
Back
Top Bottom