Soma hii halafu fanya maamuzi sahihi

Soma hii halafu fanya maamuzi sahihi

Joealexist

Member
Joined
Jun 1, 2012
Posts
21
Reaction score
10
Kwa lugha nyepesi ni kwamba ukiajiriwa maana yake umeshindwa kujitegemea kwa ujuzi wako (yaani hujui ufanyie nini) hivyo umeona uukabidhi ujuzi wako kwa wenye "akili na uwezo" wa kuupangia matumizi ya huo ujuzi wako.

Ndio maana licha ya kwamba elimu ni yako wewe, maarifa ni yako wewe, vyeti ni vyako wewe; na kazi unafanya wewe; lakini hao waliokuajiri ndio wanakuamulia kiasi gani wakulipe! Si hivyo tu bali pia wanao uhuru wa kukupiga mkwara, kukutishia na hata kukufukuza muda wowote (utakapowakosea, watakapojisikia ama watakapokuchoka)! Nini nakwambia? Kama umeajiriwa, usiridhike wala usibweteke na mshahara pekee kwa 100%, hebu jiongeze aiseee, una uwezo wa kuzalisha zaidi sambamba na mshahara (waliojisikia) kukulipa.

Usiufunge uchumi wako kwenye gereza la ajira, fikiria zaidi ya ajira maana hao waliokuajiri nakuthibitishia HAKUNA mwenye mpango mzuri na "future" yako, zaidi sana wanaihujumu "future" yako!

Nimemaliza! USHAURI WANGU ANZA KUAJIRIWA KAMA MUWEKEZAJI TU ILI UJIAJIRI NA KUAJIRI WENGINE.

We nuna weee, kasirika weee, vimba weee mpaka upasuke, lakini kidonge hicho kimeze japo kichungu, ndiyo dawa tena utafanyaje, ila mwisho wa siku uwe na SIKU NJEMA ili ukawaze na kuwazua vizuri.

JIPATIE NAKALA YAKO MAPEMA..
View attachment 307669
 
Sio kila taaluma na ujuzi inaweza kukufanya ujuajiri mwenyewe. Mi nimesomea uafisa Uhamiaji ntajiajiri vipi?
 
Au mtaaramu wa mambo ya reli utajiari vipi??

Sidhani kama ni lazima 'ujiajiri' kwenye fani uliyosomea...nina rafiki yangu mkubwa, ana jina hapa mjini, taaluma yake ni Daktari, lakini ni dealer mkubwa sana wa vifaa vya elektroniki, na sasa hakumbuki hata uDaktari tena. Kujiajiri ni uthubutu wa kuchukua fursa zilizo mbele yako bila kujali taaluma yako. Kama fursa iliyopo ni ya taaluma yako, sawa...kama si ya taaluma yako, bado si sababu ya kuiacha ipite!
 
Upo sawa kabisa mkuu ila wavivu wa kufikiri na wale nele nele watakuja hapa kukupinga na matusi juu!
Usihangaike nao sana waache walale!
 
Sio kila taaluma na ujuzi inaweza kukufanya ujuajiri mwenyewe. Mi nimesomea uafisa Uhamiaji ntajiajiri vipi?

kusafirisha watu na kwenda kuwauza kama wafanyakazi wa ndani au makahaba kama UngaUnga
 
Last edited by a moderator:
Kwa lugha nyepesi ni kwamba ukiajiriwa maana yake umeshindwa kujitegemea kwa ujuzi wako (yaani hujui ufanyie nini) hivyo umeona uukabidhi ujuzi wako kwa wenye "akili na uwezo" wa kuupangia matumizi ya huo ujuzi wako.

Ndio maana licha ya kwamba elimu ni yako wewe, maarifa ni yako wewe, vyeti ni vyako wewe; na kazi unafanya wewe; lakini hao waliokuajiri ndio wanakuamulia kiasi gani wakulipe! Si hivyo tu bali pia wanao uhuru wa kukupiga mkwara, kukutishia na hata kukufukuza muda wowote (utakapowakosea, watakapojisikia ama watakapokuchoka)! Nini nakwambia? Kama umeajiriwa, usiridhike wala usibweteke na mshahara pekee kwa 100%, hebu jiongeze aiseee, una uwezo wa kuzalisha zaidi sambamba na mshahara (waliojisikia) kukulipa.

Usiufunge uchumi wako kwenye gereza la ajira, fikiria zaidi ya ajira maana hao waliokuajiri nakuthibitishia HAKUNA mwenye mpango mzuri na "future" yako, zaidi sana wanaihujumu "future" yako!

Nimemaliza! USHAURI WANGU ANZA KUAJIRIWA KAMA MUWEKEZAJI TU ILI UJIAJIRI NA KUAJIRI WENGINE.

We nuna weee, kasirika weee, vimba weee mpaka upasuke, lakini kidonge hicho kimeze japo kichungu, ndiyo dawa tena utafanyaje, ila mwisho wa siku uwe na SIKU NJEMA ili ukawaze na kuwazua vizuri.

JIPATIE NAKALA YAKO MAPEMA..
View attachment 307669
Mkuu umepost mada nzuri,lkn naomba nikusahihishe kidogo,Kwanza kwenye maneno yako ya Mwanzo kwamba mtu ukiajiriwa basi umeshindwa kuitumia taaluma yako,sivyo,nakwambia sivyo kwasababu zipo taaluma ambazo ni lazima uajiriwe mf.wewe umesomea mafunzo ya jeshi utajiajirije hapo??umesomea mambo ya hali ya hewa utajiajirije??,umesomea political science utajiajirije kwa mujibu wa taaluma yako??,Umesomea sociology utajiajirije kwa mujibu wa sociology???,Sehemu nyingine uliyokosea ni hapo mwishoni,hayo si maneno mazuri,JF watu wako timamu ukieleza jambo kwa lugha ya ufasaha tu unaeleweka siyo mpaka udharau watu kwa maneno ya hovyo ndipo wakuelewe,Ukute wewe mwenyewe una mradi wa kawaida tu lkn unavyodharau ambao hawajajiajiri looohh!!.
 
Inawezekana kabisaa hata kampuni ya ulinzi na zaid ya hapo..
Hivi unadhani kila anayehitimu mafunzo ya Uaskari angekuwa na Mawazo ya Kufungua Kampuni za Ulinzi hao wa kuwaajiri kwenye kampuni zao wangewatoa wapi?? maana kila mhitimu angesema naenda kufungua Kampuni sasa nani wangemuajiri??,na Serikali ingeajiri nani kuwa Mlinzi wa Raia???,Jamani hiyo ndo Nature ilivyo,Lazima wawepo Mabosi na wadogo yaani wakuajiriwa,hilo halikwepeki,na Ukifanikiwa kuajiri basi Usimdharau yule uliyemwajiri kwa muona mjinga,maana yeye ndo anakufanya wewe uitwe Muajiri.
 
Naona hutaki kuifikirisha ubongo wako. Udhaifu uliopo kwenye hayo makampuni unaweza kuufanya ukawa ndio stregth kwako na ukawa kampuni kubwa tu...Ukiufikirisha ubongo utang'amua mengi zaid
 
Tusijitoe ufaham, ni kweli ukiajiriwa unakua chini ya mwajiri lakini kuna ajira zina maslahi na marupurupu makubwa na ya uhakika.
Nakubaliana na mleta mada kwa upande wa walio wengi ambao kipato hakiendani na matumizi au uhalisia wa maisha, kwa mfano mtu unalipwa 450,000 au 600,000 unatakiwa ulipe kodi, usafiri, chakula na mambo mengine mengi kwa mjini itakua ni shida na karaha hata ajira hauwezi kuifurahia. Hapo ni lazima utafute njia mbadala ya kukupatia kipato.

Swali langu kwa Joealexist, unafanya kitu gani kinachokuingizia kipato ambacho sio ajira na nje ya biashara ya hii kitabu? Tuanzie hapo ili kuweza kupata picha ya nini cha kutegemea kwenye hicho kitabu.
 
Last edited by a moderator:
Naona hutaki kuifikirisha ubongo wako. Udhaifu uliopo kwenye hayo makampuni unaweza kuufanya ukawa ndio stregth kwako na ukawa kampuni kubwa tu...Ukiufikirisha ubongo utang'amua mengi zaid
Asante mkuu.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom