Soma hapa unaweza kujifunza kitu

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,322
33,126
SOMA HAPA UTAWEZA KUJIFUNZA KITU

Mwalimu mmoja wa Darasa aliwaiita wanafunzi wake akawaambia ''Kesho kila
mwanafunzi aje na nyanya kulingana na idadi ya watu anaowachukia, yani kama unamchukia mtu mmoja uje na nyanya moja kama ni wawili basi njoo na nyanya mbili hivyo hivyo. Nyanya hizo mtazibeba kwenye mabegi yenu ya kubebea madaftari na vitu vingine vya shule.

''Wanafunzi wakakubali afu kesho yake wanafunzi wakazibeba zile nyanya vizuri kabisa wengine walibeba moja,wengine mbili na wengine nyingi sana.

Kama mwalimu alivyosema zile nyanya zikapewa majina ya watu ambao wanafunzi wanawachukia.

Baada ya kuzipa hizo nyanya majina mwalimu akawaambia kila mwanafunzi azirudishie nyanya zake kwenye begi lake afu aziache humo humo ndani ya begi kila siku awe anakuja nazo shuleni na kurudi nazo.

Baada ya siku kadhaa wanafunzi wakaanza kulalamika hasa wale waliobeba nyanya nyingi kuwa nyanya ni nzito sana na zinatoa harufu mbaya na zinaharibu vitu vyao vizuri walivyoweka kwenye mabegi.

Mwalimu akawaambia hivi ndivyo ilivyo mtu unapoweka watu moyoni usiowapenda. kama mtu huwezi kuvumilia kukaa na harufu ya nyanya kwenye begi vipi kuhusu madhara ambayo moyo unayapata kwa kuubebesha mzigo wa chuki dhidi ya watu.?
Moyo unapata madhara makubwa sana unapobebeshwa chuki kila wakati kila siku moyo unakuwa na chuki na hapo ndipo unaharibika na kusababisha kuharibu hata vitu vingine vizuri vilivyokuwa moyoni.

Moyo ni kama lile begi la kubebea madaftari unahitaji kubeba vitu vizuri na Visalia.
Safisha moyo kwa kusamehe wanaokukosea, jifunze kusamehe maana ni moja ya virutubisho vya moyo wako.
 
Last edited by a moderator:
Unajiumizaje,wakati yeye mwenyewe ndiye amekukwaza na wakati mwingine amefanyia ubaya wa hali ya juu,sasa utajitia kumpenda mtu wa namna hadi akudhuru kabisa,Mimi siwezi unafiki wa hivyo
hujui tu kasome psychology ukimchukia haikusaiidii chochote sana unajiumiza moyo ila ukimpenda yaani unajisikia bariiid na kumchukia mtu akikukosea waweza kumchukia labda kwa mda mfupi lakini ukiona hutak kumsamehe ujue wewe una roho mbaya
 
Unajiumizaje,wakati yeye mwenyewe ndiye amekukwaza na wakati mwingine amefanyia ubaya wa hali ya juu,sasa utajitia kumpenda mtu wa namna hadi akudhuru kabisa,Mimi siwezi unafiki wa h

Acha unafiki,katika zama hizi hakuna mwanadamu anayeweza kusamehe kila ubaya anaofanyiwa isipokuwa kuna kiwango cha Yale uliyofanyiwa
usiseme hakuna wapo ila wewe tu si mmoja wao,kwani mkuu we unaamini uwepo wa Mungu 'The almighty'?
 
Back
Top Bottom