IMENICHUKUA muda kuandika andiko hili gazetini kutokana na kutokuwa nimeamini kile anachodaiwa kufanya Mwenyekiti wa Mkoa wa Arusha wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kaka na rafiki yangu, Samson Mwigamba, ambaye sasa amesimamishwa uongozi.
Si kwamba siamini kwa sababu Mwigamba ni malaika hawezi kufanya makosa, la hasha! Isipokuwa nilitaka kwanza kusikia kauli yake ya utetezi wa kile kilichomtokea ili nipime kama alikuwa sahihi, alisingiziwa ama aliteleza.
Nilipigiwa simu Jumamosi iliyopita na mwanahabari mwenzangu kutoka jijini Arusha, akinieleza kuwa Mwigamba ameibua taharuki ukumbini baada ya kubainika na kukiri mbele ya kikao kuwa aliandika na kusambaza ujumbe wa uongo wa kuwadhalilisha viongozi wa kitaifa wa chama chake kwenye mtandao wa kijamii wa Jamii Forum.
Kama Yesu Kristo alivyohamaki alipobaini kuwa msaliti wake ni miongoni mwa wanafunzi wake, Yuda, nami ndivyo nilivyostuka nilipopokea taarifa ile kutokana na nilivyomfahamu Mwigamba kwa uadilifu na mapenzi kwa chama chake, hivyo sikutegemea kabisa kama anaweza kuingizwa mtego wa kucheza mchazo kama huo.
Nilijaribu kumpigia simu, lakini kwa bahati mbaya wakati huo ilionyesha inatumika kwa muda mrefu, hivyo nikaendelea kutafakari mwenyewe ni kwanini Mwigamba ajifiche wakati ana taarifa nzito kwa chama chake?
Nikajiuliza huyu ni kiongozi anayeingia kwenye vikao vikuu vya chama, ni kwanini masuala hayo hakuyahoji huko? Pili nikawaza kuwa hata kama ni kuogopa kutazamwa vibaya na wenzake au kufukuzwa, ni kwanini asingejitokeza kwenye vyombo vya habari kuanika hayo anayodhani ni bomu ndani ya chama ili wanachama wachukue hatua?
Sikupata majibu ya maswali yangu, hata baada ya kuwa nimezungumza na viongozi kadhaa wa CHADEMA hadi Jumatatu baada ya Mwigamba kuzungumza na waandishi wa habari na kueleza kile alichokiita siri iliyofichika.
Baada ya kuwa nimemsikiliza kwa makini kaka yangu Mwigamba, nilibaini kuwa utetezi wake hauna mashiko hata chembe, isipokuwa angekwenda moja kwa moja kwa kuwaomba radhi wanachama wa CHADEMA na viongozi wao kuwa aliteleza kwa kile alichokifanya.
Mwigamba alisema kuwa alilazimika kutumia njia hiyo ya kujificha ili kufikisha ujumbe kwa wahusika hatua ziweze kuchukuliwa kwani angetumia njia ya vikao kuhoji angeonekana msaliti na asingepewa nafasi.
Kwa mujibu wa Mwigamba, ndani ya CHADEMA wenye ubavu wa kuhoji au kukosoa bila kunyooshewa kidole ni Dk. Kitila Mkumbo, Prof. Mwesiga Baregu na Mzee Shilungushela, kwamba wengine wanaonekana wasaliti.
Yawezekana kaka yangu Mwigamba alikuwa na hoja na tuhuma za kweli, lakini njia aliyotumia si sahihi. Neno moja ninaloweza kumshauri kaka yangu ni hili la kwamba; Shujaa haogopi vita, anakaa mstari wa mbele, yuko tayari kwa lolote hata kukosana na marafiki zake na hata kupoteza maisha, lakini historia inaandikwa kwake.
Napata shaka kuona kiongozi kama Mwigamba hawezi kuhoji ufisadi wa chama anachodai anakipenda ndani ya vikao, eti anaogopa kuitwa msaliti. Lakini shaka zaidi ni kuona alituma andiko hilo hilo kwenye mitandao baada ya kuwasilisha taarifa ya utendaji wa chama mkoa na kutoa sifa lukuki kwa wake anaogeuka sasa kutwambia ni maadui zake.
Mwanafalsafa wa Kijerumani na mtaalamu wa maadili, Emmanuel Kant, anaamini kuwa The end does not justify the meas, yaani matokeo hayahalalishi njia uliyotumia.
Kant anasema kuwa unaweza kufanya jambo kwa nia njema, lakini matokeo yake yakawa mabaya na yenye madhara.
Hivi ndivyo alivyofanya Mwigamba. Licha ya kupata nafasi ya kukutana na viongozi wakuu wa chama na hivyo kuwa na uwezo wa kueleza madukuduku yake, hakufanya hivyo bali alisubiri kutumia njia ya kujificha kufanya alivyofanya na baadaye alipogundulika ndipo akafichua kwamba ana uadui na mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema.
Kwa mtazamo wangu, kaka yangu Mwigamba, hakuitendea haki CHADEMA, viongozi wake wala wafuasi wake, kwani hata kama hayo aliyoyaandika yana ukweli asilimia 100, kama mwanachama mtiifu, alipaswa kutumia njia sahihi bila kujificha ili kueleza hatua zichukuliwe.
Hawa viongozi wa CHADEMA si malaika, wanaweza kufanya makosa, lakini mtoa tuhuma si shujaa, ana hofu ya kuitwa msaliti na kuonekana mbaya kwa viongozi. Lakini kama nilivyoeleza awali sifa za shujaa kuwa hapaswi kuhofia chochote ilmradi tu anasimamia na kutetea ukweli kwa maslahi ya wengi.