mkuu
Kingcobra unafikiri ujumbe unafika huo? tena usishangae mahali hapo pakawa labda ni Ilula huko Iringa.
nakumbuka kuna mwaka mmoja nilikwenda kwenye sherehe za mwenge kule Tukuyu Rungwe, sijui panaitwa
makandana vile lolest .........
ujumbe wa mwaka huo ulikuwa wanaume kiini cha mabadiliko katika kutokomeza ukimwi. Huwez kuamini sherehe zilifana sana na disco languvu jamani kumbe usiku wengine wakiserebuka wengine wanaendelea na kazi nyingine hatukugundua
asubuhi ndio ikawa balaa uwanja wote ulikuwa umetapakaa condom used. na mgeni wetu mwenge na anatakiwa aangwe kwenda wilaya ya kyela siku hiyo asubuhi, kwa aibu ilibidi tuwaforce wanafunzi waokote manake ni balaa. Tena nashukuru sana enzi hizo mambo ya haki za binadam na watoto hayakuwa yamepamba moto ingekuwa ni leo mbona tungeishia lupango mkuu kwa kuwaokotesha wanafunzi condom chafu?
ujumbe haufiki kabisa kwa watu.