Soma Hapa Kumhusu Flora Mbasha

Lusam

Senior Member
Joined
Apr 4, 2013
Posts
195
Reaction score
88
Habari wana JF. Juzi nilikuja na uzi nikimshambulia Flora Mbasha kwamba hana Mungu ndani yake maana anavunja ndoa yake mwenyewe misili ya mtu ambaye hajawahi kusoma hata fungu moja la Biblia, watu walinishambilia sana. Leo nimeona hii video ya Baba yake mbasha akisema Flora alimchoka mwanangu, inasikitisha sana nasikia kulia nikitafakari mke wako mwenyewe tena wa ndoa akikumaliza huku ukiona.

HITIMISHO
Mungu haabudiwi kwa style ya kuimba kwa kupiga makelele na kukata viuno bali tunamuita Mungu awe ndani yetu kwa kuimba nyimbo za kuabudu, ndio maana katika maisha yangu sijawahi kupenda nyimbo za huyu dada pamoja na Rose Mhando sidhani kama mungu atakua ndani kwa ujinga kama ule wa kupiga kelele na kukata viuno.
 
Ulimaanisha Misri?
 

.........!
 

Ndugu mfalmw Sulemani alicheza lakini cheza yake haikuwa arranged/ planned alijikuta akipata mizuka na kurukaruka kwa furaha kwa matendo makubwa aliyofanyiwa na Mungu, hawa wakina Rose Mhango wana plan in advance jinsi gani atakata viuno na steps atakazocheza na dancers wake. Umeona tofauti?
 
Huyu dada amrudie Mungu hata kwa kufunga na kuomba na sijui kama hata anaomba tena.
 

Wewe naye boya sana hujui hata biblia,unamkosoa mwenzako wewe mwenyewe huijui,aliyecheza hadi nguo kumvuka si sulemani ni daudi,na ujue swala hilo halikumfurahisha Mungu,ndiyo maana aliporudi nyumbani mke wake alimwambia"umefanyaje ubaya huu ukamkosea Mungu?msitumie maandiko kuhalalisha vitu vya kijinga,hivyo viuno vinavyokatwa na hao wanaojiita waimbaji wa injili havimtukuzi Mungu hata kidogo,
Nikuulize swali,uimbaji ni uinjilisti,maana yake kusudi lake namba moja ni kupeleka neno la Mungu kwa watu wasiomwamini Yesu wamwamini watubu wafuate mapito yake ya maisha ya kiroho,sasa hao wanaokatika hawaufikishi ujumbe wa Mungu bali viuno,waseme tu kwamba wanakata viuno kuvutia watu wanunue cd zao,
Paulo anasema hivi,ikiwa tutafanana na mambo ya dunia patakuwa na tofauti gani kati ya nuru na giza?ukiangalia nuru na giza kamwe havichangamani,sasa hao akina rose mhando,frola mbasha na wengine wanatofauti gani na akina diamond,na wengine kama hao?
 

Aisee we ni mchambuzi mpaka nafurahi yaan. Kwel Suleiman ni furaha hadi akashindwa kujizuia ila hawa wa kwetu wanajiandaa kabisa kukata mauno yao. Ila duh uyu Flora kajaa jaa ana kamvuto flani ivi
 
Kuimba kwao kuna tofauti gan na kiduku-au huyo mungu wao ni waina yao min kiduku
 
Hili sakata la Mbasha bado linaendelea?
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…