soma hapa hili lina ukweli wowote? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

soma hapa hili lina ukweli wowote?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by kessy kyomo, Feb 6, 2011.

 1. kessy kyomo

  kessy kyomo Member

  #1
  Feb 6, 2011
  Joined: Feb 1, 2011
  Messages: 72
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 15
  hivi kuna ukweli wowote kuhusu population ya mkoa wa mwanza ni kubwa kuliko population ya chi ya zanzibar kama ni hivyo basi kumbe hata mwanza ni nchi huru kwani tunaona kura za diwani wa bara ni zaidi ya kura za mbunge wa zanzibar nawakilisha wadau:bump:
   
 2. Ukwaju

  Ukwaju JF Bronze Member

  #2
  Feb 6, 2011
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 8,287
  Likes Received: 810
  Trophy Points: 280
  Du unajua leo hayo ndo mambo ya Muungano, toa mawazo tuuvunje Muungano au tutoa mawaziri kutokana na Idadi ya watu kiMkoa, angalia Mkoa wa Kilimanjaro una mawaziri wangapi au viongozi wangapi wenyeviti wa vyama vya upinzani au waliogombea.
  Mwanza changamkeni mmeanzia kwenye Udiwani na Ubunge sasa
   
 3. N

  Nonda JF-Expert Member

  #3
  Feb 6, 2011
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 13,223
  Likes Received: 1,958
  Trophy Points: 280
  Mkuu,
  Mwanza iliungana na Tanganyika? au ni sehemu ya Tanganyika?
  Kwa taarifa tu kama huelewi kuna nchi ya seychelles, unajua population yake?
  BBC News - Seychelles country profile

  pia Cape Verde BBC News - Cape Verde country profile

  Pia Sao Tome
  BBC News - Sao Tome and Principe country profile
  Mauritius
  BBC News - Mauritius country profile

  Gambia
  BBC News - The Gambia country profile

  Haya mkuu, Kessy
  Tueleze Mwanza ilipata uhuru wake mwaka gani? Nani alikuwa waziri mkuu au rais wake wa kwanza?
  Mkuu, Unapoanzisha thread fikiria kwanza unakusudia kufikisha ujumbe gani? Zanzibar nchi, iliungana na Tanganyika nchi katika baadhi ya mambo, kumi na moja, Tanzania haijawahi kuwa nchi moja,ila kiusanii tu.
  Wingi au uchache wa population sio kigezo cha kuwa sehemu ni nchi au mkoa.
  Watawala wetu wanatuchanganya sana mpaka tunachanganyikiwa!!!!
   
 4. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #4
  Feb 6, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Ni kweli Mwanza wapo wengi sana, hata Mkoa wa Geita tu ni zaidi ya zanzibar... lakini hoja yako haina mashiko; kuna nchi inaitwa samoa ina watu laki moja, kuna St. Kits and Vincent ina watu chini ya laki moja nk

  Tusiangalie one factor in our analysis, kumbuka kwamba historia ni moja ya sababu kubwa ya kuwapo nchi kama zilivyo
   
 5. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #5
  Feb 6, 2011
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  Kwa kufuata hiyo analysis yako Mwanza ni nchi huru, na iombe kuanza kupiga kura za rais wake na kutangaza baraza lake la mawaziri.
   
 6. Donyongijape

  Donyongijape JF-Expert Member

  #6
  Feb 6, 2011
  Joined: May 28, 2010
  Messages: 1,451
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 160
  Hata Tanga, Mbeya, Arusha, Kagera, Iringa..zote zinaifunika Zenj!..lakini hili haliwezi kuifanya iwe na justification ya kuwa nchi. Mbona USA ina majimbo kibao na yana watu kuliko hata Tanzania lakini HATUSIKII yakitaka kuwa Nchi kama Tanzania,Mauritius au hata Zbar..!?
   
 7. Dumelambegu

  Dumelambegu JF-Expert Member

  #7
  Feb 6, 2011
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 1,052
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Kale kanchi kana watu wachache sana. Lakini si unajua tena uswahilini, kelele nyiiiiiiiiiingi utafikiri watu wengi kumbe hata Dar imewazidi. Kangekuwa ni kanchi independent halafu bahati mbaya tukakorofishana nako, tunachofanya watanganyika ni kuhamia wote kule basi! Haina haja hata ya kutumia silaha yoyote.
   
 8. N

  Nonda JF-Expert Member

  #8
  Feb 6, 2011
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 13,223
  Likes Received: 1,958
  Trophy Points: 280
  Mkuu,
  kweli population ya mwanza ni kubwa kuliko population ya nchi ya Zanzibar.Ambayo ni moja katika ya nchi mbili zilizounda Jamhuri ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar(Tanzania).

  Kumbe hata Mwanza ni nchi huru....huu unaweza kuwa ni utashi lakini si ukweli. Ili mwanza iwe nchi huru, inabidi Muungano wa Tanzania uvunjwe...faida ambayo wengi hatuioni ya muungano ni kuwa muungano umeisaidia Tanganyika kutokumeguka kuwa nchi mbili ,tatu, nne ndani yake, siku Zanzibar ikijitoa muungano basi kweli watu wa Mwanza, Mikoa ya kusini nk watataka kujitenga kama ilivyotokea kwa Sudan ya Kusini. Mwalimu was smart enough kulijua hili ndio maana aliing'ang'ania Zanzibar na kuwa na mpango wa kuimeza ili watu wawe na fikra kama hizi zako mkuu...usahau matatizo yaliyotuzunguka na tuone Zanzibar kuwa ni kero.

  Lakini muungano ukivunjika basi japo serikali za majimbo tutazipata Tanganyika,(bara), na ule ubaguzi uliojificha kwa muda mrefu wa kidini na kikabila utaibuka kwa nguvu ya ajabu.
   
 9. k

  kayumba JF-Expert Member

  #9
  Feb 6, 2011
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 654
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35

  Mkuu kuwa nchi huru hakutegemei idadi ya watu, au umesahau wachina ni wengi kuliko wa Afrika wote hapa duniani. Lakini mbona Afrika ina nchi karibu 54 wakati CHINA ni nchi moja tu!
   
 10. Straight corner

  Straight corner JF-Expert Member

  #10
  Feb 6, 2011
  Joined: Nov 18, 2010
  Messages: 370
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Mkuu ukitaka kulinganisha population ya Z'bar ili kuipa mikoa ya bara uhalali wa kuwa nchi basi mikoa mingi tu itapata hadhi hiyo.
  Me nadhani usijenge msimamo huo akilini kwako otherwise utaanza kulinganisha na nchi zingine na Z'bar!
  My take:
  Tuiache Z'bar ibaki Z'bar!
   
 11. Likasu

  Likasu JF-Expert Member

  #11
  Feb 6, 2011
  Joined: Jan 18, 2011
  Messages: 694
  Likes Received: 94
  Trophy Points: 45
  Elimu ya uraia ni muhimu. Hv ww unafikiri ili sehemu iwe nchi inabidi iwe na watu wangapi ? Haupo sahihi kabisa ndugu yangu. Nchi inaweza kuwa hata na watu 10,000 ilimradi inakidhi vigezo (jitahidi uvijue) vya kimataifa vya kuwa nchi.
   
 12. N

  Nonda JF-Expert Member

  #12
  Feb 6, 2011
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 13,223
  Likes Received: 1,958
  Trophy Points: 280
  Mkuu,
  Leo umeamua kufurahisha JF?
  Tembelea hapa.
  https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/108530-salamu.html#post1590180
   
 13. mchillo

  mchillo JF-Expert Member

  #13
  Feb 6, 2011
  Joined: Oct 13, 2010
  Messages: 433
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  Ipo pia nchi inaitwa Vanuatu ina population isiyozidi 50,000. Lakini ina Rais akija hapa atapigiwa mizinga 21, kukagua Gwaride na ina kiti UN.

   
 14. M

  Madcheda JF-Expert Member

  #14
  Feb 6, 2011
  Joined: Feb 18, 2009
  Messages: 416
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  Aise kweli china inabidi iwe dunia mana ina watu 1.5 billion
   
 15. M

  Madcheda JF-Expert Member

  #15
  Feb 6, 2011
  Joined: Feb 18, 2009
  Messages: 416
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  Kaka kuna vatican ina watu 750 nazan ila ni nchi,kuna kiribati inawatu 20,000 cjui ila ni nchi. Huyu bwana si mzima kusema nchi ni idadi ya watu
   
 16. kessy kyomo

  kessy kyomo Member

  #16
  Feb 6, 2011
  Joined: Feb 1, 2011
  Messages: 72
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 15
  lakini mbona rasilimali za nchi tunagawana sawa kwa sawa sio kwa kuangaria wingi watu naikiwa hivyo mbona msaada ukija kwa ajiri ya tanzania tunagawana nusu kwa nusu nandugu zetu wa zenji na ukija msaada kwa ajiri ya zenji wanapiga kimya msaada wote kwa maana hiyo kuna upande fulani unanyonya upande mwingine ahksante wadau nilikuwepo
   
 17. Arafat

  Arafat JF-Expert Member

  #17
  Feb 7, 2011
  Joined: Nov 17, 2009
  Messages: 2,582
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 0
  Mhmmm Nonda umechemka hapo, Mwalimu aliongelea Zenj; wewe pambana nao lakini husiongeze uongo, Nonda!! .
   
 18. M

  Marytina JF-Expert Member

  #18
  Feb 7, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 7,037
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145
  ni kweli ndio maana CCM wanaumia sana kuipoteza kanda ya Ziwa ambayo kama wote wakiamua kumpigia kura mtu wao basi lazima ashinde(bila uchakachuaji)
  CUF wanawabunge wengi ila waulize wanawakilisha watu wangapi mbona utashangaa? mshindi wa ubunge PEMBA kura 2834 hizo ni kura za mjumbe wa mtaa MABATINI MWANZA.
   
 19. N

  Nonda JF-Expert Member

  #19
  Feb 10, 2011
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 13,223
  Likes Received: 1,958
  Trophy Points: 280
  Mkuu,
  nakuomba unioneshe wapi nimechemka na wapi nimesema uongo....ili niweze kujikosoa na kujifunza.
  natanguliza shukrani zangu kwako mkuu.
   
 20. N

  Nonda JF-Expert Member

  #20
  Feb 10, 2011
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 13,223
  Likes Received: 1,958
  Trophy Points: 280
  mkuu,
  soma post 3...lakini ukiendeleza mantiki yako chukua China na India halafu ilinganishe population ya Tanzania na hizo nchi, jee katika ulinganisho huo bado utapenda Tanzania iwe ni nchi?
   
Loading...