Solar (Umeme jua) teknolojia mpya ya umeme nafuu

Mtakanuhu

Member
Sep 19, 2018
44
56
Solar (Umeme jua) teknolojia mpya ya umeme nafuu

Tafiti zinaonesha kuwa asilimia 36 tu ya Watanzania ndiyo wanaopata umeme huku wale waishio maeneo ya vijijini wakiwa nyuma zaidi. Kuna changamoto mbalimbali zilizokwamisha watu wa vijijini nchini Tanzania kupata vyanzo vya uhakika vya nishati au teknolojia ya umeme. (Kama watanzania tuko 50,000,000, wenye kupata huduma ya umeme ni 18,000,000; wasiopata umeme ni 32,000,000)

Kutokana na sababu hiyo, sehemu kubwa ya watu wa maeneo hayo, hutumia mafuta ya taa na kuni kwa ajili ya kupata nishati ya mwanga. Matumizi ya vyanzo hivyo vya nishati huzalisha hewa yenye sumu, ambayo huchangia mabadiliko yasiyotakiwa ya tabia nchi na kupelekea utoaji wa moshi ambao unasemekana kusababisha saratani.

Wanawake na watoto ni waathirika wakuu wa saratani inayosababishwa na moshi huo wenye sumu. Ijapokuwa matumizi ya mifumo ya nishati inayotokana na nguvu ya jua yameongezeka kwa kasi katika maeneo mengi, kuna vikwazo vikubwa vinavyokwamisha nishati hiyo kusambaa vya kiwango cha kutosha. Watu wengi hawawezi kuhimili bei ya mifumo ya nishati ya jua, au wana wasiwasi kuwa mifumo hiyo itashindwa kufanya kazi au kukosa huduma za uhakika litokeapo tatizo.

Lakini pia, ukosefu wa nishati ni moja ya visababishi vikuu vya umasikini, kutokana na ukubwa wa gharama ya mafuta. Bidhaa hizi pia kama tulivyoona ni hatari na huharibu afya. Kwa mujibu wa matokeo ya utafiti wa mwaka 2012, ugumu wa kuyafikia maeneo ya vijijini unafanya usambazaji wa umeme kupitia mfumo wa gridi kuwa mgumu na hivyo kuondoa manufaa ya kiuchumi. Katika kile, ambacho kinaweza kuonekana kama ni mafanikio mengine katika utekelezaji wa juhudi za serikali za kuhakikisha watanzania wengi wanapata umeme, kampuni inayoongoza nchini Tanzania kwa usambazaji wa Teknolojia ya Umeme wa Jua, Mobisol, ilianzisha huduma hiyo ya usambazaji wa vifaa hivyo zaidi ya miaka 3 iliyopita.

Mobisol imefanikiwa kuwa mbele katika utoaji wa bidhaa bora zilizo suluhu ya soko la nishati ya jua. Wateja wake wanapata huduma ya uhakika na kwa utaratibu wa malipo ulio rafiki. Teknolojia hii imejaribiwa nchini hapa na niina uhakika ni suluhisho kwa maeneo yasiyofikiwa na gridi vijijini nchini Tanzania na Afrika Mashariki. Mobisol wana mfumo wa malipo, ambao unaruhusu wateja kulipa amana na kiasi kilichosalia kulipwa kipindi cha miezi 36 hadi 48 ili kumsaidia mteja kutobeba mzigo wa kulipa mara moja. Huu ni mfumo wa lipa kadiri ya unavyotumia, ambao mteja anamiliki mfumo wa umeme wa jua baada ya kumaliza kulipa sehemu ya fedha iliyobakia. Bidhaa pia imetengenezwa kwa namna ya kuendana na mahitaji ya makundi tofauti ya jamii za vijijini na hata za mjini kwa vile inakuja kwa ukubwa tofauti. Vifaa hivi uwezo wa nishati kuanzia matumizi ya mwanga na kuchaji simu hadi kuwezesha vifaa vya umene kama vile runinga; feni, jokofu, sabufa, kompyuta mpakato na kadhalika.

Natoa rahi kwako wewe unayesoma hapa kwamba kuna wimbi la msambao wa bidhaa hafifu na za bei ya chee, vifaa hivi vinatishia uhalali wa mifumo ya umeme wa jua wa majumbani kwa vile wateja kwa idadi kubwa, wanakuwa hawapokei huduma inayoendana na thamani ya fedha yao waliyoivujia jasho. Kwa sababu hiyo, kuna umuhimu mkubwa kwa watu wetu kujenga tabia ya kununua bidhaa wanazozifahamu.

Nina uhakika wateja watapata fursa nzuri ya kupata bidhaa mbalimbali katika mfumo mmoja zilizo suluhisho bora la nishati na hivyo kuongeza maradufu thamani ya fedha yao. Hebu tuwe raia wawajibikaji na watiifu wa sheria zinazoongoza sekta ya umeme mbadala na maadili ya kibiashara. Onesha mfano kwa kuwajali ndugu zako walioko vijijini kwa kuwanunulia mitambo ya Mobisol ili waondokane na adha ya nishati ya mwanga.

Wasiliana nasi ili uweze kupewa utaratibu wa kukopeshwa mitambo ya Mobisol na uanze kulipa kidogo kidogo sasa. Kuna manufaa mengi unapokuwa umejiunga na Mobisol

Piga simu nambari 0754533543 / 0655-533543
 
Vipi ni zile solar za kulipia kwa mwezi kama vocha au ni ya vipi
 
Vipi ni zile solar za kulipia kwa mwezi kama vocha au ni ya vipi
Kama una cash; unaweza kulipa kuaachana nao.
Kama una hela kidogo; unatanguliza advance then balance unaendelea kulipia mdogo mdogo. Nashindwa kukwambia kuwa ni ya kulipia kama vocha kwa sababu vocha usipolipa hupati huduma ila hunyanganwi laini wala simu.
 
Kama una cash; unaweza kulipa kuaachana nao.
Kama una hela kidogo; unatanguliza advance then balance unaendelea kulipia mdogo mdogo. Nashindwa kukwambia kuwa ni ya kulipia kama vocha kwa sababu vocha usipolipa hupati huduma ila hunyanganwi laini wala simu.
Nitakupm kuna dogo ananisumbua nimnunulie solar kapelekwa chimbo moja matata na mm sina uzoefu na haya mambo
 
Back
Top Bottom