Ila nakushauri,uende duka fulani ckumbuki mtaa ila ni watu wa AFRICAN CABLES,LIPO kariakoo mtaa unaouza vifaa vya umeme nyuma ya tahafifu kama unaijua hiyo bookshop kubwa ya kariakoo,pita pembeni ya hilo duka na ingia kushoto mtaa wa kwanza na hilo duka lipo upande wako wa kulia,utaona tangazo lao la african cables, na vifaa mbali mbali
Ndugu zangu,
Natafuta information za kampuni yeyote inayouza vifaa vya umeme wa jua kwa bei nafuu. Nataka nifunge umeme wa jua kijijini kwa sabau umeme wa TANESCO ni garama sana hasa seheu inayohitaji nguzo zaidi ya moja.
Vifaa vinavyotegemea kutumia umeme ni Taa 10 za WH zisizozidi 35, TV ndogo, kucharg simu, Redio na pasi siku moja moja.
Nitashukuru sana nikipata information za bei na vifaa vinavyohitajika. Mimi niko Dar es Salaam ila hata kama vitapatikana hapa Dar nitavisafirisha kwenda Kilimanjaro kijijini kuvifunga.
Natanguliza shukrani zangu kwa msaada wako
Asante Audax kwa kuwa wa msaada kwa mwenzetu. Ila Dar na miji yetu inahitaji kuwa na physical addresses. Hatuwezi kukaa tu bila coordinates.
Ningependa mno kuachana moja kwa moja na TANESCO. Haiwezekani kuisha kwa furaha na huku unategemea umeme wa mambumbu wa TANESCO.
Nimeuliza hapa, siku za nyuma, na naomba kuuliza tena: kama kuna mtu amewahi kuweka nyumbani kwake umeme wa jua wa kutosha shughuli zote za kawaida za nyumbani, basi tafadahali atupe experience yake.
Au kama kuna mtaalamu anayeweza kutupa quotation (for discussion) ya vifaa vya meme wa jua wa kutosha taa za nyumba ya kawaida, TV, pasi, jiko, vifaa vya nyumbani kama blender, etc, basi tafadhal tusaidie.
Ni lengo langu kuachana permanently, na TANESCO. Najua initial costs zitakuwa kubwa, lakini ningependa some estimates.
Mkuu AM,
Niliwahi kukutana rafiki yangu ambaye anaishi nchi moja ya Ulaya, anatumia umeme wa solar kwa matumizi mengi ikiwa ni pamoja na kupasha joto nyumba wakati wa majira ya baridi. Alinambia kuwa gharama ya vifaa vyote ilikuwa kama $5000 (karibia 6.5m)
Kuna njia nyingine niliyojifunzia wakati wa shida ya umeme Bongo. Unanunua mashine hii;
power inverter, kwa matumizi uliyosema, waweza chukua inayozalisha 1000 watts tu, ambayo kwa bei ya mwaka jana ilikuwa approx shs laki tano, kisha unanunua na battery zako mbili/tatu za namna hii N90;
unaunganisha kwenye umeme nyumbani kwako, aah... (unatumia umeme wa battery) unawasahau Tanesco!
Unahitaji Battery mbili/tatu, sababu unatumia moja kila baada ya siku/tatu, nyingine unaipeleka ku chajiwa...na bei ya ku charge battery haizidi sh1000. Ukibahatika kupata Solar panels, hiyo adha ya kucharge battery kwa umeme wa Tanesco pia itaisha.
Muhimu, ni kuangalia genuine product ni ipi, feki ni ipi toka China.