We kasome 2 uje 2sugue wote benchi huku kitaa...
Kusugua benchi wakati una shahada ya sheria ni kiashiria cha kutokomaa kwako kisheria kwa vitendo. kuwa mwanasheria sio lazima uajiriwe mahakamani, kwenye ofisi za mashirika, kwa mwanasheria wa serikali etc. Elimu ya sheria uliyonayounaweza kuitumia kwa faida yako na mamalioni ya watanzania ambao huduma za sheria kwao ni kama mbingu na nchi.
Unaweza kuwa paralegal, unaweza kuanzisha NGO za kuelimisha mamia ya raia haki zao za ardhi, mikataba, uraia etc, kuna mashirika mengi tu yanaweza kutoa funds ukiingia kwenye njia hiyo.
Usifikirie sana kufanya kazi au kuajiriwa kwenye ofisi za wanaosheria zinavuma haitakuwa kwako kufanikiwa.
Kweli kabisa, mfundishe mtu kuvua samaki itamsaidia milele badala ya kumpatia samaki ambaye atamla kwa siku moja kisha akarudi tena kesho yake kuomba samaki!
Unaweza kuwa paralegal, unaweza kuanzisha NGO za kuelimisha mamia ya raia haki zao za ardhi, mikataba, uraia etc, kuna mashirika mengi tu yanaweza kutoa funds ukiingia kwenye njia hiyo.
usiogope mdogo wangu waambie nyumbani wakulipie ada then chakula ntakuwekea bili kwa CHACHA au DADA GIFTI,stationery utaenda pale KYUNGU napo ntwaweka bili,bia utakunywa GREEN au kwa BAUNSA, watto wazuri pale MATOLA na NYERERE hallMie ndo nme2piwa LLB MZUMBE lakn mkopo NO LOAN!
Duh! Yaani uwe paralegal huku una LLB? Aisee.....no wonder why.......
Ungejua idadi ya wenye LLB walio barabarani usingeshangaa ndugu yangu. Idadi ya wanafunzi wanaomaliza LLB kwa mwaka hailingani kabisa na soko la ajira katika fani hiyo.
Mfano wa haraka :
university of Dar es salaam 200
Mzumbe Morogoro Campus 400
Mzumbe Mbeya Campus 100
Tumaini DSM 300
Tumaini Iringa 200
Makumira 100
Ruaha University Mwanza 200
Ruaha University Iringa 200
Sebastian Kolowa Lushoto 50
Zanzibar University 50
University of Dodoma 300
Open University of Tanzania 200
Total 2,300
Wahitimu kutoka vyo vya nje India, marekani uganda kenya etc wanafika 2600, namba hiyo utawaweka wapi wote hawa
hakuna course bora kuliko nyingine..cha msingi utoke na GPA nzuri. Thats it.
Faymario, kama unataka kusoma LL.B ili kupata ajira haraka, uko kwenye wrong professional. Nilidhani wewe ni mkureketwa wa haki, hivyo unasoma ili kuwasaidia Watanzania kupata haki zao!, kumbe wewe unaitafuta LL.B ili uajiriwe?.jamani naomba kuuliza nataka nikasome sheria najua soko lake gumu lakini vitu gani vya ziada ambavyo vinaweza kunisaidia kupata ajira haraka(kufikiriwa pale nitakapoomba kazi),mfano nilisikia watu wanao soma international relations ni vizuri kujua ligha za kigeni kama french,arab.madiodo gani yanahitajika kwenye sheria?
jamani naomba kuuliza nataka nikasome sheria najua soko lake gumu lakini vitu gani vya ziada ambavyo vinaweza kunisaidia kupata ajira haraka(kufikiriwa pale nitakapoomba kazi),mfano nilisikia watu wanao soma international relations ni vizuri kujua ligha za kigeni kama french,arab.madiodo gani yanahitajika kwenye sheria?
Mimi nadhani kulingana na idadi ya wati inavyozidi kuongezeka na changamoto zinavyozidi kuongezeka ndivyo mahitaji pia yanavyozidi kuongezeka. Ukisikia watu wenye matatizo ya kisheria yanazidi idadi ya wahitimu kila mwaka. Hapa Tanzania tuna mahitaji mengi yanayohitaji wanasheria kuliko idadi ya watu waliopo. Hivyo, kama ni changamoto ya ajira hiyo ni kwa kila fani siyo sheria tu. Na hata kama ajira hi haba, haina maana kuwa ukihitimu na kuwa mwanasheria basi utakosa ajira.
Chukulia katika eneo la biashara kuna wanaofirisika na kuna wanaokuwa matajiri. Katika maisha ya ndoa, kuna wale ambao ndoa zao zinavunjika na kuna wanaoa au kuolewa. Hivyo, kwa mtazamo wangu hakuna mtu ambaye yuko kwenye loss. Kinachotakiwa ni competency. Mwanasheria mzuri na mwadilifu hata kama kuna tatizo la ajira yeye anakuwa marketable. Si ulishaona mtu anauza duka na bidhaa zote kwa vile anadhani hakuna wateja na kwenda kufungua sehemu nyingine na wakati huohuo mtu mwingine anayenunua duka na bidhaa hizo yeye anapata wateja? Hivi ndivyo life ilivyo. Kama una kipaji cha kuwa mwanasheria - unapenda kuwa mwanasheria na unaweza kuwa mwanasheria mzuri, piga moyo konde, the future will unfold for you!
Fanya utafiti kwanza, nenda Kisutu ona aina ya watu na aina ya kesi za jina na madai ni tofauti kabisa na kesi zilizopo Mahakama ya kinondoni na Temeke. Vilevile mahakama kuu kesi zilizopo kanda ya Sumbawanga haziwezi kuwa sawa hatakidogo na kesi zilizopo dar es salaam. Katika mifano hiyo miwili Kanda ya DSM na Mahakama ya Kisutu ziko tofauti sababu kubwa ni uwezo wa kiuchumi unafanya sheria zishamiri. Mtu hawezi kukubali kulala njaa kisa ametoa hela kwa wakili haitatokea. Wenye shibe na excess ndo wanaweza litigation. Maskini hawezi kulitigate.
Idadi ya watu sio Kigezo hata siku moja usidanganyike.
Fanya utafiti kwanza, nenda Kisutu ona aina ya watu na aina ya kesi za jina na madai ni tofauti kabisa na kesi zilizopo Mahakama ya kinondoni na Temeke. Vilevile mahakama kuu kesi zilizopo kanda ya Sumbawanga haziwezi kuwa sawa hatakidogo na kesi zilizopo dar es salaam. Katika mifano hiyo miwili Kanda ya DSM na Mahakama ya Kisutu ziko tofauti sababu kubwa ni uwezo wa kiuchumi unafanya sheria zishamiri. Mtu hawezi kukubali kulala njaa kisa ametoa hela kwa wakili haitatokea. Wenye shibe na excess ndo wanaweza litigation. Maskini hawezi kulitigate.
Idadi ya watu sio Kigezo hata siku moja usidanganyike.