Soko la ufuta likoje kwenye mkoa uliko?

Soko la ufuta likoje kwenye mkoa uliko?

Ndio maana Heche anapinga huu ujinga wa stakabadhi gharani. Ni unyonyaji kwa mkulima na kuwanufaisha watu ata wasio jua ugumu wa kilimo.
Anataka turudi kule kwa kuibia wakulima?

Wewe Lazima utakua dalali
 
Vumilieni wakusanye hela ya uchaguzi,mwakani litapanda bei.
 
Mwaka huu mbona ilishajulikana....wanunuzi ndio hawajatokea.
Mbaaazi na korosho kilio kitakuwa hikihiki.
Wakulima wenzangu tusikate Tamaa mwakani bei inarud kuwa juu maradufu.
 
Bei ya jana mnada wa Songea vijijini 3700. .. choma choma washastuka minada inashuka tu, kutoka bei 4540 songwe week tatu zilizopita leo 3700.... Chomachoma wakinunua hadi3400. Ila kwasasa chomachoma 2500.... Kuna uwezekano soko likashuka zaidi kwasababu ufuta upo mwingi sana kuanzia kilwa, Ruangwa,liwale na tunduru Ruvuma...

Soko la dar limeshuka zaidi hadi 3500. Wananunua wachina... Ila wanapata ufuta unaotoka moro kilosa,, ila kwa kusini kote ni stakabadh ghala Tu, hauwezi kusafirisha kupeleka dar.

Kama una pesa zako tulia tu kwanza, soko likiyumba katikat hapa ya mwenz wa sita.. chomachoma bei zitashuka zaidi hapo hapo ndo wataalamu wa hizi kazi ndo wanaingia porini kuzoa ufuta kwa bei rahis ya 2000, mwishoni bei inakuja kustuka hata kwa 3500-4000.
Samahani mkuu, choma choma ndo nani?
 
1. Kama shamba ni la kukodi
Ekari moja = 30,000
2.Mbegu kilo 3 per ekari @4000
3.palilizi per ekta = 25,000
4. Uvunaji= 18, 000 per ekta
5. Upandaji =2,500 per ekta
6.kupiga( kukung'unta) = 3000 per gunia
7.kulima kwa trekta = 40, 000 per ekta

Gharama za msingi ni hizo, na huku nilikolimia, ekari moja inaweza toa hadi gunia 3 .
Gharama hizi zina uhalisia? Kwasababu huku kilwa 1.kukodi ekari ni 50000 2.kufyeka ni 30000 3.sumu ya magugu ni chupa mbili ambazo ni sawa na 18000 4. Kutibua ni 50000 kwa ekari 5.kupanda ni 30000 kwa ekari 6.kupogolea ni 50000 kwa ekari 7 kupalilia ni 50000 kwa ekari 8 sumu na mbolea ya maji wastani ni 15000 kwa ekari 9 kuvuna 50000 kwa ekari
 
Mwaka huu mbona ilishajulikana....wanunuzi ndio hawajatokea.
Mbaaazi na korosho kilio kitakuwa hikihiki.
Wakulima wenzangu tusikate Tamaa mwakani bei inarud kuwa juu maradufu.
Nini kimefanya wanunuzi wasitokee mwakahuu,na waliotokea hao wachache mbona wamechukua kwa bei ndgo.
 
Masoko ya kilimo ni changamoto sana:
Ukizingatia ghalama za kulima ziko juu sana:
 
Naona soko la ufuta sio zuri kwa mwaka huu, kondoa wana elf 2630, uliko soko likoje?
ufuta unalima dodoma sehemu gani?! naskia kongwa na chemba wapo vizuri kwenye ufut. nataka nilime ufuta nipo dodoma
 
Gharama hizi zina uhalisia? Kwasababu huku kilwa 1.kukodi ekari ni 50000 2.kufyeka ni 30000 3.sumu ya magugu ni chupa mbili ambazo ni sawa na 18000 4. Kutibua ni 50000 kwa ekari 5.kupanda ni 30000 kwa ekari 6.kupogolea ni 50000 kwa ekari 7 kupalilia ni 50000 kwa ekari 8 sumu na mbolea ya maji wastani ni 15000 kwa ekari 9 kuvuna 50000 kwa ekari
Umeelewa kweli?, nimesema nilipo
 
Mkùu habari,naomba nichek inbox maana mimi nashindwa kukuchek
Nataka nipate elim zaidi
 
Back
Top Bottom