Soko la samaki la feri laungua majiko 48 yateketea. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Soko la samaki la feri laungua majiko 48 yateketea.

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MziziMkavu, Mar 5, 2010.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Mar 5, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,770
  Likes Received: 4,912
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
  Picha inaonyesha jinsi gani moto ulivyoharibu miundo mbinu ya soko Thursday, March 04, 2010 2:58 PM
  Soko la kukaangia samaki la Feri lililopo katika kivuko cha Kigamboni limeteketea kwa moto usiku wa kuamkia leo. Soko la kukaangia samaki la Feri lililopo katika kivuko cha Kigamboni limeteketea usiku wa kuamkia leo , akizungumza shuhuda mmoja aliyekuwepo katika tukio hilo aliye jitaja kwa jina la Jafari Juma alisema kuwa soko hilo liliungua majira ya saa 4 usiku wakati wakaanga samaki wengi walikuwa tayari wameondoka.

  Mmoja wa wakaanga samaki alikuwa anawahi kuondoka ndipo alipo chukua mafuta yaliyokuwa na uchafu wa samaki ambao tayari walikuwa wamekaangwa akarushia kwenye jiko ndipo mlipuko ukatokea mripuko huo umesababisha hasara ya Majiko 48 kuungua.

  Kutokana na moto huo kuunguza soko hilo vibaka na baadhi ya wavuvi wameiba vitu mbalimbali vikiwemo vyuma chakavu vilivyo salia katika janga hilo.
   
 2. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #2
  Mar 5, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,770
  Likes Received: 4,912
  Trophy Points: 280
  MOTO WATEKETEZA SOKO LA SAMAKI FERI


  [​IMG] MOTO mkubwa umezuka na kuteketeza baadhi ya majiko ya kukaushia samaki katika soko la Feri lililoko Kivukoni jijini Dar usiku wa kuamkia leo.
  Akiongelea tukio hilo, Meya wa Wilaya ya Ilala, Abu Juma, alisema jana majira ya saa tatu na nusu usiku alipata tarifa za moto kuteketeza soko hilo ambapo alikwenda kushuhudia tukio na kukuta kikosi cha Zimamoto kikiendelea na uzimaji wa moto huo.
  Alisema chanzo cha moto huo hakikufahamika mara moja isipokuwa alihisi baadhi ya watumiaji wa majiko katika soko hilo hawakuyazima baada ya kuyatumia, hususani jiko Namba Moja ambako moto unadaiwa kuanzia.

  [​IMG]
  Jengo la soko hilo lilivyoteketea kwa moto.

  [​IMG]
  Meya wa Wilaya ya Ilala Abu Juma (katikati) akijaribu kuelezea chanzo cha moto huo kwa waandishi wa habari.

  [​IMG]
  Baadhi ya askari na raia wakishudia juhudi za kuuzima moto huo.

  [​IMG]
  Shughuli ya kuuzima moto ikiendelea.​
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...