Soko la Samaki Feri walia umeme | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Soko la Samaki Feri walia umeme

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by Saint Ivuga, Jul 21, 2011.

 1. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #1
  Jul 21, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,274
  Likes Received: 19,416
  Trophy Points: 280
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: contentheading, width: 100%"]Soko la Samaki Feri walia umeme
  [/TD]
  [TD="class: buttonheading, width: 100%, align: right"] Send to a friend [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: createdate"] Wednesday, 20 July 2011 20:42 [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD] 0digg

  Timothy Marko
  WAFANYABIASHARA wa samaki katika Soko la Feri lililopo Dar es Salaam wameiomba Serikali kuliboresha soko hilo kwa kuliwekea jenereta ili kuepusha kuoza kwa samaki wanaotunzwa kwenye majokofu.

  Meneja wa soko hilo, Bure Mdoe alisema hayo jana alipozungumzia mgawo wa umeme unavyosababisha hasara kwao.Mdoe alisema mgawo wa umeme unasababisha samaki wanaotunzwa kwenye majokofu kuoza na kuwakosesha mapato.

  Aliiomba Serikali kuwa na mpango wa kuliweka jenereta sokoni hapo ili kupunguza hasara kwa wafanyabiashara.
  ‘’Mgao wa umeme unatusababishia samaki wetu kuoza katika majokofu. Umeme unapokatika samaki wanaoza na kutusababishia hasara”alisema.
  Kuhusu masuala ya kuwapo kwa wizi wa mizigo ya wafanyabiashara nyakati za usiku, meneja huyo alisema uongozi ulishalijua suala hilo na kwamba mikakati iliandaliwa ili kudhibiti wezi.

  Alisema uchunguzi wa awali ulibaini kuwapo kwa baadhi ya wafanyabiashara wadogowadogo wengi ambao siyo rasmi jambo ambalo linasababisha msongamano wa watu na kuzuka kwa wezi.

  Meneja huyo alisema uongozi kwa kushirikiana na Manispaa ya Ilala umeimarisha ulinzi kwa kuongeza wanamgambo nyakati za usiku.
  Naye mfanyabiashara wa samaki sokoni hapo, Hamis Mwewe alisema mgawo wa umeme umesababisha wafanyabiashara wasiwanunue samaki wengi kutoka kwa wavuvi.

  “Tunaogopa kununua samaki wengi kwa hofu ya kuoza. Hali hii inasababisha upungufu wa samaki hata kwa walaji”, alisema.
  Alifafanua kwamba hali ya biashara ya samaki kwa sasa ni mbaya kutokana na kukatikakatika kwa umeme na kwamba hata wateja wa rejareja wananunua kidogo kwa hofu ya kuoza.
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
Loading...