Soko la mayai, je hii ni kawaida?

Soko la mayai, je hii ni kawaida?

kijani11

JF-Expert Member
Joined
Jan 19, 2014
Posts
8,383
Reaction score
9,216
Habari zenu wana jukwaa,

Mimi ni mfugaji wa kuku wa mayai ila bado ni mgeni ndo nimeanza kupata mayai wiki chache zilizopita.
Nilipoanza kupata mayai watu walikuwa wanakuja na kuweka order kabla hata hayajatagwa lakini baada ya mda hali imebadilika mayai yamejaaa mtaani naambiwa mayai yamezidi mahitaji bei imeshuka kutoka 7000 tray mpaka 4500-5000 lakini hamna wa kumuuzia hayo mayai

Je hii ni kawaida kwamba kipindi hiki soko hupotea?
 
Mkuu kijani11 ni kweli kabisa hiyo biashara kwasasa ni ngumu sana
 
Last edited by a moderator:

Kweli mkuu yaani unajikuta una rundo mayai unakosa hela ya kununua chakula cha kuku ndio hata najiuliza hii hali ni ya kawaida?
 
mkuu hapo sasa ndo wakati wa kubadilisha hiyo changamoto kuwa fulsa...ikibidi kuuza chipsi fanya hivyo ili mradi usitegemee kuwauzia watu...fanya kile wanachoyafanyia wao...
 
Nikipindi cha mpito tu mkuu, ila jaribu kutafuta wateja maeneo kama kisutu (kama uko dar)
 
mkuu hapo sasa ndo wakati wa kubadilisha hiyo changamoto kuwa fulsa...ikibidi kuuza chipsi fanya hivyo ili mradi usitegemee kuwauzia watu...fanya kile wanachoyafanyia wao...

Hahaha umenichekesha mkuu
 
mkuu hapo sasa ndo wakati wa kubadilisha hiyo changamoto kuwa fulsa...ikibidi kuuza chipsi fanya hivyo ili mradi usitegemee kuwauzia watu...fanya kile wanachoyafanyia wao...
Usemacho ni sawa lakini shida sasa mtu unazalisha 20+ trays kuzipa matumizi ghafla ni changamoto kubwa.
 
kweli mkuu ni changamoto kubwa...ila jitahidi yasikuharibikie...kuna hawa jamaa wakurya jaribu kuongea nao hata kuwapa kwa mkopo
 
Mkuu kuna kipindi mayai yalikuwa adimu sana, mpaka 7500 yalikuwa yanagombaniwa. Nasikia kuna kampuni ya kuku ipo chanika, wanazalisha tray nyingi balaa, halafu wanauza tray 4000-4500.
Hapa ndani nina karibia tray 200
 
Duh aisee hali isipobadilika mambo yatakuwa si mambo.
 
mkuu hapo sasa ndo wakati wa kubadilisha hiyo changamoto kuwa fulsa...ikibidi kuuza chipsi fanya hivyo ili mradi usitegemee kuwauzia watu...fanya kile wanachoyafanyia wao...

yah chips moja sh 800
 
Mkuu kuna kipindi mayai yalikuwa adimu sana, mpaka 7500 yalikuwa yanagombaniwa. Nasikia kuna kampuni ya kuku ipo chanika, wanazalisha tray nyingi balaa, halafu wanauza tray 4000-4500.
Hapa ndani nina karibia tray 200

Wahindi nini hao??
 
Duh aisee hali isipobadilika mambo yatakuwa si mambo.
mkuu Kijani 11 Vipi hali ya soko la Mayai bado baya? Nami nimeanza ufugaji kuku wa Mayai ! Baada miezi 4 hivi nitakuwa nauza Mayai
 
Back
Top Bottom