Soko la dhahabu Geita lazinduliwa na Waziri Mkuu

Hasa wananchi "wanyonge" Hawa anawajali zaidi. Hakika awamu hii, wanatembea vifua mbele.
 
View attachment 1049718

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amekuwa akiwajali sana wananchi wake.

Waziri Mkuu ameeleza hayo katika ziara yake Misungwi wilayani Misungwi alipokuwa
akizungumzia suala la wananchi kuunganishiwa huduma ya umeme.

"Rais wetu Magufuli anajali sana wananchi wake, hivyo ametenga fedha nyingi zitakazotosheleza
kusambaza umeme katika vijiji vyote vikiwemo na Wilaya yenu hii ya Misungwi," ameeleza.

Waziri Mkuu ameeleza kuwa Gharama za kuunganishiwa umeme huo ni Tsh. 27,000. Katika hatua nyingine Wilayani humo, Waziri Mkuu amefungua Ujenzi na Ukarabati Mkubwa wa Kituo cha Afya cha Koromije.
SWALI KWA MH. WAZIRI MKUU;
Hivi REA imeanzishwa na Magufuli?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mnapenda kujikomba sana hata huku mliko anonymous,kauli sahihi ni.
Watendaji msiwaangushe wananchi.
Habari nzuri kwa nchi yetu..

Watendaji msiwaangushe viongozi wetu

Loyalty To country Alyways,To government When it deserves
 
Mnapenda kujikomba sana hata huku mliko anonymous,kauli sahihi ni.
Watendaji msiwaangushe wananchi.

Loyalty To country Alyways,To government When it deserves

Jionee aibu.. andika yako bila kutafutia kiki kwa kuninukuu.. ulivyoonyesha wewe ndicho unafanya humu.💀💀💀
 
Ni kweli kabisa.
Kodi hizi za Kuwaachia TRA wakadirie tu zimewaumiza wafanyabiashara sana.
Zinawafanya maafisa wa TRA kuwa Miungu watu na kupanua wigo wa Rushwa.

Utaratibu aliouanzisha Mh. Rais kwa wafantabiashara wadogo nadhini ni mzuri sana.
Watu walitakiwa wauchangamkie mana una lengo zuri sana.
Na pia unapunguza rushwa na ubabaishaji mwingi.
Utaratibu huo ulitakiwa uhamie kwa wafanyabiashara wote kulingana na ukubwa wa mtaji.
Siasa iwekwe pembeni.
Mfano uliotaja kwa masonara ni wa kweli ,na pia ni rahisi kudili na kodi kwao ikiwemo Leseni ya biashara.

Maushuru yanakua mengi na yanapewa majina mengi sana mpaka inakua ni tabu kulipika.
Kodi ingewekwa kwenye Leseni ya mmiliki wa Mashimo ya wachimbaji wadodgo wa dogo tu.
Mana sio kila siku anapata. Kisha iende kwenye Leseni ya wafanyabiashara wa wadogo ,mabroka na wale wakubwa . Kila mmoja apewe Kiwango chake cha kulipia Leseni mpaka kule kwenye sonara.
Hizi kodi kodi nyingine ndio zinazosababisha Rushwa kwa maafisa wa TRA.
Matokeo yake ni kuwa na Maafisa wa TRA wanaomiliki Mali nyingi na zenye thamani kubwa kwa ujumla wake kuliko Mali wanazomiliki walipa kodi. Ikiwa na maana hela nyingi zinapotea kwenye Rushwa ili wasiwakomoe wafanya biashara kwa kuwakadiria kiwango cha juu.

Sheria zinapokua nyingi zinasababisha wigo wa Rushwa uwe mkubwa badala ya tija kwa taifa na wananchi waliowekeza mitaji na nguvu zao.
Nchi inakua na matajiri wasiozalisha wala kurumia nguvu zao kumiliki Mali zaidi ya Rushwa. Ni bora kuwapa unafuu wafanyabiashara wa kitanzania kisheria ili mitaji yao ikue waongeze wigo wa ajira na TRA wapate kodi kwenye income tax ,kuliko huu mfumo mbovu wa makodi mengi ya kukisia tu na kuwafanya wafanyabiashara wafilisike huku maafisa wa TRA wakijilimbikizia Mali na kujenge mijengo isiyozalisha wala kutoa ajira kwa watoto wa maskini wa Tanzania.

Wakati mwingine naona kuwa ni bora kuwa na wafanyabiashara wakwepa kodi kuliko maafisa wa TRA wala Rushwa.
Mfanyabiashara mkwepa kodi anaweza akakuza mtaji na biashara ikapanuka na akaongeza wigo wa ajira tofauti na TRA mla Rushwa na hasara kwa taifa na wafanyabiashara pia.

Sent using Jamii Forums mobile app

Ni kweli mkuu yaani faida ya taasisi ya TRA ni ndogo sana halafu ukiwachunguza mmoja mmoja mali walizokuwa nazo ni majasho ya damau ya wafanyabiara
 
Back
Top Bottom