Soko la dhahabu Geita lazinduliwa na Waziri Mkuu

mamayoyo1

JF-Expert Member
Jul 25, 2018
1,011
1,019

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amezinduliwa soko kuu la dhahabu mkoa wa Geita leo baada ya kumaliza ukaguzi wa mabanda yatakayotoa huduma ndani ya soko hilo. Waziri Mkuu alikuwa ameongozana na Waziri wa Madini, Dotto Biteko pamoja na watendaji mbalimbali wa taasisi mbalimbali za serikali.

Katika uzinduzi huo Waziri Mkuu ametembelea na kuhoji masuala mbalimbali katika banda la Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), litakalotoa huduma mbalimbali ikiwamo uthibitishaji wa thamani halisi ya mapato yatokanayo na madini kwa wauzaji wa madini.

Ametembelea banda la kamati ya ulinzi na usalama kwa ajili ya kuimarisha usalama kwa wafanyabiashara na wadau wa soko hilo. Pia alitembelea katika mabanda ya benki za NMB na CRDB zilizojipambanua namna zitakavyohusika katika ufanikishaji wa huduma za kifedha ndani ya soko hilo.

Soko hilo litakalofungua fursa za kiuchumi kwa mkoa huo, litahusisha wadau wote walio kwenye mnyororo wa biashara ya madini wakiwemo wanunuzi, wauzaji, TRA, Tume ya Madini, benki na mamlaka ya serikali za mitaa.
 
Hili soko limeshindwa kabla hata halijaanza.
Biashara ya dhahabu haipo kiivyo. Aliyebuni wazo hili alipaswa kujifunza kwanza jinsi mfumo mzima wa biashara ya dhahabu unavyofanya kazi.

Kuna matajiri wakubwa ambao wanazungusha mitaji yao kwenye dhahabu.
Hawa wanaitwa Ma-kota. Hawa wanagawa fedha nyingi kwa makota wadogo wadogo kwa misingi ya uaminifu na kwakuwa wanatanguliziana hela wanapanga kabisa bei ya kuja kukabidhi mali.

Huyu kota mdogo anaenda kwa wachimbaji wadogo na kutanguliza hela za uendeshaji wa kazi na hapo pia wanapeana bei ya kuja kukabidhi mali.
Biashara hii ni ya imani/kuaminiana mwanzo mwisho. Haina maandishi

Sasa ukileta mfumo mpya kabisa na umekaa tu ofisini ukaubuni kwa players walewale ,wenye mfumo wao ambao jinsi hali imekaa uko efficient, kuna kufaulu kweli?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
TOA MAWAZO NA USHAURI NI MUHIMU SANA
 
Vipi kwenye hilo soko hawajengi ukuta kama kule mererani ili kuzuia wezi wa madini yetu ?

Halafu kwanini hawajalihusisha jeshi letu kwenye ulinzi na usiamizi wa hili soko, mbona kwenye yale masoko ya kubadilisha hela walilihusisha mwanzo mwisho ?

Wafanye hivyo hapa kabla mambo hayaharibika naamini jeshi letu litasimamia vizuri hilo soko kuliko hata hao TRA na Polisi.
 
Mfumo wa ununuaji wa sonara ungeachwa uendelee halafu TRA apange utaratibu mzuri wa kukusanya kutoka kwa sonara na chain itakayoanzia hapo mpaka kwenye end product.

Serikali ikae chini na hawa Makota wakubwa maana wengi wanafahamika ikubaliane mfumo ambao wao nao watalipa kodi na chain yote kutoka kwao kwenda kwenye end product au nje ya nchi!

Ila kabla ya kwenda kujenga hilo soko serikali ilipaswa kutoa dodoso za kukusanyia taarifa kwa wachimbaji wadogo na wakubwa ili kujua namna chain ya biashara ya dhahabu imekaa!
Kuwa na mfumo ni jambo moja, kuwa na mfumo unaofanya kazi kwa ufanisi ni jambo jingine!
TOA MAWAZO NA USHAURI NI MUHIMU SANA

Sent using Jamii Forums mobile app
 
sijaelewa, hilo soko lina ukubwa gani, na average kwa siku hao wachimbaji wadogo wanaweza pata kgs ngapi, au litakuwa na huduma nyingine yaani kama Kariakoo na department ya kununua dhahabu?
 
Mfumo wa ununuaji wa sonara ungeachwa uendelee halafu TRA apange utaratibu mzuri wa kukusanya kutoka kwa sonara na chain itakayoanzia hapo mpaka kwenye end product.

Serikali ikae chini na hawa Makota wakubwa maana wengi wanafahamika ikubaliane mfumo ambao wao nao watalipa kodi na chain yote kutoka kwao kwenda kwenye end product au nje ya nchi!

Ila kabla ya kwenda kujenga hilo soko serikali ilipaswa kutoa dodoso za kukusanyia taarifa kwa wachimbaji wadogo na wakubwa ili kujua namna chain ya biashara ya dhahabu imekaa!
Kuwa na mfumo ni jambo moja, kuwa na mfumo unaofanya kazi kwa ufanisi ni jambo jingine!

Sent using Jamii Forums mobile app
seen,,
 
Ni kweli kabisa.
Kodi hizi za Kuwaachia TRA wakadirie tu zimewaumiza wafanyabiashara sana.
Zinawafanya maafisa wa TRA kuwa Miungu watu na kupanua wigo wa Rushwa.

Utaratibu aliouanzisha Mh. Rais kwa wafantabiashara wadogo nadhini ni mzuri sana.
Watu walitakiwa wauchangamkie mana una lengo zuri sana.
Na pia unapunguza rushwa na ubabaishaji mwingi.
Utaratibu huo ulitakiwa uhamie kwa wafanyabiashara wote kulingana na ukubwa wa mtaji.
Siasa iwekwe pembeni.
Mfano uliotaja kwa masonara ni wa kweli ,na pia ni rahisi kudili na kodi kwao ikiwemo Leseni ya biashara.

Maushuru yanakua mengi na yanapewa majina mengi sana mpaka inakua ni tabu kulipika.
Kodi ingewekwa kwenye Leseni ya mmiliki wa Mashimo ya wachimbaji wadodgo wa dogo tu.
Mana sio kila siku anapata. Kisha iende kwenye Leseni ya wafanyabiashara wa wadogo ,mabroka na wale wakubwa . Kila mmoja apewe Kiwango chake cha kulipia Leseni mpaka kule kwenye sonara.
Hizi kodi kodi nyingine ndio zinazosababisha Rushwa kwa maafisa wa TRA.
Matokeo yake ni kuwa na Maafisa wa TRA wanaomiliki Mali nyingi na zenye thamani kubwa kwa ujumla wake kuliko Mali wanazomiliki walipa kodi. Ikiwa na maana hela nyingi zinapotea kwenye Rushwa ili wasiwakomoe wafanya biashara kwa kuwakadiria kiwango cha juu.

Sheria zinapokua nyingi zinasababisha wigo wa Rushwa uwe mkubwa badala ya tija kwa taifa na wananchi waliowekeza mitaji na nguvu zao.
Nchi inakua na matajiri wasiozalisha wala kurumia nguvu zao kumiliki Mali zaidi ya Rushwa. Ni bora kuwapa unafuu wafanyabiashara wa kitanzania kisheria ili mitaji yao ikue waongeze wigo wa ajira na TRA wapate kodi kwenye income tax ,kuliko huu mfumo mbovu wa makodi mengi ya kukisia tu na kuwafanya wafanyabiashara wafilisike huku maafisa wa TRA wakijilimbikizia Mali na kujenge mijengo isiyozalisha wala kutoa ajira kwa watoto wa maskini wa Tanzania.

Wakati mwingine naona kuwa ni bora kuwa na wafanyabiashara wakwepa kodi kuliko maafisa wa TRA wala Rushwa.
Mfanyabiashara mkwepa kodi anaweza akakuza mtaji na biashara ikapanuka na akaongeza wigo wa ajira tofauti na TRA mla Rushwa na hasara kwa taifa na wafanyabiashara pia.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amezinduliwa soko kuu la dhahabu mkoa wa Geita leo baada ya kumaliza ukaguzi wa mabanda yatakayotoa huduma ndani ya soko hilo. Waziri Mkuu alikuwa ameongozana na Waziri wa Madini, Dotto Biteko pamoja na watendaji mbalimbali wa taasisi mbalimbali za serikali.

Katika uzinduzi huo Waziri Mkuu ametembelea na kuhoji masuala mbalimbali katika banda la Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), litakalotoa huduma mbalimbali ikiwamo uthibitishaji wa thamani halisi ya mapato yatokanayo na madini kwa wauzaji wa madini.

Ametembelea banda la kamati ya ulinzi na usalama kwa ajili ya kuimarisha usalama kwa wafanyabiashara na wadau wa soko hilo. Pia alitembelea katika mabanda ya benki za NMB na CRDB zilizojipambanua namna zitakavyohusika katika ufanikishaji wa huduma za kifedha ndani ya soko hilo.

Soko hilo litakalofungua fursa za kiuchumi kwa mkoa huo, litahusisha wadau wote walio kwenye mnyororo wa biashara ya madini wakiwemo wanunuzi, wauzaji, TRA, Tume ya Madini, benki na mamlaka ya serikali za mitaa.
So what??
 
aziri Mkuu, Kassim Majaliwa amekabidhi matrekta16 yenye thamani ya shillings bilioni 1.8 kwa wenyeviti wa baadhi ya Vyama vya Ushirika via Msingi mkoani Mwanza, iliyoandaliwa na Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC) kwenye mtaa wa Posta jijini Mwanza, leo Machi 19, 2019.

1553077397441.png

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amekuwa akiwajali sana wananchi wake.

Waziri Mkuu ameeleza hayo katika ziara yake Misungwi wilayani Misungwi alipokuwa
akizungumzia suala la wananchi kuunganishiwa huduma ya umeme.

"Rais wetu Magufuli anajali sana wananchi wake, hivyo ametenga fedha nyingi zitakazotosheleza
kusambaza umeme katika vijiji vyote vikiwemo na Wilaya yenu hii ya Misungwi," ameeleza.

Waziri Mkuu ameeleza kuwa Gharama za kuunganishiwa umeme huo ni Tsh. 27,000. Katika hatua nyingine Wilayani humo, Waziri Mkuu amefungua Ujenzi na Ukarabati Mkubwa wa Kituo cha Afya cha Koromije.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom