Soko la bata maji (Muscovy Duck)

up-grader

Member
Jul 23, 2010
8
1
Habari wadau,

Nina mradi wangu mdogo wa bata, kwa sasa wapo kama 50 ukiweka na watoto, mpango wangu ni kuzalisha mpaka nifikie uwezo wa kuzalisha atleast bata 100 kwa mwezi ndani ya mwaka mmoja, 200-500 ndani ya miaka miwili. kwenye suala uwezo wa bata kuzaliana sina shaka kwani nilianza na majike matano na dume moja miezi saba iliyopita na nina wawili wanalalia kwa sasa.....

Utafiti wangu wa soko inaonekana bata anaweza kuuzwa kati ya sh 15000-25000 kulingana na umbo na wakati, hizi ni bei ambazo nimepata kwa kuuliza kwa wauzaji wadogowadogo masokoni, soko hili kwa bata 10,20,30 hivi linaweza lisisumbue, ishu inakuja kwenye bata 100, 200.etc bado sijapata majibu mazuri kwenye hili...

kwa mwenye uzoefu wa kufunga bata naomba ushauri kwenye soko hasa
1. bei na kama kuna uhitaji wa product tofauti ie mayai, vifaranga etc
2. wateja wakubwa na terms zao
3. changamoto na mengineyo

mimi Nipo Dar, shamba langu lipo Kigambon -Tundwi

Natanguliza shukrani.
 
Wakati ukisubiri majibu ya maswali yako ya kimsingi. Nitangulize hongera kwa mtazamo wako mzuri wa ujasiriamali kwenye kufuga.
Hongera sana.
 
kaka mi nina maswali kwako(1)soko gani kwa dar na weza kuuza kirahis bata 20 kwa bei ya tsh 15elf,(2)juzi vifaranga vyangu25 vimekufa,je njia ipi yaweza nifanya nipunguze vifo
 
1. kuhusu soko nimewauliza watu wenye vibanda kadhaa sinza na keko, wao wanauza btn 20-25 kwa bata wa kawaida madume arround 25-30, isipokuwa wanataka uache bata wako uchukue hela wakishauza.... kimsing hawa hawana mtaji kwahiyo kwa biashara ya bata wachache mnaweza fanya na uwe mvumilivu

2.kuhusu suala la vifaranga kufa.... hapa naomba niwe mwazi, sijawahi kufiwa na kifaranga hata mmoja kwahiyo sina majibu na hilo, ninachofanya ni
---.kuwalisha hawa vifaranga chick starter kwa mwezi mmoja
---kuwatenga vifaranga na bata wengine wakubwa -ukiwaweka pamoja kuwa madume yanawadono -nilipewa ushauri wakati naanzaila
kunamtu alikuwa na tatizo kama hili akashauriwa abadilishe dume kutokana na uwezekano wa in breeding -(kuzaa kwa bata mzazi na mtoto, kaka na dada etc), amefanya hivyo. nitakupa matokeo bata wake wakizaa tena

naomba wenye uzoefu zaid watusaidie,
 
Muscovy Duck Care Practices - Department of Animal Science
tembelea hapa mdau
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom