Soka la bongo OVYO sana | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Soka la bongo OVYO sana

Discussion in 'Sports' started by Anselm, Apr 24, 2012.

 1. Anselm

  Anselm JF-Expert Member

  #1
  Apr 24, 2012
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 1,705
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Mpaka usawa huu bingwa yeyote atakayepatikana(kati ya Simba na Azam) kwa mtazamo wangu atakuwa hajapatikana kwa haki,ni miapango tu tena ya nje ya uwanja.
  Wakati kina Mwasyika walipomtandika ngumi Israel Nkongo,wapenda soka wote tulikilaani kitendo kile kwakuwa si tu hakikuwa cha kiungwana bali pia kilikuwa kimetia doa kubwa sekta ya michezo hapa Tz,mengi yalisemwa na hatua kali zilichukuliwa tena tukianzia na wale waliokuwa hata hawastahili kuchukua hatua(kamati ya ligi) lakini hakuna Mtanzania yeyote aliyethubutu kujiuliza ni nini kilichowapata Yanga mpaka kuamua kurusha ngumi, kama kufungwa ile haikuwa mechi ya kwanza Yanga kufungwa,walishafungwa mechi kadhaa na hawakupiga mtu,kwa yeyote anaeyeiruhusu akili yake kutafakari kwa kina basi anapaswa atambue kuwa kulikuwa na tatizo tena la wazi kabisa.
  Bahati mbaya sana tukianzia na vurugu za mechi ya Yanga na Azam,refferee ambaye ndo alikuwa chanzo cha tatizo hajafanyiwa kazi kabisa,hakuna hatua zozote zilizochukuliwa na Wahusika TFF au FRAT,thanks to kina Mwasyika walioamu kumchukulia hatua palepale uwanjani, baada ya mechi ile Azam wakapiga mechi nyingine (nimeisahau kidogo) mchezaji wa team pinzani iliyokuwa inacheza na Azam kama kawaida akapigwa red card na maamuzi mengine mengi ya utata Azam wakaibuka na ushindi,team pinzani ikalalamika na kuishia zake,mechi iliyofuata Azam ikasafiri mpaka Dodoma kukipiga na Polisi,kama kawaida maamuzi ya utata yakawapa Azam ushindi wa goli 1 la dakika za mwishoni kabisa,Jamaa wakasubiri kipyenga cha mwisho wakamtandika vizuri refferee,jana sasa Mtibwa akawa mgeni wa Azam pale Chamazi ngoma imepigwa mpk dakika za mwishoni kabisa maaamuzi mengi ya utata ikiwemo la goli 1 la wazi la Mtibwa kukataliwa yalikuwa yanafanywa na refferee,Mtibwa wakilalamika kila wakati lkn wakiendelea kukomaa,mpira ukiendelea ukingoni kabisa huku matokeo yakiwa bado ni 1-1 refferee akiwatafutia ushindi Azam akawapa penalt ya dk 87,Mtibwa wakaona that too much,punch 2,3 zikabadilishwa na kufuatiwa na Mtibwa kugoma kuendelea na mchezo,mpira ukavunjika,definately Azam watapewa ushindi wa mezani wa point 3 na magoli yao ma'3...yote haya yanatokea katika mechi zinazohusisha Azam,wahusika wanshindwa kujiuliza kuna nini wakafanya uchunguzi na kuchukua hatua,sijui wanasubiri nini au wanasubiri siku atakayekufa refa m'1 ndo wajue kuwa kuna hatari sana kuacha wenye pesa wakitengeneza matokeo ya ushindi kwa njia zisizo halali?
  Naomba kuwasilisha.
   
 2. G

  Gagso Member

  #2
  Apr 25, 2012
  Joined: Apr 16, 2012
  Messages: 58
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Yan hiyo n kweli azam wanaonga,na kitendo hicho hao FFT WANAJUA KABSA NA NDIO MAANA SOKA LETU LIPO PALEPALE 2?yan cha msingi hapo hiyo fft wote wafunguzwe na upatikane uongoz mpya ndio tutaendelea!
   
 3. Mc Tilly Chizenga

  Mc Tilly Chizenga JF-Expert Member

  #3
  Apr 25, 2012
  Joined: Feb 7, 2012
  Messages: 3,722
  Likes Received: 824
  Trophy Points: 280
  kwa nini umeihusisha simba ktk mambo ya azam?

  pili ktk soka hatuangalii chanzo tunaangalia matendo mfano zidane-materazzi saga!
   
 4. BONGOLALA

  BONGOLALA JF-Expert Member

  #4
  Apr 25, 2012
  Joined: Sep 14, 2009
  Messages: 13,793
  Likes Received: 2,402
  Trophy Points: 280
  Mohammed dewji aliuza african lyon sababu wachezaji wake walikua wakiuza mechi na marefa rushwa
   
 5. CAMARADERIE

  CAMARADERIE JF-Expert Member

  #5
  Apr 25, 2012
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 4,427
  Likes Received: 159
  Trophy Points: 160
  Watu wa YANGA kwa ubishi na kulalama hamuwezekani....kwani Azam imeaanzishwa lini?...ngoja aje BALANTANDA hapa!
   
 6. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #6
  Apr 25, 2012
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  Mimi ni mmoja wa watu nilio waponda sana Yanga kwa kitendo cha kumshamulia refa lakini sasa naanza kuelewa na kuungana na mtani wangu kwa kitendo cha kumtandika refa na watu kama mwasika wanapaswa kuitwa machujaa na jua nimewagalimu lakini itabaki kwenye kumbukumbu kuwa mpira wa ujanja ujanja noooooo......................
   
 7. O-man

  O-man JF-Expert Member

  #7
  Apr 25, 2012
  Joined: Nov 17, 2011
  Messages: 318
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Chama cha marefa toeni hoja zenu. Wengi tunapenda kuona kabumbu likisakatwa kwa ufundi na manjonjo ya mchezaji binafsi. Inapotokea waamuzi ndio chanzo cha kuuvuruga mchezo, nachelea kusema, huu ni muda muafaka chama cha waamuzi kutoa tamko kuhusiana na hili. Soka ni burudani kwanza ikifuatiwa na biashara au masilahi binafsi. Burudani ikivurugwa na biashara hufa. Mwamuzi hapaswi kuwa chanzo cha kutuondolea burudani ya ushindani ndani ya uwanja. Timu zetu zinalemazwa kiasi ya kwamba zinapotoka nje ya nchi hazitegemei uwezo ila hutegemea bahati pekee. FRAT amkeni sasa. Ikibidi kuamshwa basi mjuwe wazi kwamba hamhitajiki tena kwenye nafasi zenu. Nawasilisha.
   
 8. mmbangifingi

  mmbangifingi JF-Expert Member

  #8
  Apr 25, 2012
  Joined: Mar 9, 2011
  Messages: 2,855
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Nimesikitishwa sana,but kwa lililotokea this week Mtibwa vs azam game proves liko jambo kwa marefa na timu nzima ya azam
   
 9. Anselm

  Anselm JF-Expert Member

  #9
  Apr 26, 2012
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 1,705
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Mc Chizenga nitakueleza kwanini...
  Unajua mipango mingi ya nje ya uwanja ya Azam ligi ilipokuwa katikati ilikuwa inapangwa pamoja na Simba,can U believe this? sasa ukitaka nikuthibitishie hili nitafute chemba ndo utaamini kuwa Bongo Tz ni zaidi ya unavyoijua.
  Hlf hivi unakumbuka Kamati ya Ligi ilikutana baada ya muda gani tokea vurugu za Azam na Yanga zitokee,umeshawahi kujiuliza ni kwanini ilikutana siku ya 2 tu baada ya mechi na ni sababu gani iliyopelekea isikutane mapema baada ya vurugu za mechi ya Mtibwa na Azam(tuliambiwa ilikuwa ikae jana lkn mpk leo hakuna taarifa zozote)...tafakari vizuri Kaka.
   
 10. kichwat

  kichwat JF-Expert Member

  #10
  Apr 26, 2012
  Joined: Mar 4, 2010
  Messages: 1,824
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  Dawa ni kupiga marefa hadi watakapoona hailipi kuchukua 3m halafu akajigharamie matibabu kwa 5m. Nashauri wapigaji waongeze mkong'oto ili hesabu ya hasara vs faida ikae vizuri, wataacha tu.
  (samahani njia hii ni crude kidogo, lakini very effective
   
Loading...