Soka la bongo ni Nyoso Ila sio Juma

Zombie S2KIZZY

JF-Expert Member
Mar 15, 2021
823
1,613
Soka la bongo halitaendelea kamwe kwasababu ya ubovu wake kuanzia kwny timu zake unafiku uzandiki ushamba

Hivi hizi simba na yanga n timu za Kenya na Tanzania au? maana ushabiki unazidi Sasa si ajabu jumapili umuone mwana simba anawashabikia rivers hadharan kwa mkapa wampige yanga hii hata watu walioko nje wanaona akili hamna

Yaan uwanja wenu taifa lenu alafu mnakaa kuwashabikia wageni hivi kwa mtindo huu soka la bongo litafika kwel au ndy tutakua tunaishia robo !
Chakushangaza hadi kwenye timu ya taifa napo usimba na uyanga umeshamiri daaah huu ni ujinga pro max

Mtu na domo lake refu hata halijaswaki unalikuta Bora simba imetolewa Asante wydad mnyama ungempiga hata nane
Sasa bi ashura na Hilo domo lako em nikuulze hvi simba niyawapi si ni Tanzania
Sasa wakipigwa nane huko ugenini aibu kwa nani si ni kwa watanzania wote mnaaibika

Hiv hamjiuliz mbona hamjawaona mashabiki wa raja kwenye mechi ya wydad na simba kwamba wawashabikie simba alafu wawaponde wydad kisa tu ni wapinzan wao ?

Na pia hizi mentality za kwamba tukienda kucheza na waarabu lazima watufunge mbn sisi hatuwazag kuwafunga si tunawaza kushindwa tu huu ni ujinga na soka letu halitafika kwny hatua kubwa kama wenzetu
Wenzetu Wamorocco timu zao zimeshatinga nusu fainali ya klab bingwa

Sisi Sasa kuingiza timu zetu robo klab bingwa na shirikisho tunatambiaaana hivi kwann hizo nguvu za kutambiana na kuombeana mabaya tusiwe tunawaombea wapinzani wetu ambao tunakutana nao kwenye ligi za nje tubaki tu kutambiana kwny premier yetu tu ?

Kwa mtindo huu tulionao tutabaki tu kuchambana wakati huo tukishuhudia wenzetu wakipeana zamu ya kunyanyua mikono juu msimu huu mamelodi msimu ujao raja unaokuja wydad unaokuja mwngne na mwngne sisi tutabaki tu kushindana kutoa Jezi mpya Kila mwezi .

Shhhiieeeet
 
Maneno hayo ungeyatoa juzi yangekuwa na mantiki lakini si leo baada ya kuchapwa ndipo unaona uchungu wa kuzomewa. Umesahau mlivyokuwa mkimfanyia mtani wenu? Pole jaribuni tena msimu ujao!!
 
Maneno hayo ungeyatoa juzi yangekuwa na mantiki lakini si leo baada ya kuchapwa ndipo unaona uchungu wa kuzomewa. Umesahau mlivyokuwa mkimfanyia mtani wenu? Pole jaribuni tena msimu ujao!!
Imechapwa simba au timu kutoka Tanzania?
 
Si mmekufa kiume wakuu, na mashabiki tuwasifu kufa kiume sio kikike.

Huu ndio utamaduni wetu, kwani kwa mashabiki wa Yanga kushabikia wageni ndo kumefanya simba atolewe??
Mashabiki wa simba kushangilia wageni ndo kumefanya yanga aende shirikisho??

Acheni kutafuta vijisababu wafa kiume fc.
 
Kwa hiyo mashabiki wa Yanga ndo wamemwambia chama na kapombe wapige penalty mbovu zidakwe? Nawakamwambia Alky Salum awe anapishana na mpira kwenye penalty? Na wakamwambia onyango aweweseke kwenye kulinda? Mna nn na yanga enyi kufa kiume fc?
Zngatia swal
 
Si mmekufa kiume wakuu, na mashabiki tuwasifu kufa kiume sio kikike.

Huu ndio utamaduni wetu, kwani kwa mashabiki wa Yanga kushabikia wageni ndo kumefanya simba atolewe??
Mashabiki wa simba kushangilia wageni ndo kumefanya yanga aende shirikisho??

Acheni kutafuta vijisababu wafa kiume fc.
Hii sio sababu hata tungeshinda Ila hali halisi kwa soka la bongo ndo hyo
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom