Mashabiki wa Simba kususia mechi yao jana imesababishwa jinsi tulivyoamua kuendesha Soka la Bongo

THE FIRST BORN

JF-Expert Member
Apr 24, 2019
1,729
3,290
Habari wapenda soka wenzangu, naam nianze kwa kusema Mpira wetu kivyetu vyetu, ndio naweza kusema hivo.

Jana Simba amecheza Match ya CAF Champions League walichokiona Viongozi na wapenda Mpira ni matokeo ya Mfumo ambao tumeutengeneza sisi kwa mda mrefu.

Naomba niseme tusijaribu kuwaita majina ya ajabu mashabiki wa Simba, wao hawana kosa ila wenye kosa ni Viongozi wa Simba.

Nahisi bado hamjanipata, issue hapa nayotaka kuiongelea ni kuwa imezoeleka na imetengenzwa kua kila kitu kwetu sisi kwenye mpira kinafanyiwa promo na Hamasa kubwa yaani ukisikia Mkapa imejaa Pomoni ujue promo iliyopigwa ni watu hawajalala week nzima wanapiga promo kila kona wanawaza wafanyeje ili uwanja ujae,

Yaani wamesahau kua Mpira ukiufanyia Hamasa ipo siku utakusaliti tu na utashindwa kufanya HAMASA.

Kwa Simba ya sasa hivi unapata wapi nguvu ya kufanya Hamasa kwa Mfano?

Ila laiti wangeacha Mashabiki wakaja wao wakapenda wao Mpira hata ingekua timu inapata matokeo mabovu vipi wangekuja tu maana wameipenda Team yao kutoka Moyoni na hawajapenda kwa kuvutwa kwa Maneno Mengi "Leo Mashabiki wanasusa kwa sababu wengi waliokua wanajaa kwenye Match hapo siku za Nyuma walikua Wanakuja kwa sababu ya Promo sio mapenzi yao kwa Simba".

Sasa hivi hamuwezi kupiga Promo kwa sababu Team inacheza vibaya haieleweki unaanzaje kupiga Promo? Ukishika kipaza saut mnaogopa mtatukanwa siku nzima.

Kwahio Niseme tu wale waliokuja jana ndio mashabiki zenu halisi wanaowapenda na wenye Mapenzi ya dhati na SIMBA sio wale mnaojivuniga na picha za Drone kua mmejaza. Yaani ni sawa na "Ukimpata Demu kwa Pesa Amini ipo siku utampoteza, sababu itakuwa ni pesa"

Ukitaka amini angalia mashabiki wa Manchester united pale England yaani team yetu mbovu ila kabla hata msimu haujaanza tickets zote hua zimeisha za msimu mzima, wale mashabiki hawapigiwi promo ila wameipenda team wao kwa moyo wao hawakuwa influenced na mtu bali the way team ilivyokua inacheza ndio waliipenda na wanaipenda hivohivo hata sasa hivi.

So, ukipata kitu kwa hamasa amini kwamba ikitokea siku hicho kitu kikajazwa Maneno kitakuacha tena na hautakua na nguvu ya kukirudisha maana utakua katika hali mbaya, ndio
Simba na Uongozi wake na ndio mfumo wa Soka la Bongo, kila kitu promo.

#LifeisDream🇵🇹
 
Wazungu ni watu wa ratiba tuache kujifananisha nao. Tiketi zao ni bei ghali ila zinaisha mapema sababu ya mfumo wao wa ratiba. Wengi unaowaona pale inawezekana ratiba yake tayari anayo tangu mwaka uliopita kuwa kila tarehe atakuwa wapi na atafanya nini na huenda kuwepo uwanjani ni sehemu ya mapumziko.

Sisi pesa hatuna, tupo free, wengi hatuna ratiba hata ya siku tatu mbele, hii inasababisha tusiwe na taarifa ya mambo tunayotaka kuyafanya ikiwemo kwenda uwanjani, sasa usipofanya promotion utajikuta upo wewe msemaji na kocha kwenye jukwaa.
 
Leo Mashabiki wanasusa kwa sababu wengi waliokua wanajaa kwenye Match hapo siku za Nyuma walikua Wanakuja kwa sababu ya Promo sio mapenzi yao kwa Simba".
Hii ni dharau kubwa kwa Mashabiki wa Simba. Mleta mada una Nia ovu dhidi ya Timu ya Simba. Mimi ni shabiki wa Yanga lakini sijafurahishwa na kauli hii uliyoitoa.

Waombe radhi.
 
Nimeanza kuingia mpirani muda mrefu kabla hata ya Azam kuanza kuonyesha mpira, Tena watu walikuwa wanakaa Hadi wanakosa tiketi. Wakati huo Kuna watu walikuwa wanawahi kununua tiketi baadae wanalangua. Hayo Mambo ya promo ni upigaji wa watu kwani shabiki wa kweli haji kwa promo.
Viongozi walijisahau na kutojua nguvu ya washabiki na hayo ndio matokeo take.
Mashabiki wa promo ni hao wasanii wa bongo movie na miziki wa kizazi kipya.
 
Hii ni dharau kubwa kwa Mashabiki wa Simba. Mleta mada una Nia ovu dhidi ya Timu ya Simba. Mimi ni shabiki wa Yanga lakini sijafurahishwa na kauli hii uliyoitoa.

Waombe radhi.
Ingekua kama unavyodhani wewe mashabiki wa kweli wangekuja kuangalia match ya timu yao ila wale walifata kelele za msemaji.
Hilo halina ubishi hata alivyohama Manara si watu wengi walihama au waliacha kufaifatilia simba? Au uongo?
 
Nimeanza kuingia mpirani muda mrefu kabla hata ya Azam kuanza kuonyesha mpira, Tena watu walikuwa wanakaa Hadi wanakosa tiketi. Wakati huo Kuna watu walikuwa wanawahi kununua tiketi baadae wanalangua. Hayo Mambo ya promo ni upigaji wa watu kwani shabiki wa kweli haji kwa promo.
Viongozi walijisahau na kutojua nguvu ya washabiki na hayo ndio matokeo take.
Mashabiki wa promo ni hao wasanii wa bongo movie na miziki wa kizazi kipya.
Oky Jazeni mechi zinazokuja bila promo.
 
Wazungu ni watu wa ratiba tuache kujifananisha nao. Tiketi zao ni bei ghali ila zinaisha mapema sababu ya mfumo wao wa ratiba. Wengi unaowaona pale inawezekana ratiba yake tayari anayo tangu mwaka uliopita kuwa kila tarehe atakuwa wapi na atafanya nini na huenda kuwepo uwanjani ni sehemu ya mapumziko.

Sisi pesa hatuna, tupo free, wengi hatuna ratiba hata ya siku tatu mbele, hii inasababisha tusiwe na taarifa ya mambo tunayotaka kuyafanya ikiwemo kwenda uwanjani, sasa usipofanya promotion utajikuta upo wewe msemaji na kocha kwenye jukwaa.
Oky Reply nzurii mnoo.
 
  • Thanks
Reactions: Tsh
Ingekua kama unavyodhani wewe mashabiki wa kweli wangekuja kuangalia match ya timu yao ila wale walifata kelele za msemaji.
Hilo halina ubishi hata alivyohama Manara si watu wengi walihama au waliacha kufaifatilia simba? Au uongo?
Ngoja niwasubiri Mashabiki wa Simba waje wajisemee wenyewe!!!
 
Back
Top Bottom