soda hii ni hatari kwa maisha yetu

Mimi leo nilikuwa safarini toka dar kuja kaskazini, nilipofika pale mombo liverpool luxury restaurant nikanunua maji makubwa yana jina la kiarabu its like AL YA...... Yanatengenezwa Tanga. TENA YALIKUWA YAMEWEKWA KWENYE FRIJI YA MAJI YA KILIMANJARO, Kufika kwenye gari nafungua nagundua kuna deposit ya uchafu mweusi umetulia chini, ukitingisha vitu vinaelea tu. Imebidi niyaache yale maji.
 
Soda sijainywa madhara sijapata madai mahakamani inabidi niifungue ninywe niende hospitali ya serikali dr athibitishe kuwa nimedhurika kutokana na soda hii then kesi mahakamani itasukuma kama miaka miwili hv maana ubishani utakuwa mwingi then fidia yake milioni kumi tu wakati huo nahesabu masaa ya kuishi!!!

Acha kupiga kelele basi. Kama kitu kimetokea ni imani yangu sio nia ya mwenye kampuni. Kuripoti tukio panapohusika kutasaidia aliyesababisha uzembe huo awajibike na usirudiwe tena. Kukaa kimya na kuja kubwabwaja hapa ni kutafuta umaarufu na kuharibu biashara za watu. Au umetumwa na mpinzani wake?

Peleka hiyo chupa pale ubungo TBS au tuliza ball
 
Mimi siku hizi nimeacha kuagiza Sprite.. Ilikuwa ninakaribia kumaliza kuinywa,ndipo nikasense kitu cha kuteleza mdomoni,cha kuteleza mithili ya mayai mabichi,au makamasi...

Nilipoangalia kwa macho nikaona ni vitu vyeupe vinaelea... Nikamwaga hapohapo...

Hahahahahaha mbavu sina aroooooo
 
Acha kupiga kelele basi. Kama kitu kimetokea ni imani yangu sio nia ya mwenye kampuni. Kuripoti tukio panapohusika kutasaidia aliyesababisha uzembe huo awajibike na usirudiwe tena. Kukaa kimya na kuja kubwabwaja hapa ni kutafuta umaarufu na kuharibu biashara za watu. Au umetumwa na mpinzani wake?

Peleka hiyo chupa pale ubungo TBS au tuliza ball

Umaarufu ningekwenda kwny media (magazeti radio tv)live na siyo huku JF ambako hatujuani we punguani uliyetumwa na kampuni.
 
Soda hii nimeinunua jana kwa muuzaji wa jumla ilikuwamo katika kreti la soda ndani kuna kisoda ambacho inaonyesha kuwa mwywaji wa mwisho alikikunja na kukiweka ndani ya chupa na iliporudishwa kiwandani haikusafishwa kabla ya kujazwa soda nyingine hii ni hatari kumbe chupa hazioshwiiii maisha si salama tena cha kushangaza hadiinatoka kiwandani hakuna uhakiki wowote jamani ni hatariii!!tdfa mpoo na tbs mpooo!!!
Ndio maana mimi sinywi soda direct from chupa yaani labda mpaka na glass,coz hizo chupa hazioshwi vyema au hazioshwi kabisa,na ukizingatia hapo vinaingia vinywa vya watu tofautitofauti,wengine wanafungus midomoni,na wengine wanamatatizo kibao ya vinywa!!
 
Kunyweni vinyaji vya kopo. Hivi vya chupa recycled ni kansa tupu. Mi nilikuta mshumaa ndani.
 
Nakubaliana na wewe Amoeba Error zipo tena nyingi tu= chupa uoshwa na mashine,then kukaushwa kabla ya kujazwa soda, pia kuna sehemu ambapo watu hutumika kuangalia matatizo kwa macho kabla azijawekwa kwenye creti ukiangalia ni kwamba chupa usafishwa kwa maana ya kutoa mabaki ya soda na mtambo auna akili ya kusema au jinsi ya kukitoa kisoda hicho ,pia rangi ya chupa pamoja na rangi ya soda yenyewe na inspection time tatizo hili lazima linaweza tokea. Mzalishaji anaweza kushtakiwia lakini inabidi uisibitishie mahakama kuwa kile kisoda kilikuwepo ndani ya chupa wakati unanunua soda, na umepata madhara kwa kiasi gani kabla ujawa na kesi ya ukweli
Error zipop tu mama, hata kwenye noti ya Dollor huwa zinatokea! Sijui uoshaji wao uko vp, na uhakiki kabla ya kuruhusu chupa itumike ukoje; vyote kwa vyote error huwa zinatokea. Vp una mpango wa kuwawajibisha?
 
kwa kuwa leo nipo kwenye computer oneni vitu mnavyokunywa

View attachment Soda.jpg

attachment.php


soda 4.jpg


soda 4.jpg
 
Nchi nyingi duniani wameacha kutumia haya machupa ya kujazwa tena, watu mambo ni disposable tu. Bongo Bingo.
 
Umaarufu ningekwenda kwny media (magazeti radio tv)live na siyo huku JF ambako hatujuani we punguani uliyetumwa na kampuni.

Sasa unataka tukusaidiaje?

Siku ukigundua kuwa mumeo anatoka nje ya ndoa, utawashauri wanawake wenzio wote wawaache waume zao au utasolve matatizo yenu na mumeo. Shida ni kwamba, unaongea in terms of problems.

Ukienda Coca Cola utawasaidia wao kama wafanyabiashara kujua tatizo walilonalo, utawasaidia na wananchi wengine ambao hawatauona huu ujumbe wako hapa. Bidhaa ikirekebishwa ubora wake ndio kitu cha maana kitakuwa kimefanyika. Huu unaoleta hapa ni umbea tu wa kike
 
afadhali hii ni kisoda....kuna mdau mwingine alishalalamika pia
yakwake ilikuwa sprite na ndani ina condom (salama) ukitafuta
post za nyuma utaipata

Hii ndio shida yetu Watanzania. Hivi inasaidia nini kwako binafsi na kwa sisi wenzio ukija hapa kunung'unika na kuishia hapa?

Hivi kweli kwa akili yako unaona mwenye kiwanda chake anaweza akawa amewaelekeza wafanyakazi wake waweke condom kwenye chupa ilhali anajua ya kuwa ubora ndio msingi wa biashara yake?

Kutopeleka ushahidi sehemu husika ni upumbavu usio na shaka. Wale waliopewa kazi pale kiwandani ni Watanzania wenzetu, ila kwa kutokuwa kwao makini wanaleta yote haya. Ikiwa leo mwekezaji ataamua kuleta hadi waosha chupa kutoka kwao South Africa nadhani wote tutapiga kelele na nafikiri sheria haimruhusu.

Tusiwe watu wa kunung'unika kama mapanya. Jambo limetokea do the needful. Kuja hapa kuletea gumzo ambalo kwa maoni yangu nafikiri ni sehemu ya udhaifu wa jamii yetu ni ujinga. Akitolewa muosha chupa pale akawekwa kuhindi tutanuna, lkn wakati huu ambapo tuna uwezo wa kumsaidia mwekezaji kuboresha tupo nyuma kazi umbea na majungu.

Juzi juzi hapa tulikuwa na malalamiko oooh tiGO imefanya hivi mara tiGo imezua hili. Kama sio ndugu zetu vilaza (Wanaojiita wataalam) wa IT ni nani wa kulaumiwa ikiwa server ipo down? Kama leo mwekezaji wa tiGO angeruhusiwa kuleta wazungu wenzake kusimamia system, unafikiri tuongea madudu ya kupiga simu halafu uje ujumbe kuwa huna salio la kutosha wakati una 1800?!

Mfano mwingine ni hapa hapa JF. Mara ngapi jitu linalalama tuuu kuwa limetukanwa wkt hapo pembeni kuna button ya Report Abuse, halibonyezi, liaona kulalamika ndio solution.

Haya mambo ya umbea mnayoyafanya hapa, hayaisaidii Tanzania kama Taifa. Coca Cola ikikosa soko kwa ujinga wamuosha chupa akisaidiwa na aliyeona kizibo na kuacha kutoa taarifa sehemu husika ili wanaofanya huu uzembe wachukuliwe hatua, kitakachotokea ni kwamba kampuni itashindwa kujiendesha na kiwanda kitafungwa. Kiwanda kikifungwa ndugu zetu wengi watakosa ajira, hata wale waliofanya kazi yao kwa uaminifu mkubwa. Sasa huu ni wakati wa nyie wenye ushahidi kuisaidia jamii yetu kuimarika kwa kurekebisha makosa.

Kukuta kizibo ndani ya chupa ya soda sio uvumbuzi wa mtu kujinadi as if ameunda mtambo. Jambo sahihi ni kuripoti ili mzembe aondolewe, na walio waaminifu wasipoteze ajira zao kwa kiwanda kufungwa.
 
Sasa unataka tukusaidiaje?

Siku ukigundua kuwa mumeo anatoka nje ya ndoa, utawashauri wanawake wenzio wote wawaache waume zao au utasolve matatizo yenu na mumeo. Shida ni kwamba, unaongea in terms of problems.

Ukienda Coca Cola utawasaidia wao kama wafanyabiashara kujua tatizo walilonalo, utawasaidia na wananchi wengine ambao hawatauona huu ujumbe wako hapa. Bidhaa ikirekebishwa ubora wake ndio kitu cha maana kitakuwa kimefanyika. Huu unaoleta hapa ni umbea tu wa kike

Sema usemayo, kama soda ni chafu ni chafu tu,
na tutayabandika tu hapa hapa jamvini.
 
Sema usemayo, kama soda ni chafu ni chafu tu,
na tutayabandika tu hapa hapa jamvini.

Sio nia yangu kubishana na watu wa aina yako, lkn jua kuwa ili jamii yetu iwe bora, tunalazimika kuirekebisha na sio kuikosoa. Muosha chupa na aliyeona condom na asifikishe taarifa mahali panapohusika wote wanahatarisha ajira za wafanyakazi wengine waaminifu wa kampuni inyotengeneza hizo soda.

Hivi unaamini kama mwenye kiwanda ndio angekuwa anaosha chupa, angeacha chupa hata moja ipite na uchafu?
 
Sema usemayo, kama soda ni chafu ni chafu tu,
na tutayabandika tu hapa hapa jamvini.

Labda nikuulize kwa namna nyingine Miss. JF Premium Member.

Mbuzi wa jirani yako wakiingia shambani kwako na kusababisha uharibifu wa mazao, unaona ni lipi sahihi la kufanya:
1. Kuwawajibisha mbuzi kwa kuwakata miguu
2. Kumwajibisha mchunga mbuzi kwa kumripoti kwa mwenye mbuzi ambaye bila shaka atamfukuza kazi
3. Kutofanya A wala B badala yake kupita mitaani kuhubiri kwa watu kuwa mbuzi ni wabaya?

Natamani mmoja wa waliopata bahati mbaya ya kukutana na uchafu angefikisha jambo hili TBS na TFDA ili wazembe wachache wenye kusababisha yote haya wafukuzwe na waajiriwe wengine waaminifu kwa kazi yao. Kwa kufanya hivi, Coca Cola itaendelea kuboreka, afya zetu zitakuwa salama na ndugu zetu wanaopata riziki zao kwa kufanya kazi pale nao wataendelea na ajira zao.

Narudia tena, sidhani kama ni lengo la mwekezaji ni kuzalisha product chafu. Hii ni incompetence ya watanzania wenzetu waliopata nafasi ya kuajiriwa hapo.

Chuki dhidi ya SODA ni ujuha, tuelekeze chuki zetu kwa mzembe anayesababisha hali hii. Naamini waajiri (wawekezaji) linawaumiza zaidi ya mnavyofikiri, ndio maana wanaatempt kutufukuza kazi mara kadhaa lkn sheria zetu mbovu zinatulinda na kutufanya tuwe wazembe zaidi kazini.
 
Back
Top Bottom