Social Networking/Mitandao ya ki-Jamii...


...hahaha, wewe ni miongoni mwa wale msovua pete ya ndoa hata kama kuti lishadondoka...
nice one, ushajichongea kuweka status yako hadharani, endelea nayo tu...wengine tupo tupo kwanza,
hatuna status japo nililazimishwa niweke eti married to, ebo?!...lol



...aisee kama ni sukari basi ishaingia sumu,...sawa na kufunga upepo 'Dengu Beach' pale Ocean Road na lile shombo la mwani.
 
Mapenzi nayo ni kitu cha msingi kakondoo. . . muhimu watu wasichakachue na kuharibu maana.

Sasa kama yanageuka disaster, kwanini watu wasijichimbie zaidi kwenye mambo mengine jamani?? Alafu inaonesha kama wanachokifuata ni hicho tu......maanake hizi case sasa ni too much!!!
 
Reactions: Mbu

....daaahhh, pole bana....duhhhh!?




...unataka kuniambia ujanja angefanyaje hapo naye lengo lake labda ilikuwa ni cheating?

Ahsante ndugu. Maana alikuwa anacheat na mamsap wake unknowingly.
Sijui alipagawa na sura, maana niliweka picha bomba acha, na nikawa namchombeza kweli kweli. Just kupima uaminifu wake na kuthibitisha yale niliyokuwa naletewa kuhusu yeye.
 
Reactions: Mbu
We acha tu Lizzy, tulipokuwa tunachart wakati mwengine nilikuwa nacheka, s'times nilikuwa naumia kweli kweli. Akinikosa tu net msg ktk simu analalamikaa. Na hajui anamlalamikia mtu anamjua in and out. Na ni moja ya vitu vilivyofanya tukatengana.

...aiseee,....kukosa uaminifu ni kitu mbaya sana na hizi social networks zinatusaidia sana kubaini mapungufu ya wenza wetu,
ebana weee!? sikupi pole, nakupa hongera kunasuka.


.....Duh! Makubwa haya!!!!!

...kaka ni balaaa!....we yasikie tu hivi hivi haya...
huu ni ushuhuda tosha wa haya matufani,...sasa nisikilizie kwenye Twitter nako,...
watu wananasana si mchezo...utadhani vidole vyaop vimelaaniwa...

kwani lazima ku update status? aaarrghhh?
 
Reactions: BAK

Wengine wanasema kabisa wenzao hawaifahamu JF na hawatokaa wawaonyeshe/tambulishe JF kwao. Pengine ili wasikose uhuru wa hizo "innocent flirting" .
Wengine wanadai hazina ubaya ilhali hawawezi kushea na wenzi wao. Sasa hivi kutokua kwenye mahusiano kunaleta amani sana, tofauti na kuwa na mtu ambae hata kwenye hiyo acc yake ya facebook hauko kwenye list ya marafiki zake.
 
Reactions: Mbu

Mpaka aliyenunua aje kunidai. . . Lolzzz
Hahaha. . . hiyo ya kulazimishana nayo haijakaa sawa. Ila ukikataa lazima uulizwe "kwani unamuogopa nani" kabla ya kununiwa.

Sasa kama yanageuka disaster, kwanini watu wasijichimbie zaidi kwenye mambo mengine jamani?? Alafu inaonesha kama wanachokifuata ni hicho tu......maanake hizi case sasa ni too much!!!

Ndio maana wengine tunaangalia kama movie tu kakondoo. Kama na wewe unaweza karibu ila waliopo uwanjani watacheza tuuuuuu mpaka siku watakapokosa nguvu, so we angalia tu na kujifunza.
 
Reactions: Mbu

kweli mwanagu ila tambua kwamba "mtenda hutendwa" na matumizi ya majina bandia ni mazuri coz kinachotakiwa ni kujielewa, kujiheshimu,kujitambua na kujipanga ili gurudumu la Jf lisonge4ward.
 

...hahahahaa, bro NN mimi hunichekesha wale wanaotongozana kwa mvuto wa Avatar na ID, tena wengine hufikia mbali kweli kumbe mtu anatongozana na dume mwenzake...

...halafu jamiiforums ilivyo addictive, unaweza kuta mume umejilaza kitandani, mke yupo busy na smartphone yake anajibu pm ya mbu....sasa bahati mbaya ukute na mume sio mwelewa hapo, duuuh!....mbu ananuniwa buree maskini na thread zake...
 
Reactions: BAK
Wengine wanasema kabisa wenzao hawaifahamu JF na hawatokaa wawaonyeshe/tambulishe JF kwao. Pengine ili wasikose uhuru wa hizo "innocent flirting" .

Sasa hapo panakuwa patamu zaidi pale ambapo na hao wenza wao wanakuwa wamo humu JF halafu nao wanakuwa wanafikiri hao wenza wao hawamo humu. Yaani wote mpo halafu wote mnadhani mwenzio hayumo na haijui JF na hutakuja umfahamishe lol. Yaani full usanii to the nth degree.

Wengine wanadai hazina ubaya ilhali hawawezi kushea na wenzi wao. Sasa hivi kutokua kwenye mahusiano kunaleta amani sana, tofauti na kuwa na mtu ambae hata kwenye hiyo acc yake ya facebook hauko kwenye list ya marafiki zake.

Facebook, facebook, facebook! Hii Facebook hii.

Halafu kuna ile unamuomba boyfriend au girlfriend wako urafiki huko Facebook halafu haku-add lol. Unaanza kuwaza na kuwazua kulikoni...kwa nini hataki kuni-add....hataki nione nini....na maswali mengine lukuki. Ukimuuliza kwa nini hajaku-add anakupa lame excuses tu. Baada ya siku mbili unaona idadi yake ya marafiki imeongezeka kutoka 180 na kuwa 185 ilhali wewe alikuambia hakuweza kuku-add. Mweeeh!
 
Reactions: Mbu

Tulikuwa wachumba shostii, ndoa ilikuwa bado, ila on process.
Kwanza akaanza kujifutua, maana nilianza na mengine kwa upole tu na unyenyekevu wa high degree. Akakanusha, na akazidisha jeuri akasafiri na kusafiri. Afu akasugest ananiacha eti nina malalamiko na namsingizia sana through sms. Upande wa pili anadeka kweli kweli, eti anataka anione, aonje utamu wangu. Yeye yupo alone, na yuko conviced mimi ndo mke anaemhitaji. UPOO. Tukapanga kuonana mkoa tofauti na tulipo but hajui anapanga na mm. Tatizo likaja kwa sbb za kiafya nilikuwa bedrest na sikuruhusiwa kusafiri. Ndo nikaamua kumwaga ugali, nikimuuliza yote unadeny na hili? Stori ni ndefu shosti na kuna mengi ndani yake, i wish ndo ningekuwa nakuelezea face to face ingenoga. Facebooook!
 
Sasa kama yanageuka disaster, kwanini watu wasijichimbie zaidi kwenye mambo mengine jamani?? Alafu inaonesha kama wanachokifuata ni hicho tu......maanake hizi case sasa ni too much!!!

...na bado,...kuna mwingine kashikwa koo majuzi kulazimishwa a log in na mumewe aone kama kuna mtu online kwenye skype, sasa hii ndio nini tena jamani?....


Ahsante ndugu. Maana alikuwa anacheat na mamsap wake unknowingly.
Sijui alipagawa na sura, maana niliweka picha bomba acha, na nikawa namchombeza kweli kweli. Just kupima uaminifu wake na kuthibitisha yale niliyokuwa naletewa kuhusu yeye.

dahhh,....kwa mtazamo wangu, wengi wanaangukia kwenye ulimbo wa "fantasy world" jamani....tuwahurumie tu.
Nishajionea profile pics za celebrities lakini bado watu macho na udenda unawatoka....



...hahahahaa,...hiyo sentensi yako ya mwisho umenichekesha sana..na kweli ndipo tulipofikia.
Mume/mke kwakuwa hayupo kwenye friends list inazua pia 'kasheshe!'
 
Najaribu kujiuliza hivi hawa siku wakija kugundua walikua wanaflirt na waume/wake zao wenyewe nani atakua wa kwanza kumlaumu mwenzake? Nani atakua na ujasiri wa kumwambia mwenzie hajatulia? Au ndio kila mmoja atajikausha kama vile hamna kilichotokea?




Hahahaaha. . . yale yale ya "privacy muhimu". Yani mtu anakua na mambo ambayo watu wengine lukuki wanaweza kuona isipokua mpenzi wake!! Hapo ukute simu nayo haruhusu iguswe, JF yupo ila hajawahi.hata kumdokeza mwenzie. Nadhani watu wengine hawana haja ya kua kwenye mahusiano (wasio waaminifu, wasiotaka wenzi wao hata wafahamu kuna JF wakati ye anadai anafaidika nayo, wanaotaka kila kitu kibaki kuwa chake chake ) maana mwisho wa siku wanaishia kusumbuliwa na kukoseshwa raha tu na uwepo wa wenzi wao.
 
Reactions: Mbu

Mbu namaanisha kuwa sio lazima uone wivu kwa kila neno au nukta iliyopo kwenye ujumbe, hata kama anachat na ex wake.......kuna haja gani ya mimi kulipatia maana mbili mbili kila linaloandikwa na kuanza kuhesabu kila like wanayopeana??
 
Reactions: Mbu

Dah!!
Ila afadhali ulimsoma mapema ukampotezea , ungekua ushakua mke mara ndugu kibao wakushinikize uvumilie ungekua unalia kilio kingine.

MBU huyo wa skype nae hajatulia. Hivi kumbe ndani ya kuta nne kuna vituko hivyo?
 
Reactions: Mbu

Mkuu NN wewe unasema boyfriend na girlfriend, mwenzetu Kokutona mkewe alikataa kumu-add ikabidi aingie kwa gia nyingine, yaani usanii wa hali ya juu.
 

Ndo yaliyonikuta mimi, nikaamua kujitengenezea jina bandia, picha bandia. Nikaomba urafiki. Sikutaka shida ya kulumbana nae why hataki kuniadd. Na udhalimu wake ukawa hadharani.
Inaumaaa na ni ngumu kumeza i see
 
Reactions: Mbu

...hahahaha, huu mfano hai ulioweka jf noma....ndio maana mimi si entertain kuhudhuria vikao vya jf, nisijepigwa chupa bure kwa kosa la ku flirt na mali za watu!


...ila hiyo ya kuomba friend request mwenza wako halafu aku ignore inauma hiyo acha aisee....au ana ku add kisha baada ya siku chache unakuta kesha ku delete...hahahahaha!



...umeona ee? basi hii ndio hali iliyofikia kwenye hii mitandao ya kijamii na athari zake...
mtu ana share kila kitu na ulimwengu mzima, ila mwenza wake hapewi access, aisee inauma kweli!


Hata ukijifanya kujisahaulisha, sumthing at the back of your mind kitakuwa kinakuwasha utafute by any means ujue anaficha nini...ngumu kupuuzia aisee
.
 

Ndo hivyo mkuu.
I loved him, then he take the advantage.
Ila huwa najiulizaga kuanzisha mahusiano na mtu usiyemjua na huna uhakika km kweli mtaweza onana. Eti ukampenda kabisa afu na kupropose juu inawezekanaje? Tena mtandaoni. Kweli tunatumia technologia vibaya mno!
 
Reactions: Mbu

Ndo wale wanaojifanya wao wanajua kuwaomba wenzao urafiki na kuandika kwenye status "married to, in a relationship with" wajifunze kusoma alama za nyakati. Kama mwenzako ana mambo ambayo haoni tabu kushea na ulimwengu isipokua wewe basi jua umepatikana. Kama bado hamjafungana pingu huo ni wakati wa kukimbia, kama mmefungana ni wakati wakuwekana sawa. Hamna haja ya kulazimishana/kuombana vitu vidogo vidogo ambavyo vilitakiwa vitoke kwa hiari.
 
Reactions: Mbu
Mbu namaanisha kuwa sio lazima uone wivu kwa kila neno au nukta iliyopo kwenye ujumbe, hata kama anachat na ex wake.......kuna haja gani ya mimi kulipatia maana mbili mbili kila linaloandikwa na kuanza kuhesabu kila like wanayopeana??

...basi you are one in a million...kuna watu wakifika nyumbani tu, cha kwanza mke/mume anaikagua mobile phone kisha anaiweka kibindoni mwake mpaka kesho utapoenda kazini, kila sms au simu itayoingia ataisoma au kuipokea yeye kwanza.....kwenye social network ndio balaa...anataka kujua sababu, nia na madhumuni ya kupewa comment, like, au tagged!

Dah!!
Ila afadhali ulimsoma mapema ukampotezea , ungekua ushakua mke mara ndugu kibao wakushinikize uvumilie ungekua unalia kilio kingine.

MBU huyo wa skype nae hajatulia. Hivi kumbe ndani ya kuta nne kuna vituko hivyo?

...eeeh? ushaona mtu anakusimamia u log in skype, au msn messenger kwakuwa anajua kuna live video, kisha yeye anajibanza nyuma ya kiti? paropokwe neno tu hapo,

...akikukosa huko, ana-print chat history!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…