Ngwananzengo
JF-Expert Member
- Jul 28, 2012
- 1,911
- 1,320
Kuwa na mwanamke mzuri asie na akili, ni sawa na Pete ya dhahabu kwenye pua ya nguruwe.
Mimi ni kijana mabaye nimeoa na nimebahatika kupata watoto wawili na huyo mke wangu. Mimi ni mtu ambaye sipendi kuanika sana mambo yangu na familia yangu hadharani hasa kwenye social media. So hio ni tabia yangu na mke wangu nilimjulisha mapema sana.
Katika siku za hivi karibuni huyo mwanamke ameanza tabia za kupost mapicha facebook ambazo zinadegrade image yangu na ninapomkataza anasema anapost picha zake binafsi kwa hio mimi hazinihusu. Lakini pia amekua anapost mambo ya nyumbani kwangu kwenye profile zake. Kama mumeuziana kuhusu ishu fulani basi ataweka facebook message ambazo unaona kabisa ni madongo kwangu. Kwa hio nikaamua ku-unfriend nae kwenye facebook lakini hayo mambo yamehamia whatsapp na viber.
Ukiondoa maumivu ya kauli zake za mdomoni, hii ishu ya facebook tumeshindwa kuelewana kabisa. Na kimsingi mimi mapenzi naye ni kama yamekufa kwani sijisikii kuendelea nae kabisa. Mpaka sasa hakuna la maana linaweza kuendelea kuendeleza hii familia maana pesa zangu nyingi imebidi niwekeze kwingine kwa siri ili nisikilizie hii ndoa inaendeleaje lakini naona hakuna future mpk sasa. Na mimi nataka kujijenga mahali napoishi kwa sasa. Maana nimejikuta nawekeza pesa mahali ambapo hapatanisaidia sana kwa muda huu na pia ni mbali na napo ishi mangement ni ngumu sana.
Nimerealize niko na wrong woman na napoteza muda wangu. Mimi ni mtu ninaejiheshimu na matendo yake nayona kama yana degrade sana image yangu kwenye jamii. Lengo langu hasa ni kuachana nae na kuishi bila kuoa tena ili niweze kulea watoto wangu kwa uhuru bila hofu ya kusumbuliwa na mama wa kambo.
Nawaomba wenye experience wanisaidie ushauri maana hili jambo nimedhamiria kulifanya mimi mwenyewe bila kumshirikisha mtu. Tutumie lugha nzuri sio ya kuniongezea maumivu mpaka nikajuta kushare nanyi.
Nashukuru sana kwa ushauri wako ambao nikili uko vizuri sana. Nimemweleza yote na nimeenda nae pole pole sana lakini ni kama anafanya mambo kunikomoa. Nasema hivi kwa sababu kitu unachomwambia hukipendi yeye anakifanya muda huo huo ili kukuonesha kua anakifanya. Mimi nimehisi kua anaweza kua na spiritual hasband lakini hata jeuri na kiburi kinachangia sana. Suala la kuvunja ndoa nimelikifiria sana for 5 months now. Ukweli kutoka moyoni ni kua sioni future ila naona naweza kufa mapema. Sipendi kucheat ni maisha ambayo nimeyakataa toka moyoni na hua nipo clear sana.Duu!! sasa sijui tuanzie wapi. Maana tukisema uende kwa washauri, Juzi humu ndani habari imeletwa MSHAURI ANATEMBEA NA MKE WA MSHAURIWA.
Cha msingi, Tulia mweleze kila kiu, na impact ya maamuzi anayochukua ya kutokukusikiliza. Tulia tafakari angalia faida na hasara ya kutokuwa na MKE, Usisahau sala, kama unaamini katika Kufunga FUnga, Ili upate uamuzi wenye nguvu wa Hatma ya maisha yako. Tulia kwanza mkuu, Kufunja ndoa ni rahisi lakin madhara yake ni makubwa kwako na kwa watoto.
Mkuu unavyo ongea inamanisha umevumilia mengi sana tumbua ilo jipu mkuu
Unataka Acha mke kisa Facebook tu??angalia hayo madongo ni Yapi,ana maumivu ya kihisia probably, muweke karibu mke yapaswa umjali na ajue unampenda, then mweleweshe tu upya asiweke ishu zenu huko
Pia na wewe mara moja moja si mbaya kumuweka mkeo watsap na fb,tafta picha kapendeza muweke mtag, caption hata ndogo tu 'my wifey' inatosha kumpa raha ajijue unampenda, to her anaamini kuwekwa mitandao ya kijamii ni mapenzi
Ila grow up mke haachwi kirejareja hivo
Kabla hatujaenda mbali...Hizo picha za facebook zilizoku"degrade" ni za aina gani? Za uchi?????
I
Maana haileti picha kuwa picha tu zisababishe mapenzi yaishe.... msisshirikishane kiuchumi nk nk
Pia hebu jikague mpaka mkeo kero anapeleka fb..basi mna tatizo kubwa ....
Pia hamjaoa malaika ...kama madhaifu yako anakuvumiloa kinachokufanya ushindwe kumvumilia ni nini?[/QUOTE
Picha ni picha cha msingi ni amani ya moyoni kwanza. Haijarishi picha sio za uchi kama mwenzako hazipendi unapaswa kumsikiliza ndio maana ya ndoa. Mambo ya kiuchumi yani pele unapomsogeza karibu kwa kumshirikisha ndio tabia inabadilika sana. Hasa nilipoanza kumpa priority kubwa sana ndio maumivu yamezidi mara 100.
Kuna ishu ambayo naiona pengine ni maturity lakini haiendani na umri. Kwa umri wake ni mtu amabe inapaswa afocus kwenye familia kwanza kama priority ya kwanza. Na tabia za kupeleka kila tukio katika public wall ni dalili ya imaturity au kuna shida ya makuzi.
Kuna mengi tunavumilia lakini inapofikia unapoteza future yako ambayo umeisotea kwa maisha yako yote. Nafikiri hata katika hatua za uokozi wa majonga kuna order ya priority inayofuata. Tunaambiwa jiokoe kwanza wewe then ndio fikiria mtu mwingine. So ilipofika ni kama nahitaji kuokoa future yangu ambayo nimeinvest miaka yangu yote hapa duniani. So hatutegemei wasiwe na makosa but waelewe pale wanapoelekezwa
kwa hiyo kaenda kuanika siri zako kwenye mitandao kuwa jamaa ni kibamia?!
kuna umuhimu wa kuwashirikisha watu was karibu yenu kama vile wazazi wa pande zote mbili km unaona ushauri na maonyo yako hayatilii maanani
How?you should acy like a man
Ndio kitu amabacho ninapangilia kwa sasa hasa kuangalia vipengele vya kisheria lakini pia kulinda heshima ya kila mtu. Ninajaribu kumshauri tuachane kwa amani japo hataki lakini ninamuandaa kisaikologia ili lisiwe jambo la kushtukiza tu. so nakwenda nalo pole pole huku nikijiandaa hasa kisaikologia na natumaini ndani ya huu mwaka mambo yatakamilika yote.Umeshaamua kumuacha, fuata taratibu zinazofaa.
Kumpiga chini kwa issue hiyo ndogo sio busara unless yapo mengii ambayo hajayaelezaHahitaji kumnyanyasa apige chini tu, huyo atakuwa ana mchepuko unamzuzua akichelewa yeye atamwahi.
Lakini issue ni hiyo tu bro au na wewe hukumpenda kivileee heb eleza ukwelNdio kitu amabacho ninapangilia kwa sasa hasa kuangalia vipengele vya kisheria lakini pia kulinda heshima ya kila mtu. Ninajaribu kumshauri tuachane kwa amani japo hataki lakini ninamuandaa kisaikologia ili lisiwe jambo la kushtukiza tu. so nakwenda nalo pole pole huku nikijiandaa hasa kisaikologia na natumaini ndani ya huu mwaka mambo yatakamilika yote.
Unazungumza na mkeo shida zenu? Ukimkera akikuambia upo tayari kuyaongea??
Make watu wengine hamuambiliki mtu anaona ajifariji mtandaoni na ujumbe utaukuta mtandaoni
Wengine njia hiyo inajenga ha ha ha ha haNafikiri hakuna situation ambayo inafanya mtu mzima na akili yake aweke family matters kwenye public walls. Kuna mambo we disagree kabisa lakini mazungumzo ni priority number one. Maana mtu anapoamua kubehave immaturely hapo ndo shida inaanza. Kwanza haijengi zaidi ya kubomoa. Maana hata kama kulikua na masikilizano kidogo inaua kabisa hata hio kidogo. Pili, hata kama kulikua na mapenzi nayo yanakufa. Situation inakua mbaya kuliko mwanzo, ndio maana wahenga wanasema ziba ufa kabla hujajenga ukuta. Nafiri nidhamu kwanza mengine baadae. Hata kama unakereka ni vizuri ukatumia heshima kuwasilisha ujumbe wako. Hakuna mume anaejitambua atakusikiliza kama humuaproach kwa heshima.
Hahahahaha aisee umeongea kitu cha msingi sanaUkishakamilisha taratibu za kumuacha hakikisha unaenda kuwaomba radhi mliowachangisha michango ya harusi kwa utapeli mliowafanyia. Ndo mana nilishaacha kuchangia michango ya harusi unakuta limtu kila siku mimassage ya mchango ukilichangia baada ya mwaka linaanza kusema eti huyu sio chaguo langu kweliiiiii!!!!! shame on you