Social media na ndoa yangu

PIMs

Member
Feb 24, 2016
59
49
Mimi ni kijana mabaye nimeoa na nimebahatika kupata watoto wawili na huyo mke wangu. Mimi ni mtu ambaye sipendi kuanika sana mambo yangu na familia yangu hadharani hasa kwenye social media. So hio ni tabia yangu na mke wangu nilimjulisha mapema sana.

Katika siku za hivi karibuni huyo mwanamke ameanza tabia za kupost mapicha facebook ambazo zinadegrade image yangu na ninapomkataza anasema anapost picha zake binafsi kwa hio mimi hazinihusu. Lakini pia amekua anapost mambo ya nyumbani kwangu kwenye profile zake. Kama mumeuziana kuhusu ishu fulani basi ataweka facebook message ambazo unaona kabisa ni madongo kwangu. Kwa hio nikaamua ku-unfriend nae kwenye facebook lakini hayo mambo yamehamia whatsapp na viber.

Ukiondoa maumivu ya kauli zake za mdomoni, hii ishu ya facebook tumeshindwa kuelewana kabisa. Na kimsingi mimi mapenzi naye ni kama yamekufa kwani sijisikii kuendelea nae kabisa. Mpaka sasa hakuna la maana linaweza kuendelea kuendeleza hii familia maana pesa zangu nyingi imebidi niwekeze kwingine kwa siri ili nisikilizie hii ndoa inaendeleaje lakini naona hakuna future mpk sasa. Na mimi nataka kujijenga mahali napoishi kwa sasa. Maana nimejikuta nawekeza pesa mahali ambapo hapatanisaidia sana kwa muda huu na pia ni mbali na napo ishi mangement ni ngumu sana.

Nimerealize niko na wrong woman na napoteza muda wangu. Mimi ni mtu ninaejiheshimu na matendo yake nayona kama yana degrade sana image yangu kwenye jamii. Lengo langu hasa ni kuachana nae na kuishi bila kuoa tena ili niweze kulea watoto wangu kwa uhuru bila hofu ya kusumbuliwa na mama wa kambo.

Nawaomba wenye experience wanisaidie ushauri maana hili jambo nimedhamiria kulifanya mimi mwenyewe bila kumshirikisha mtu. Tutumie lugha nzuri sio ya kuniongezea maumivu mpaka nikajuta kushare nanyi.
 
Duu!! sasa sijui tuanzie wapi. Maana tukisema uende kwa washauri, Juzi humu ndani habari imeletwa MSHAURI ANATEMBEA NA MKE WA MSHAURIWA.

Cha msingi, Tulia mweleze kila kiu, na impact ya maamuzi anayochukua ya kutokukusikiliza. Tulia tafakari angalia faida na hasara ya kutokuwa na MKE, Usisahau sala, kama unaamini katika Kufunga FUnga, Ili upate uamuzi wenye nguvu wa Hatma ya maisha yako. Tulia kwanza mkuu, Kuvunja ndoa ni rahisi lakin madhara yake ni makubwa kwako na kwa watoto.
 
Wakati nampata haya mambo ya facebook yalikua hayajashamiri sana
Nimekupata Kiongozi.

Pole sana, ndio ukubwa huo.

Kwa kila mkasa wa mwenzako inabidi kujifunza, mikasa ya kimapenzi inatokea kila siku
 
Tv na mitandao imewaharibu dada zetu hataree. Ukiona mkeo amebadilika kitabia ujuwe kuna kishetani mtu ndicho kinacho mbadilisha. Marafiki wengine wana tabia za kibinaadamu lakini wengine wana tabia za kishetani. Mimi na Jf tu hio mitandao mengine nayasikia tu.
 
kuna umuhimu wa kuwashirikisha watu was karibu yenu kama vile wazazi wa pande zote mbili km unaona ushauri na maonyo yako hayatilii maanani
 
Kabla hatujaenda mbali...Hizo picha za facebook zilizoku"degrade" ni za aina gani? Za uchi?????

I
Maana haileti picha kuwa picha tu zisababishe mapenzi yaishe.... msisshirikishane kiuchumi nk nk

Pia hebu jikague mpaka mkeo kero anapeleka fb..basi mna tatizo kubwa ....

Pia hamjaoa malaika ...kama madhaifu yako anakuvumiloa kinachokufanya ushindwe kumvumilia ni nini?
 
Unataka Acha mke kisa Facebook tu??angalia hayo madongo ni Yapi,ana maumivu ya kihisia probably, muweke karibu mke yapaswa umjali na ajue unampenda, then mweleweshe tu upya asiweke ishu zenu huko
Pia na wewe mara moja moja si mbaya kumuweka mkeo watsap na fb,tafta picha kapendeza muweke mtag, caption hata ndogo tu 'my wifey' inatosha kumpa raha ajijue unampenda, to her anaamini kuwekwa mitandao ya kijamii ni mapenzi
Ila grow up mke haachwi kirejareja hivo
 
Kama shida ni hiyo tu uaimwache

Mimi ni kijana mabaye nimeoa na nimebahatika kupata watoto wawili na huyo mke wangu. Mimi ni mtu ambaye sipendi kuanika sana mambo yangu na familia yangu hadharani hasa kwenye social media. So hio ni tabia yangu na mke wangu nilimjulisha mapema sana.

Katika siku za hivi karibuni huyo mwanamke ameanza tabia za kupost mapicha facebook ambazo zinadegrade image yangu na ninapomkataza anasema anapost picha zake binafsi kwa hio mimi hazinihusu. Lakini pia amekua anapost mambo ya nyumbani kwangu kwenye profile zake. Kama mumeuziana kuhusu ishu fulani basi ataweka facebook message ambazo unaona kabisa ni madongo kwangu. Kwa hio nikaamua ku-unfriend nae kwenye facebook lakini hayo mambo yamehamia whatsapp na viber.

Ukiondoa maumivu ya kauli zake za mdomoni, hii ishu ya facebook tumeshindwa kuelewana kabisa. Na kimsingi mimi mapenzi naye ni kama yamekufa kwani sijisikii kuendelea nae kabisa. Mpaka sasa hakuna la maana linaweza kuendelea kuendeleza hii familia maana pesa zangu nyingi imebidi niwekeze kwingine kwa siri ili nisikilizie hii ndoa inaendeleaje lakini naona hakuna future mpk sasa. Na mimi nataka kujijenga mahali napoishi kwa sasa. Maana nimejikuta nawekeza pesa mahali ambapo hapatanisaidia sana kwa muda huu na pia ni mbali na napo ishi mangement ni ngumu sana.

Nimerealize niko na wrong woman na napoteza muda wangu. Mimi ni mtu ninaejiheshimu na matendo yake nayona kama yana degrade sana image yangu kwenye jamii. Lengo langu hasa ni kuachana nae na kuishi bila kuoa tena ili niweze kulea watoto wangu kwa uhuru bila hofu ya kusumbuliwa na mama wa kambo.

Nawaomba wenye experience wanisaidie ushauri maana hili jambo nimedhamiria kulifanya mimi mwenyewe bila kumshirikisha mtu. Tutumie lugha nzuri sio ya kuniongezea maumivu mpaka nikajuta kushare nanyi.
 
kuna umuhimu wa kuwashirikisha watu was karibu yenu kama vile wazazi wa pande zote mbili km unaona ushauri na maonyo yako hayatilii maanani
Binafsi ikifika stage hatuwezi kuelewana mpaka tutafute msaada kwa wazazi sijui wa pande tatu, basi hapo penzi ni la kulazimisha na linatesa pia halina furaha ndani yake. Siwezi kufika stage hiyo aisee
 
Kwenye kufunga hapo ni mtihani, maana Mungu siku hizi hata sala ni kama hasikilizi tena, Maovu yamezidi. Na wanaoyafanya na kuyatenda ni sisi
Duu!! sasa sijui tuanzie wapi. Maana tukisema uende kwa washauri, Juzi humu ndani habari imeletwa MSHAURI ANATEMBEA NA MKE WA MSHAURIWA.

Cha msingi, Tulia mweleze kila kiu, na impact ya maamuzi anayochukua ya kutokukusikiliza. Tulia tafakari angalia faida na hasara ya kutokuwa na MKE, Usisahau sala, kama unaamini katika Kufunga FUnga, Ili upate uamuzi wenye nguvu wa Hatma ya maisha yako. Tulia kwanza mkuu, Kufunja ndoa ni rahisi lakin madhara yake ni makubwa kwako na kwa watoto.
 
Back
Top Bottom