Son of Gamba
JF-Expert Member
- Oct 26, 2012
- 4,358
- 6,077
Kwa wale wenzangu ambao ni mashabiki wa mpira wa miguu hasa wa timu za Ulaya, mnaletewa kitu kipya kinaitwa Dugout.
Mtandao huu unafanya kazi kama vile facebook au Instagram lakini wenyewe unahusu habari za wacheza mpira wa miguu pekee. Uzuri wa mtandao huu tofauti na facebook au Instagram, ni kwamba unaweza kuwaona wachezaji wote bila haja ya kumfollow mmoja mmoja. Hapa utakutana na timu unayoipenda na pia unaweza ukafuatilia kwa karibu timu nyingi sana kwa wakati mmoja.
Mimi nimeanza kuutumia na hakika nimefurahishwa sana. Pia ndani ya mtandao huu utakutana na fans wenzako na mnaweza kujadili mambo yoyote yale kuhusu timu mnazozipenda. Nilichokipenda zaidi pia humu ndani ya mtandao huu unaweza kuona mechi mbali mbali zilizochezwa na pia kuna clips fupi za wachezaji wakiwa kwenye mazoezi, au mahojiano na waandishi.
Mtandao huu unafaa sana kwa wale wazee wenzangu wa kuweka "mikeka" kwani utakuwa unakupa taarifa za wachezaji mbalimbali unaowafuatilia hivyo itakuwa rahisi kwako kujua nani yuko fit au la.
Namna ya kujiunga, ingia, Dugout - Football Inside Out na utapewa maelekezo namna ya ku join. Karibuni tufurahie soka!
Source; BBC NEWS