Sober house zichunguzwe na kusaidiwa

Sober house zichunguzwe na kusaidiwa

and 998 others

JF-Expert Member
Joined
Jun 27, 2012
Posts
28,224
Reaction score
39,704
Kumekuwepo la ongezeko kubwa la matumizi na athari za dawa za kulevya nchini, hasa mijini, hivyo watu kwa utashi wao wameamua kuanzisha
"Sober House". Lakini watu kadhaa waliowahi kwenda huko, matokeo yao hurudia hali kutumia madawa kwa kasi ya ajabu.

1. Nini hasa hufanyika humo ndani?
2. Sifa za kitaaluma (Saikolojia/ushauri nasaha, kitabibu/udaktari za wanaohudumia hizi nyumba)
3. Nini malengo makuu ya muanzilishi wa hizi nyumba? Nani hufuatilia? wanawajibika kwa nani?

USHAURI;
i. Zisajiliwe kisheria (kwa kufuata vigezo vya miundo mbinu & Taaluma pia Wizara/manispaa ifuatilie kwa karibu sana.
ii. Zisaidie pale amabapo kuna mapungufu kwani kwa kiasi fulani zinasaidia vijana walioathirika na madawa ikiwemo UKIMWI.
 
Utagundua Sober House na vinavyoitwa vituo vya watoto yatima vinaendeshwa na waswahili swahili, huenda hata mambo yanayofanyika humo ndani ni ya kustaajabisha!
Waziri wa afya tafadhali fuatilia hili vijana na watoto wanapata nini kwenye hizi nyumba?
 
Naunga mkono hoja...serikal iingilie kati na kuvisaidia na kuvisimamia
 
Kwa uchunguzi wa haraka haraka (sijafanya uchunguzi wa kina) Vituo hivi vinaendeshwa kwa kutegemea misaada ya wahisani, hivyo wajanja huenda wakajipenyeza humo ili kukomba hiyo misaada. Mambo mengine hawana habari nayo.
 
Hili ni ombi maalum kwa Waziri wa Afya pia Waziri wa Mambo ya Vijana.
 
Nachelea kusema Sober House nyingi ni machimbo ya wauza/wala unga. Hakuna uangalizi/ufuatiliaji. Pasipoangaziwa ipo siku majumba hayo yatalipuka kwa wingi wa dhambi zinazofanywa humo.
Pia, hata jamii za jirani hazijishughulishi kwa lolote na mi-sober hausi hiyo. Wengi hupaogopa kama GEREZA.
 
hivi wasomi wetu hawawezi kuandikia proposals hizi sober house wakaja na miradi mikubwa ya kusaidia vijana wetu, kuliko kuwaachia makanjanja juendesha hivi vituo?
 
Kigwangala yumo humu JF? If yes, basi amesikia, ameona atalifanyia kazi
 
Kumekuwepo la ongezeko kubwa la matumizi na athari za dawa za kulevya nchini, hasa mijini, hivyo watu kwa utashi wao wameamua kuanzisha
"Sober House". Lakini watu kadhaa waliowahi kwenda huko, matokeo yao hurudia hali kutumia madawa kwa kasi ya ajabu.

1. Nini hasa hufanyika humo ndani?
2. Sifa za kitaaluma (Saikolojia/ushauri nasaha, kitabibu/udaktari za wanaohudumia hizi nyumba)
3. Nini malengo makuu ya muanzilishi wa hizi nyumba? Nani hufuatilia? wanawajibika kwa nani?

USHAURI;
i. Zisajiliwe kisheria (kwa kufuata vigezo vya miundo mbinu & Taaluma pia Wizara/manispaa ifuatilie kwa karibu sana.
ii. Zisaidie pale amabapo kuna mapungufu kwani kwa kiasi fulani zinasaidia vijana walioathirika na madawa ikiwemo UKIMWI.
Sober house nyingi ni za wauza unga
 
Sasa UKIMWI ni madawa nayo, ah 😂😂😂😂
 
Back
Top Bottom