Sniper wa Kikanada avunja rekodi ya dunia

Sniper wa Kikanada avunja rekodi ya dunia

EWGM's

JF-Expert Member
Joined
Jul 22, 2013
Posts
1,521
Reaction score
2,112
Sniper au mlenga shabaha hodari wa Kikanada ameweka rekodi kwa kumtungua gaidi wa kikundi cha IS (Islamic State) “daesh”aliyekuwa umbali wa zaidi ya takribani maili 2. Katika kuweka rekodi hiyo, Sniper huyo alitumia silaha aina ya “McMillan TAC-50 sniper rifle” akiwa juu ya moja ya majengo marefu inchini Iraq.
canadian-forces-kabul.jpg
C:\Users\ERIC-M~1\AppData\Local\Temp\msohtmlclip1\10\clip_image002.jpg


Risasi hiyo ilisafiri chini ya sekunde 10 kumi na kumuua gaidi huyo aliyekuwa umbali wa mita 3,540 (maili 2.19) umbali huo ni sawa kabisa na urefu wa kutoka kwenye kanisa la Mviringo (KKKT Magomeni) na kona ya kwenda Mabibo kutokea barabara kuu ya Morogoro.

Risasi hiyo iliweza kusimamisha tukio lillokuwa linaenda kutekekelezwa na magaidi hao dhidi ya askali polisi wa Iraq na tukio hilo zima lilirekodiwa na wenzake kwa mfumo wa video ili wahifadhi kwenye kumbukumbu zao.

Tukio hilo lilivunja rekodi iliyowekwa mwanzo na mwanajeshi (sniper) wa Kiingereza Craig Harrison aliyewahi kumpiga adui (taliban) risasi akiwa kwenye umbali wa mita 2,475 (maili1.53) nchini Afghanistan (Helmand Province) mwaka 2009 akitumia “L115A3 long range rifle”.

Kamanda wa kikosi cha Operesheni Maalumu cha Jeshi la Kanada alizibitisha hilo na ushahidi upo ila alikataa kusema ni lini tukio hilo lilifanyika kutokana na sababu maalum za kuisalama.

Walenga shabaha hao hodari huwa wanatakiwa kuweka mahesabu yao sawa kulingana na uvumi wa upepo, milima na mabonde na mruko wa risasi yenyewe ili iweze kutimiza malengo.

Hii ni habari nzuri kwa waziri mkuu wa Kikanada ambaye alisimamisha matumizi ya ndege za kudodonsha mabomu mwaka 2016 na kuhahidi kuongeza maradufu wanajeshi hao maalum na pia wa kawaida ili kusaidia kutoa mafunzo jeshi la Iraq.

McMillan TAC-50
379c413e3caac3f1cd042f4a7f2491b4.jpg


Source: BBC & Sky News
C:\Users\ERIC-M~1\AppData\Local\Temp\msohtmlclip1\10\clip_image004.jpg
 
Back
Top Bottom