SMS zimenifanya nimuoe shangazi yangu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

SMS zimenifanya nimuoe shangazi yangu

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by MziziMkavu, Nov 7, 2011.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Nov 7, 2011
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,616
  Likes Received: 4,617
  Trophy Points: 280
  INAWEZA kuwa kama simulizi lakini ni ukweli mtupu. Baada ya kujikuta nikimuoa shangazi yangu kutokana na kufanya naye mapenzi kwa njia ya simu kwa muda wa mwaka mmoja.
  Uhusiano wetu ulianza baada ya shangazi ambaye sasa ni mke wangu kukuta ‘missed calls' kwenye simu yake na kuamua kunipigia kutaka kujua mimi ni nani.

  Lakini katika hali ya kushangaza sikupiga simu kwake kwa sababu tulikuwa hatujuani hata kwa sura.
  Alipiga simu na kusema kuwa yeye yupo Arusha wakati mimi nipo Dar es Salaam. Nilimwambia kuwa sikumpigia simu kwa sababu sikumfahamu. Nilipomuambia hivyo alicheka na kukata simu.

  Zilipita kama siku mbili shangazi alinitumia sms ya kunijulia hali nami nikamjibu. "Habari yako kaka, nimeona leo nikukumbuke kwani tangu siku ile hatujaongea tena, nimekukumbuka kweli."
  "Usijali, tupo pamoja nami pia nimekukumbuka. Nilikuwa natafuta muda wa kukupigia simu lakini kutokana na kubanwa na majukumu nikashindwa."

  "Oke, hakuna shida, nikutakie siku njema ila kuna swali nilitaka kukuuliza kabla sijakuaga."
  "Swali gani tena hilo, wewe uliza tu nitakujibu usiwe na wasiwasi."
  "Samahani kama nitakukosea maana simu ndiyo imetufanya tujuane."
  "Kweli kabisa, nami nimekwambia usijali wewe uliza tu nitakujibu."

  "Umeoa?"
  "Hapana sijaoa, wewe umeolewa?"
  "Bado, nashukuru kwa kutambua hilo, nakutakia siku njema."
  "Oke, wewe pia Mungu akubariki kwa kazi uifanyayo."
  Baada ya muda nilianza kujiuliza kwa nini aliniuliza swali la kama nimeoa. Mara mawazo ya kimapenzi yakaanza kuutesa moyo wangu.

  Siku iliyofuata sms iliingia kwenye simu yangu kutoka kwa shangazi. "Hellow dear, mzima? Nimekukumbuka sana, natamani kuiona sura yako."
  Ujumbe ule ulinifanya nishtuke kidogo, lakini kwa kuwa mawazo yangu yalikuwa yameanza kuelekea kumpenda kimahaba mwanamke yule niliamua kumjibu.

  "Hellow sweat, mimi mzima hofu na mashaka ni kwako, nami pia natamani kukutana nawe ili niione sura yako."
  Tulianza kutumiana sms za mapenzi tangu siku hiyo. Nilimuuliza jina lake alinitajia moja tu la Susan. Sikuwa na mawazo kama angeweza kuwa ni shangazi yangu.

  Hali ya kutumiana sms iliimarisha penzi letu na kumfanya kila moja kuwa na shauku ya kumuona mwenzake.
  Tukiwa katika hali hiyo ya kuchati kwa njia ya sms, ilifika kipindi tukawa tunatoshelezana kwa njia hiyo kwani miili ilikuwa ikisisimka kwelikweli.

  Baada ya mwaka mmoja kuisha tulifanya taratibu za kukutana na tukafanikiwa kuonana na kuanza mikakati ya kuoana.
  Habari za kwamba yeye ni shangazi yangu zilijulikana baada ya kwenda kujitambulisha kwao. Ndugu zetu walishangaa kuona nimekuwa na uhusiano wa kimapenzi kwa njia ya simu na shangazi yangu.

  Kwa kuwa tulikuwa tayari tumeshamaliza kila kitu kwa njia ya sms, sikuona haja ya kusitisha uhusiano wetu, nikaamua kumuoa japo ndugu zetu wa pande zote mbili wameamua kututenga kwa madai kuwa tumewaaibisha

  Chanzo: http://www.globalpublishers.info/profiles/blogs/sms-zimenifanya-nimuoe-shangazi-yangu
   
 2. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #2
  Nov 7, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,806
  Likes Received: 420,394
  Trophy Points: 280
  hii inatisha sana................................umependa buzi kwenye begi...........................................sidhani huu ndiyo mwisho wa safari yako bado utayumbishwa sana na hili wimbi la mahaba...........hutatulia hivi karibuni naona safari ndefu usoni..................
   
 3. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #3
  Nov 7, 2011
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  hiki kisa kinavutia sana....... wakati mwingine wanandoa hukutana kwa njia za ajabu
  hao waliowatenga wana lao jambo mbona hakuna tatizo hapo
   
 4. HorsePower

  HorsePower JF-Expert Member

  #4
  Nov 7, 2011
  Joined: Aug 22, 2008
  Messages: 3,617
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 145
  Mkuu kutenda kosa si kosa, kosa ni kurudia kosa. We ushafanya kosa umaelimishwa kuwa ni kosa, halafu still unang'ang'ania kuendelea na kosa? Sidhani kama upo right! Shangazi ni mzazi tu kama alivyo baba mdogo/mkubwa, mjomba nk.

  Kuwa mwangalifu bwana!
   
 5. Kipilipili

  Kipilipili JF-Expert Member

  #5
  Nov 7, 2011
  Joined: May 25, 2010
  Messages: 2,207
  Likes Received: 482
  Trophy Points: 180
  Achana naye wangu laana iyoo!ohooo
   
 6. Pasco_jr_ngumi

  Pasco_jr_ngumi JF-Expert Member

  #6
  Nov 7, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 1,811
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 145
  hadithi za uongo za SHIGONGO zimehamia JF?????""""""""""""""""...................LOOOOOH
   
 7. Masikini_Jeuri

  Masikini_Jeuri JF-Expert Member

  #7
  Nov 7, 2011
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 6,809
  Likes Received: 364
  Trophy Points: 180
  Haingii akilini! Whatever happened to courtship?
   
 8. M

  Malova JF-Expert Member

  #8
  Nov 7, 2011
  Joined: Apr 21, 2011
  Messages: 777
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 45
  hata utotoni au baada ya kubarehe tulikuwa tanakulana mzigo(piga mahaba) watu ambao ni ndugu. kaka ukiweza achana nae
   
 9. Eiyer

  Eiyer JF-Expert Member

  #9
  Nov 7, 2011
  Joined: Apr 17, 2011
  Messages: 28,238
  Likes Received: 3,676
  Trophy Points: 280
  Sijajua kama unataka ushauri au unatupa taarifa,any waya sijajua imani yako,kama kwa mujibu wa imani yako hilo linaruhusiwa go on!
   
 10. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #10
  Nov 7, 2011
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,876
  Likes Received: 6,230
  Trophy Points: 280
  je shangazi yako huwapigia tena kuwajulia hali na kuwa-text kuwauliza kama wameoa wanaume wote wanaopiga simu kwa bahati mbaya kwake?
   
 11. kajwa

  kajwa Member

  #11
  Nov 7, 2011
  Joined: Oct 26, 2011
  Messages: 48
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  kwamara ya kwanza kusikia hii, lakini mimi nakushahuri wewe na huyo mkeshangazi mjipange mkawaombe msamaha ndugu zenu. na pia muwe na tabia ya kuwatembelea ndugu zenu ili jambo hili lisijitokeze tena,ni hayo tu.
   
 12. Yericko Nyerere

  Yericko Nyerere Verified User

  #12
  Nov 7, 2011
  Joined: Dec 22, 2010
  Messages: 16,250
  Likes Received: 3,863
  Trophy Points: 280
  kula raha kijana ndugu achana nao
   
 13. MAMMAMIA

  MAMMAMIA JF-Expert Member

  #13
  Nov 7, 2011
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 3,822
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 0
  Shangazi, ninavyofahamu mimi ni dada mkubwa au mdogo wa baba yako. Kama ni hivyo, WACHANA NAYE. Lakini mara nyengine anaweza kuwa shangazi kwa sababu ya extension tu ya ukoo: "Dada yake mkwe wake baba wa kaka yake wa kambo kitukuu cha babu", ikiwa ni hivyo, ng'ang'ania hapo hapo.
   
 14. Jaluo_Nyeupe

  Jaluo_Nyeupe JF-Expert Member

  #14
  Nov 7, 2011
  Joined: Dec 21, 2010
  Messages: 2,269
  Likes Received: 413
  Trophy Points: 180
  hebu fafanua kidogo hii simulizi.....ni shangazi yako kivipi?
   
 15. TECHMAN

  TECHMAN JF-Expert Member

  #15
  Nov 7, 2011
  Joined: May 20, 2011
  Messages: 2,677
  Likes Received: 162
  Trophy Points: 160
  kama kuna kosa lolote la kibaologia, inaweza kuwa ni makosa, lakini kama ni swala la kibila au la kiimani hajafanya kosa, kabla hujafanya kosa angalia nafsi yako ina ku drive vipi. Katika hadithi za kale za biblia, inaonyesha kuwa ukitaka kuo unakwenda kuoa kutoka kwa ndugu za babako au mamako, ndio unaweza ukasema sababu ilikuwa idadi ya watu, no kulikuwa na sababu za kiimani zaidi kiutamaduni zaidi, lakini bado wapo ambao walikwenda oa mbali na ndugu zao.

  Katika maisha tukiangalia, Mila zetu zina sema nini, wengi tutakuwa washitakiwa wa mila hizo. tunapokubali changes katika mifumo ya kimaisha sio kila change itakuwa nzuri au kupendeza katika kila jamii na tamaduni na desturi zake.
   
 16. bombu

  bombu JF-Expert Member

  #16
  Nov 7, 2011
  Joined: Jun 8, 2011
  Messages: 1,134
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 145
  Jamani keshawaambia Source: Shigongo sasa mbona mwamswalisha mwenzenyu hivyooo?
   
 17. v

  valid statement JF-Expert Member

  #17
  Nov 7, 2011
  Joined: Sep 18, 2011
  Messages: 2,737
  Likes Received: 177
  Trophy Points: 160
  Mwaka mnachati usijue jina lake la pili?
  Huyo jamaa alikuwa mbwiga mbwiga aisee.
   
Loading...