Sms vehicle tracking system available in tanzania-chunga gari lako

Sms vehicle tracking system available in tanzania-chunga gari lako

Gharama za SMS ni kama ukituma sms kawaida na sasa kampuni nyingi za TZ zina promosheni kupata sms 100 or 200 za bure kwa siku so ukiwa kwenye hizo Promosheni utapata ujumbe sms bureee kabisa.
 
Gharama za SMS ni kama ukituma sms kawaida na sasa kampuni nyingi za TZ zina promosheni kupata sms 100 or 200 za bure kwa siku so ukiwa kwenye hizo Promosheni utapata ujumbe sms bureee kabisa.
Mkuu andrew gharama za kufunga hi system ni the same kwa kila gari?I mean umesema $600 kwa GX100 vipi kama mimi namiliki prado?
Na ingependeza kama utaweka na contacts nur zako hapa pls.
 
Kwa magari madogo(saloon na Station wagon/van/hiace bei ni FIXED 600 USD....Malori/Mabasi bei itaongezeka kidogo kutokana vifaa kutumika zaidi. Iwapo mteja atakuwa na magari/wateja zaidi ya 3 (kwa mkupuo)tunafanya discount tutamfungia DEVICE kwa 550 USD. punguzo la 50USD... Kwa maelezo zaidi wasiliana nami Andrea Kalima email:andreakalima@gmail.com AU Meneja Masoko Msaidizi simonipetro@gmail.com simu 0769 096861 zaidi ya hizo FEATURES nilizozieleza hapo juu pia kuna PUNIC BUTTON in case umekuwa attacked/hijacked ukishabonyeza hiyo PUNIC BUTTON inatuma texts kwa namba 3 ambazo utakuwa umesave ikiwapa taarifa kuwa umepata tatizo (sehemu ulipo, Uelekeo,Landmarks za karibu na hapo ulipo........Tunakuhakikishia Ubora wa Kifaa hicho.
 
hatari mwanawane,,Kilichobaki mtengeneze na vya binadamu nimfunge wife, coz sina imani kabisa na nyendo zake
 
agrrrrrr........
asije tu akaipata mzee hii huduma manake ntakwama
 
vipi kama mimi nahitaji kufunga ndani kwangu na mawasiliano yaende kwenye kampuni ya ulinzi mfano hiyo punic button, pia vipi kufunga kwenye ofisi za kampuni yangu ili niwe nasikiliza yanayojili ofisini pindi ninapokuwa mbali na ofisi gharama zake zikoje, au hili mmeliweka vipi. maana kwenye ghari tayari nin mfumo makini kwa kutumia afrikan blakmagic.
 
Mkuu hii nimeipenda wherever ya ni brand ya kichina au ya nchi yoyote ile, utawezaje kunifungia mimi nipo Kahama, Shinyanga bila ya kuja Dar?
 
Mjamaica!
Kama upo mbali na Dar (kwa wewe Kahama, Shinyanga) tutaongeza fedha ya nauli na pesa ya kujikimu kwa fundi tutakaye mtuma kwako (maana kama kampuni tunapaswa kumlipa stahili zake Nauli, Allowances fundi tukimtuma sehemu ya kusafiri, eg Dar-Kahama..kwa maelezo zaidi wasiliana nami meneja masoko andreakalima@gmail.com AU Meneja Msaidizi simonipetro@gmail.com. Karibu
 
Eneo letu halijapimwa, ukifika sehemu ambapo hakuna details za eneo hiyo system haitafanya kazi.

Ni eneo gani basi hapa Dar au na sehemu nyingine hapa nchini ambapo inaweza kufanya kazi, yaani details zote za eneo zipo?
 
andreakalima naomba namba yako ya simu tuwasiliane nahitaji hiyo tracking device maana nimenunua COASTER sasa dereva anazingua sana anadai hamna biashara lakini kilomita zinasogea. hii DEVICE itanisaidia kujua movement zake
 
hatari mwanawane,,Kilichobaki mtengeneze na vya binadamu nimfunge wife, coz sina imani kabisa na nyendo zake
mbona rahisi kwa phone yake tuu inawezekana
sio wote ni wajuz wa tech
 
Mkuu nimekutumia email ichek nahitaji kuweka kwenye gari yangu.
 
Wadau kuna hii SMS Vehicle Tracking System ambayo ni device inawekwa kwenye gari yako then inaunganishwa na simu yako so unaweza ku-itrack gari yako popote pale wewe ulipo duniani au gari yako inapokwenda popote duniani,ili mradi unatumia simu yako iliyounganishwa na device kwenye gari yako.
FAIDA:
1. Unalipia Mara 1 tu (Hakuna Malipo ya kila Mwezi)
2. Unaweza ku-monitor movement ya gari yako popote kupitia ujumbe wa simu (sms)
a. Kujua lilipo(location) endapo si wewe unaendesha, kama umemuazima mtu au limeibiwa, inakupa na landmarks mfano, Andrea T 502 CAB:Stopped, 1.45 km W of Tegeta Mwisho Bus Station,Dar es Salaam,TZ,7.86787,56.21156,10:32 Jun 13
b. Kusikiliza sauti ya anayeendesha maana linakuwa limetegwa Speaker ndani ya gari
c. Ku-STOP ENGINE popote pale
d. Inakupa Summary Report ya Movement ya Gari kwa siku nzima, kilomita ilizo tembea,
e. Unaweza kujua maeneo ya karibu ambapo gari yako imepaki/ilipo
WALENGWA: Makampuni ya Usafiri(Car Rental, Mabasi,Malori)& Wamiliki wa Magari Binafsi
Kwa maelezo zaidi tunaweza kuwasiliana kwenye andreakalima@gmail.com
Mpaka leo ipo
 
Unalipia 600 USD (unalipia once) kwa miaka yote ikitokea unataka kuuza gari yako tunaweza kukutolea hiyo device na kui-install kwenye gari mpya utakayonunua. Tafadhali hupaswi kubainisha kwa watu usiowaamini kuhusu kufungwa kwa kifaa hiki ndani ya gari yako. Ukifika ofisini kwetu,tunafunga na tunakufundisha jinsi ya kutumia hiki kifaa. ukituhitaji tunakuja popote Tanzania hata nchi jirani Kenya, Uganda, Congo DRC, Burundi, Rwanda.
Mr ,$600 is too much [emoji33] [emoji33]
 
BEI IMEPUNGUA: bei Ni 150 USD Kwa saloon/SUV. Karibuni
 
Ukisikia wizi ndio huu
Kifaa chenyewe chauzwa Dollar 85
Line ya simu 1000
Installation 50,000
Kwanini Watanzania wakijua kitu wanapenda sana ibia wengine kisa hawajui?
Yaani vifaa wananunua Alibaba afu wanakuja zingua hapa
 
Ukisikia wizi ndio huu
Kifaa chenyewe chauzwa Dollar 85
Line ya simu 1000
Installation 50,000
Kwanini Watanzania wakijua kitu wanapenda sana ibia wengine kisa hawajui?
Yaani vifaa wananunua Alibaba afu wanakuja zingua hapa
Hii ni biashara ndugu. Aliye tayari kwa bei yangu ya 150 USD anakaribishwa ambae ana hiyo 85 USD akuone umfungie. Asante
 
Back
Top Bottom