Sms kutoka kwa JMKikwete

Sms kutoka kwa JMKikwete

kwa kweli hata mimi na familia yangu hatuku hesabiwa kwa iyo waongeze watu wanane kwenye hiyo hesabu
 
Mimi na famili yangu nadhani tunashida. Hii ni sensa ya pili nikiwa naishi maeneo tofauti wamekuwa wakiishia nyumba moja kabla ya kufika kwangu, huwa nawaona hao lakini nyumba yangu hawafiki, kwahiyo kwenye hesabu hiyo ongeza watu wanne wa wafamilia yangu.
Wanalipua lipua tu,hawako makini na kitu chochote.
 
3% ya watanzania wanaishi Zanzibar, na 97% wanaishi Tanganyika. Nafikiri hili ni jambo la kuzingatiwa sana katika mgawanyo wa Rasilimali pamoja na kutenga budget ya Serekali.

huko zenji jamani ni pasua kichwa, watakujibu kuwa hiyo ni nchi kamili hivyo kila kitu pasu. huoni wamekomaa mpaka wakabalance kamati ya maoni ya mabadiliko ya katiba! kulikuwa na haja gani ya upasu! bora ni nchi, angekuwa ni mtoto wako akuendeshe hivyo, sijui hata unamfanyaje
 
Hata kwenye Bunge la Muungano wabunge wa Zanzibar wawe 3% ambao sio zaidi ya 10 ndio hapo ngoma itakuwa draw


hapa inaonekana tunatumikia watu kwa kodi zetu bure maana kwa zanibari walitakiwa hata wabunge 7 au 8 tu sasa tuna rais mawaziri,naibu mawaziri wakuu wa mikoa na wengine, ndiyo maana nasema huu muungano hausaidii chochote bara
 
Mtoto umleavyo ndivyo akuavyo,wamelelewa kwa kudekezwa hao wa Zanzbar,wakilia kidogo tu Watanganyika(viongozi) wanawabembeleza.Hivi kati ya Tanganyika na Zanzbar nani anafaidi ndoa hii?(muungano huu).Unawake wa2 mke mkubwa anawatoto 6,wapili anawatoto2 ukiwapa hela inayolingana yupi hujamtendea haki?
 
Hapa kwenye 97% kwa 3% ndo pana utata.... Muungano unaoshikiliwa kwa uzi
 
Hivi Marekani nao wana sensa? Na majibu hutolewa na Obama kwa sms?
samahani lakini, nauliza tu, maana hamchelewi kunipiga Ban
 
Ask first the salary of Dr slaa for sure you are going to faint(zimia)

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
kwa kweli hata mimi na familia yangu hatuku hesabiwa kwa iyo waongeze watu wanane kwenye hiyo hesabu

Mi pia waniongeze kwenye hiyo idadi.. Mi bechula.. ila nilikuta tiki mlangoni,wakati sikuhesabiwa..
Na rafiki yangu mmoja alikuwa akitembeza hayo madodoso ya kuhesabu watu.. ye mwenyewe hakuhesabiwa!
 
hapa inaonekana tunatumikia watu kwa kodi zetu bure maana kwa zanibari walitakiwa hata wabunge 7 au 8 tu sasa tuna rais mawaziri,naibu mawaziri wakuu wa mikoa na wengine, ndiyo maana nasema huu muungano hausaidii chochote bara

Muungano ulioshauriwa na Mh Lissu ndiyo sahihi..
 
wengi wamepata hata mimi nimepata labda cm za kichina sm hazingii
 
Back
Top Bottom