Sliders watu wenye nguvu ya ajabu ya ku-control/kuingiliana na umeme

Mkuu mimi nakumbuka enzi tupo shule ya msingi kuna nyumba ya mzee mmoja hivi alikuwa na bomba ile ya kubebea dishi za ving'amuzi yale maungo makubwa ya zamani.

Sasa lile bomba lilikuwa ni la chuma kila tunavyoludi shule lazima tulichezee sasa maajabu yalikuwa wengine wakishika amna kitu ila mimi nikishika napigwa na shoti ya umeme kila nikiwaeleza wenzangu kuwa iyo bomba mimi nikishika inanipiga shoti awaelewi maana wao wanashika vizuri tu.

Mpaka leo sijawaielewa kwanini ilikuwa inatokea vile.
Duuuuh mkuu hii ni nyingine ya aina yake
Vipi ni bomba lile lile tu lilikuwa linakupata matokeo uliyoyazungumza

Au ushawahi kukumbana na hali kama hiyi tofauti na mazingira hayo.
Labda ukashika kitu kingine kikakuletea athari kama hiyi???
 
Nimewahi kufanya kazi na kijana mmoja ambaye kila anapopita kwenye scanner anasikia kimlio kama kengele kwenye sikio lake... akaomba ruhusa asiwe ana pita direct kwenye scanner...... Nilikuwa najiuliza hii ni nini,sijawahi elewa... labda wajuzi watasema jambo
Hata Dr Evans anasema kuna mengi hayagundulik zaidi kuhusu phenomen iliyozungumzia hapo zaidi
Watafiti wa mambo ya panaroma kil sku wanatuletea aina tofauti tofauti za hali kama hizi

Huend hii pia ipo na katika hizi phenomen na si mtu mmoja anekumbana nayo pengine ni mamia ya watu.
Uzuru wa sayansi italeta tu majibu. Kadri inavyopanukaa
 
Wakati nipo mdogo kipindi icho nina miaka kama 9 nilikataga waya ya redio afu nikachomeka kwenye umeme mawazo yangu nikilamba labda ntaona ladha ya chaji kilichotokea ni siri yangu!
😅😅😅😅😅😅 nlitaka kukuuliza hukufa mkuu ..nikakumbuka kumbe umecomment so sure uko hai
Pole sana mkuu😅😅😅
 
Nimepigwa sana shot na umeme kipindi nipo mdogo nilikua mtundu ila mara nyingi nilikua narushwa wenzangu ndio walikua wanadhurika sana nahisi pengine ni bahati tu. nakumbuka kuna jamaa yangu alikaukia kwenye transfoma mabatini
 
Duuuuh mkuu hii ni nyingine ya aina yake
Vipi ni bomba lile lile tu lilikuwa linakupata matokeo uliyoyazungumza

Au ushawahi kukumbana na hali kama hiyi tofauti na mazingira hayo.
Labda ukashika kitu kingine kikakuletea athari kama hiyi???
Ni bomba lile lile tu lenye wenzangu walikuwa wanashika ndo ilikuwa inatokea.
 
II

KISA CHA PILI

BCEC40AB-AF31-4EF0-A47F-651543A2A57B.jpeg

Mwamba mwingine ni Jones anasema yeye alianza kuona hali hii ya Ajabu alipokuwa ana miaka 10 tu pale wazazi wake walipomuacha nyumbani peke yake alipoanza kulia mara mfumo umeme ndani kwao ukaanza , kufanya kazi kwa nguvu TV ,zilizimika ghafla na shoti kutoka kwenye baaadhi ya viunganisho vya umeme

Anasema alipata kugombana na rafiki yake shuleni kipindi cha miaka 17, mara taa zikaangaza kwa mwanga mkali zaidi ya kawaida na hali hiyo imejitokeza mara kwa mara anapopata hasira

KISA CHA TATU

9291C7A3-457D-43AC-B169-E9386ACDAFA3.jpeg

Saa zinazotumia mfumo wa betri au kielektoniki pia huwa zinaathiriwa wa mara kwa mara na watu hawa, na hulka hiyo inaweza kuwa katika familia yoyote .

Huyu kijana mwingine aliyeitwa Murph anasema ana tatizo na saa na vifaa vya elektronic

Murph anasema. Dada yake alikuwa na hali sawa kama ya kwake anasema dada yake Alipoaga dunia, alimkuta ana boksi la saa zaidi 30 chumbani mwake ambazo zilikuwa hazifanyi kazi zingali bado mpya . Anasema Akaelewa mara moja hali hiyo maana hata yeye ni muanga mmoja wapo.

KISA CHA NNE

7886FB17-F37C-4B2C-A8A7-8B5C2E1863AB.jpeg

Tybald yeye ni mmoja wa waanga wa dhana hii anasema hali hiyo imeathiri karibu familia yao nzima , kwa upande wa wanawake hasa hasa Mama yake hakuna hata mmoja anayeweza kuvaa saa , uwezo wao wa kuathiri vifaa vya umeme umewapata karibu wote asema. “Hakuna Hata mmoja katika wanawake anayeweza kuvaa saa basi zote huaribika anasema hata yeye kuna muda akikaribiana na vifaa baadhi kama taa basi huzima au kufifia mwanga waka.

HALI HII HUTOKEA ZAIDI MUDA GANI??

(MSONGO NA HISIA)

6B0F7B6C-5D7F-490E-857E-6A86E0DC35D5.png

Mara nyingi, watu hawa wamegundua kwamba inaonekana kuna uhusiano kati ya matukio haya na jinsi wanavyohisi.

Wanapokuwa na stress au hasira, au furaha isiyo kifani hisia zao huonekana kuingiliana na vifaa vya elektroniki vilivyo karibu nao.

Wengi hawaitamani hali hiyo wengine walitamani pengine kungekuwa na vidonge vya kuondoa nguvu hizo za Ajabu

Kisayansi bado haijajulikana nini tatizo haswa na sababu kuu ya nguvu hizo.,

Labda majibu yapo spiritual zaidi.

SHUKRAANI

DA VINCI XV
 
mkuu hii mada imenigusa
na kunichanganya pia
maana hiki kitu unachokizungumzia kimenitokea juzi
hapa mji wa kiselikali dodoma.
nilikuwa nmepanda pikpki
mimi na mwenzangu
tulipofika kwenye mataa kila tukifika kwenye taa mwanga unaongezeka panakua peupe sana,
ukivuka mwanga unapungua
hii hali ilitushangaza hadi mwenzangu aliniuliza kwamba
kwanini tukifika kwenye taa mwanga unaongezeka?
mimi nikamjibu kwamba
labda inawezekana hizi taa
wamezifunga maalumu
kwa mwanga wa wastan
ili zisitumie umeme mwingi
lakin mtu akipita zinatoa mwanga ili mtu aone vzur
kisha zinarud kwenye hali ya kawaida
ili zisitumie umeme mwingi.
Hizo taa zimesetiwa hivyo mkuu, zipo pia Morogoro municipal, awali na mimi zilinichanganya lakini baada ya kuzifuatilia nikagundua zipo hivyo..ukiikaribia inajiongeza mwanga ukivuka zinapungua..
 
Hizo taa zimesetiwa hivyo mkuu, zipo pia Morogoro municipal, awali na mimi zilinichanganya lakini baada ya kuzifuatilia nikagundua zipo hivyo..ukiikaribia inajiongeza mwanga ukivuka zinapungua..
Ooohoo😅
 
Siku moja nilitokewa na tukio ambalo mpaka leo sijawai elewa, nilikuwa na marafiki usiku tunakunywa na kucheza pooltable. Kwenye kona za pooltable palikuwa na vibati flan hivi ambapo niliweka glass ya mvinyo na palikuwa na kiwekeo cha sigara. Wakati nataka kuchukua glass niligusa kile kibati ambapo nilipigwa shot ya ajabu ambayo ilitoa mshindo mkubwa, taa iliokuwa inatumulikia ilipasuka.

Tukio lile kila mtu aliekuwepo lilimshangaza na mpaka leo sijawai lielewa'
 
Duuuuh , so haijawahi kukutokea tena katika mazingira mengine??
 
Sayansi inavitu vingi naamini Africa kuna mambo mengi kama haya Ila Majasusi wa NJE wamefanikiwa KUYAZIBA kwa mgongo wa IMANI
 
Mkuu mimi nakumbuka enzi tupo shule ya msingi kuna nyumba ya mzee mmoja hivi alikuwa na bomba ile ya kubebea dishi za ving'amuzi yale maungo makubwa ya zamani.

Sasa lile bomba lilikuwa ni la chuma kila tunavyoludi shule lazima tulichezee sasa maajabu yalikuwa wengine wakishika amna kitu ila mimi nikishika napigwa na shoti ya umeme kila nikiwaeleza wenzangu kuwa iyo bomba mimi nikishika inanipiga shoti awaelewi maana wao wanashika vizuri tu.

Mpaka leo sijawaielewa kwanini ilikuwa inatokea vile.
Kuna watu wako sensitive na umeme kuliko wengine. Kuna watu wanaumwa sana kichwa pasipo kujua wako sensitive na Wi-Fi
 
Mkuu mimi nakumbuka enzi tupo shule ya msingi kuna nyumba ya mzee mmoja hivi alikuwa na bomba ile ya kubebea dishi za ving'amuzi yale maungo makubwa ya zamani.

Sasa lile bomba lilikuwa ni la chuma kila tunavyoludi shule lazima tulichezee sasa maajabu yalikuwa wengine wakishika amna kitu ila mimi nikishika napigwa na shoti ya umeme kila nikiwaeleza wenzangu kuwa iyo bomba mimi nikishika inanipiga shoti awaelewi maana wao wanashika vizuri tu.

Mpaka leo sijawaielewa kwanini ilikuwa inatokea vile.

Mie milango ya aluminium inanitesa mno!! Nikiugusa kwa mara ya kwanza napigwa shoti kali sana. Baada ya hapo nikiugusa tena sipigwi, nikienda mlango mwingine hali ni hiyo hiyo.

Hali hii ni toka naijua aluminium mpaka sasa. Napata tabu sana na aluminium zenu maofisini
 
Back
Top Bottom