Sliders watu wenye nguvu ya ajabu ya ku-control/kuingiliana na umeme

Da Vinci XV

JF-Expert Member
Dec 7, 2019
3,403
5,369
SLIders WATU WENYE NGUVU YA AJABU YA KU-CONTROL/KUINGILIANA NA UMEME ... JE WEWE NI MMOJA WAO.?

Wasalaam

9A2EF1B2-8817-4704-88C9-4F5A2E6AF10C.png


Kwa mara ya kwanza wakati nipo vidudu nikizitazama movie za wataalamu wa kutengeneza movies dunia hii, Marvel na movie yao ya Spider Man , nami nikajitamani nafsini mwangu pengine ningeng'atwa na Buibui ili niwe na uwezo kama wa kijana Peter Parker.

Ningeweza kupaa na kuruka kwa utando kama kijana yule wakati mwingine nikikumbuka huwa najicheka mwenyewe magorofa gani pale mwanakwerekwe zanzibar yangeniwezesha kudanda na kuhama kutoka ghorofa moja kwenda jengine.

Usingenilaumu ni mjongeo na ashiki za utoto kutamani mengi yasiyowezekana, hii ni hulka ya watoto wengi huku wengine wasingeliacha kujipachika majina ya wakongwe maarufu wa movie wa nyakati zetu kina Ajay, shah rukhkhan , vandamme , Check norris , james bond na wengineo wengi

Waliotengeneza utoto wetu kuwa kitu cha kukumbukwa zaidi

Umaridadi na ufanisi wa kazi kutoka kwa watalaamu na waandaji hawa 'Marvel' ukaathiri ubongo wangu na kuwa shabiki yao mkubwa sana, mpaka kesho kutwa..

Lakini bahati nzuri wakati huu sikuwa mtu mwenye kutamani tena kuwa kama kina Hulk au Iron Man

Wakati ni ule akili yangu ilipofunguka zaidi na kujiuliza maswali ambayo pengine Mungu na Sayansi ndio pekee ambao wangediriki kunipa majibu ya kuridhisha na kushibisha ubongo wangu wenye kiu iliyotaradadi., nikitazamaa wataalamu wa Marvel kina Anthony Lusso mwenzake au kina Jon Watts katika kuongoza movie au subiri kidogo kuna mkono wa wataalamu Wa DC walipoandaa movie ya The flash jamaa anapita zaidi ya speed isiyo mfanowe wala kumithilika supercharged man, basi kuwahusu hawa superhuman na superheros kuna kitu kiliongeza tafakuri katika ubongo wangu wa mbele.

Inshaallah kwa mapenzi yake mwenyezimungu nitaleta makala mbeleni kuhusu superheros,superhuman na uhalisia katika maisha na fumbo la wazungu kwetu.

E271AD78-1E12-4497-B305-50D0EF6C4CDD.jpeg


SLIders NI NANI??

SLIders & the Streetlight phenomenon vipi kuhusu hii??

Hawa wao kuathiri taa za umeme, za barabarani , taa za mgari na vifaa vingine vya kielektroniki.

SLI inatokana na neno STREET LIGHT INTERFERENCE hawa watu wameonekana kuwa na uwezo usio wa kawaida wa kuingiliana na mwanga wa barabarani, moja ya matokeo ya hali hii ni ya taa za barabarani kuangaza zaidi au kuwa na mwanga mkali mithili ya mtu aliyekaa kizani na ghafla akamulikwa machoni au zaidi au pia mwinga kuzima ghafla wakati watu hawa wanapozikaribia watu hao huitwa SLIder.

Ni dhana ya kawaida tu kwamba karibu kila mtu anayeanza kusoma au anayenza kung'amua kuhusu dhana hii angalau ataanza kuvuta taswira ya mtu mmoja ambaye ni SLIder ambaye anamjua au labda hata anaweza kuwa slider yeye wenyewe.

Watu hawa wanatambulika kwa namna mbalimbali pasi na ubaguzi ni wanaume kwa wanawake, vijana kwa wazee, mashoga na wasio mashoga, weusi kwa weupe na wanaishi katika maeneo yote mijini na vijijini.
Wanaweza kuwa madaktari, wanasayansi, waandishi wa habari, mechanics au kazi nyingine yoyote unayoifahamu wewe.

4CB2C5BA-2D57-4BF9-A71C-C9825BF4CDCD.jpeg


Uwezo huu unaonekana kuwa wa namna tofauti tofauti kabisa baadhi ya watu wamepata uwezo mkubwa sana , wengine wanao uwezo mdogo na mwingine anaweza kuwa na uwezo wa kati na kati , lakini bahati mbaya imeonekan anayehusika na uwezo huo huwa hana udhibiti wa dhahiri juu yake.
Pia inaonekana kuwa ni random bila mpangilio wowote wa sababu na athari.

Wakati mwingine slider ataonesha effect mbele ya vyanzo hivi vya umeme au Mwanga mara kadhaa katika wiki , au mara moja kwa mwezi.
Au nyakati nyingine inaweza kutokea kwa muda mrefu hata mwaka mara moja.


2BEA9F08-F535-452E-A028-164BF21B5F2D.jpeg


Taa za barabarani huzimika pindi wanapozikaribia muda mwingine wenye nguvu zaidi taa na nyaya zenye kusafirisha umeme hukatika na kuanguka wanapokuwa na hasira sana.

Pia kuna wengine saa ,au mapambo mengine yaliyo katika mfumo wa umeme hushindwa kabisa kufanya kazi kila wakati wanapozitumia.


Nini kipo ndani ya watu hawa???


SABABU ZA UWEZO WA SLIders


Sababu ya nguvu hizo kikawaida na kisayansi haijajulikana labda kiroho zaidi
Na kwa hakika kuna sababu za kawaida za taa za barabarani au vifaa vya umeme kufanya kazi kimakosa, hata kuzima mara kwa mara usiku, kutokana na taa au kifaa kuchakaa, ubovu, au kuharibiwa
Lakini.

Watu wengi, wanaripoti kwamba wanaonekana kuwa na athari sio tu kwenye taa za barabarani lakini kwa vifaa vya elektroniki vya kila aina.

Pasi na kujua sababu ya uwezo wa nguvu hizo mfano muhusika,akiwa na hasira au furaha sana Athari za nguvu hizo huweza kujitokeza

C7810E83-0F9F-4040-8EB0-DF7745A769AD.jpegUTAFITI WA DR.EVANS


Mwaka 1993 mwanasayansi wa Marekani, Dr Hilary Evans, alichapisha ripoti ya kina zaidi juu ya hawa SLI,Ripoti ambayo Dk Evans alijumuisha kwa kushirikiana na chama cha uchunguzi wa kisayansi wa matukio ya kutisha.
Aliripoti uzoefu wa SLI Katika ripoti yake, Dk Evans alisema kwamba, uwezo huu wa SLIders unapaswa kuchukuliwa kama jambo ambalo ni la kweli na lililopo, pia alisema kuwa uchunguzi na Elimu zaidi inahitajika kujifunza zaidi kuhusu hilo.
Dr Evans aliambatanisha na Baadhi ya visa na Maelezo ya SLIders na Hali hii inavyowatokea.

Watu wengi katika utafiti wa Dr Evans pia waliripoti kwamba wamekuwa wakijiuliza sana juu hali zao na namna zilivyowatokea na walipata kusema kwamba kama wangeliuliza kwa watu wengine ili kupata majibu kutoka kwa watu wengine basi yalikuwa majibu ya kudharauliwa.

Dk Evans aliweka hitimisho lake kwamba inaonyesha kwamba SLI ilikuwa kwa hali fulani ya kushikamana na msukumo wa umeme unaozalishwa na ubongo


60168627-9D89-4BB8-8A32-55A11BD1AA5A.jpeg


BAADHI YA VISA VYA SLIders.


Watu wengi ambao wameripoti kasumba hii wamepata kueleza kuwa mashine za kielektroniki huzima au kuanza kufanya kazi kwa kasi zaidi pindi wanapokuwa karibu nazo

KISA CHA KWANZA


30B8A9EE-C204-45A7-936D-784FACDD8A53.jpeg
Sarah bidada mmoja aitwaye sarah huko nchini marekani anasema Alipata kusogea karibu mashine zilianza kufanya kazi kwa kasi isyo ya kawaida kupokea umeme ulio mkubwa kukiko kawaida na kupasuka hali hiyo ilijitokeza zaidi ya mara sita tofauti lakini bado hakung'amua

Ajabu,

Sarah anasema alipata kujifahamu baada ya kwenda kwenye jumba la makumbusho la sayansi na alibaini kuwa ana athari na hali hiyo isiyo ya kawaida kwenye majaribio ya umeme.

KISA CHA PILI

ITANDELEA....

JE WEWE NI MMOJA SLIders??

DaVinci XV.


E2D6E277-2A41-4637-9366-8155629B47D4.jpeg
 

Super Handsome

JF-Expert Member
Jul 16, 2013
3,854
6,401
Kuna Mzee fulani kwa sasa ni mstaafu wa JWTZ yeye alikua kila akikatisha Pori la Makaburi ya Jeshi ili kuja uswahilini mitaa ya Kawe usiku mnene alikua akimulikiwa taa inayotoka angani na inapiga usawa wake tu pale anapo kanyaga..na akikaribia kumaliza kuvuka kichaka hali inatoweka!
 

Da Vinci XV

JF-Expert Member
Dec 7, 2019
3,403
5,369
Kuna Mzee fulani kwa sasa ni mstaafu wa JWTZ yeye alikua kila akikatisha Pori la Makaburi ya Jeshi ili kuja uswahilini mitaa ya Kawe usiku mnene alikua akimulikiwa taa inayotoka angani na inapiga usawa wake tu pale anapo kanyaga..na akikaribia kumaliza kuvuka kichaka hali inatoweka!
Huyu naye tumuweke kundi la SLIders au???
😅😅
 

low thinking capacity

JF-Expert Member
Jun 4, 2018
1,239
1,336
Kuna Mzee fulani kwa sasa ni mstaafu wa JWTZ yeye alikua kila akikatisha Pori la Makaburi ya Jeshi ili kuja uswahilini mitaa ya Kawe usiku mnene alikua akimulikiwa taa inayotoka angani na inapiga usawa wake tu pale anapo kanyaga..na akikaribia kumaliza kuvuka kichaka hali inatoweka!
Anaitwa mzee nani
 

Mgmi

Member
Jul 25, 2021
59
125
Huyu naye tumuweke kundi la SLIders au???
😅😅
mkuu hii mada imenigusa
na kunichanganya pia
maana hiki kitu unachokizungumzia kimenitokea juzi
hapa mji wa kiselikali dodoma.
nilikuwa nmepanda pikpki
mimi na mwenzangu
tulipofika kwenye mataa kila tukifika kwenye taa mwanga unaongezeka panakua peupe sana,
ukivuka mwanga unapungua
hii hali ilitushangaza hadi mwenzangu aliniuliza kwamba
kwanini tukifika kwenye taa mwanga unaongezeka?
mimi nikamjibu kwamba
labda inawezekana hizi taa
wamezifunga maalumu
kwa mwanga wa wastan
ili zisitumie umeme mwingi
lakin mtu akipita zinatoa mwanga ili mtu aone vzur
kisha zinarud kwenye hali ya kawaida
ili zisitumie umeme mwingi.
 
7 Reactions
Reply
Top Bottom