"Slang" sio kile wanachofikiri

Nimecheka sana kwa uzi huu. Kipindi nipo form 5 tulikuwa kwenye paper, sasa kukawa na swali la kuelezea maana ya Slang, jamaa mmoja acha adundike anavyojua yeye akatoa na mifano anasema, instead of saying "whatsap a person can say Wharrap"
ulikuwa unachungulia mtihani wa mwenzio
 
Nakitoa …………. naondoka zangu
Nitakufua ………nitakupiga
Manzi …………… msichana
Mshikaji ……….. mpenzi wa jinsi tofauti (siku hizi ni rafiki tu wa kawaida)
Bonga ………….. tongoza (siku hizi ‘zungumza’)
Dingi ……………. baba
Charara ………... ishiwa fedha
Mambo du kinaa .. mambo safi/poa :D:D:D

……………….
Duh! Vijana wa sasa hawawezi kukuelewa kabisa kwa maneno haya, maana yametumika miaka ya sabini na themanini...
 
Kwa kifupi slang ni misimu watu wengi wakimaskia MTU ameongea ligha hasa kiingereza kwa lafudhi flan yenye radha husema jamaa anapiga slang lakin kumbe slang haiko katika lafudhi (accent) Bali ni kimisamiati zaidi
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom