"Slang" sio kile wanachofikiri

Translator

JF-Expert Member
May 19, 2017
286
297
Mara nyingi mtaani utasikia watu wakisema, “Jamaa anapiga slang si mchezo.”

Wengi hudhani “slang” ni Kiingereza cha Kimarekani.


Lakini maana halisi ya “slang” ni lugha ya mtaani. Ni ile lugha ambayo utajisikia aibu kuitumia mbele ya watu unaowaheshimu. Na mara nyingi huwa ni maneno yanayokaa kwa muda kisha yanapotea.


Hivyo, kila lugha ina slang – iwe Kiingereze, Kiswahili, au lugha za makabila yetu.


Je, ulikuwapo wakati slang hizi za Kiswahili zikiwa kwenye chati? :D:D


Nakitoa …………. naondoka zangu
Nitakufua ………nitakupiga
Manzi …………… msichana
Mshikaji ……….. mpenzi wa jinsi tofauti (siku hizi ni rafiki tu wa kawaida)
Bonga ………….. tongoza (siku hizi ‘zungumza’)
Dingi ……………. baba
Charara ………... ishiwa fedha
Mambo du kina .. mambo safi/poa :D:D:D

……………….

Hebu ongeza na mengine.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom