Elungata, wewe ni mtanzania? Na kama ni mbongo jee unaijua katiba ya nchi hii? Ibara ya 41.-(7) inasema hivi:-Iwapo mgombea ametangazwa na Tume ya Uchaguzi kwamba amechaguliwa kuwa Rais kwa mujibu wa ibara hii, basi hakuna mahakama yoyote itakayokuwa na mamlaka ya kuchunguza kuchaguliwa kwake. Sasa ulitegemea aende mahakama ya nchi gani? Yeye Dr. alitaka wao wakamshitaki na yeye katika kujitetea angepata mwanya wa kumwaga ushahidi wake ambapo ulimwengu wote ungejua kwani kesi ingekuwa inaripotiwa na vyombo vya habari.Kama una kumbuka kesi ya Mrema ya Milioni 900, kulikuwa na kanda ambayo upande wa mashitka ulikataa isichezwe mahakamani kwa kigezo kuwa sheria hairuhusu ushahidi wa aina hiyo ,lakini wakili wa Mrema akaomba ichezwe siyo kama ushahidi bali alitaka shahidi wa upande wa mashtka aliyekuwa anataka kum cross examin aisikilize kwani maswali yake yangetoka humo, Hakimu akakubali, na ni ndani ya kanda hiyo mchele ulimwagwa kwenye kuku wengi kwani vyomabo vya habari viliripoti ukweli amabao kwa hali ya kawaida usingejulikana kwa wengi, na ndiyo msingi wa serikali kuja kuifuta kesi hiyo baadae. Elungata upo mkuu?