Wana wa Nchi,
Natanguliza Shukrani kwa Mola wangu,
Watanzania wenzangu, kimsing ni miaka miwili tu imepita tangu tumalize uchaguzi mkuu wa mwaka 2010, na bado tuna miaka mitatu mbele kabla ya uchaguzi mwingine mwaka 2015, ingawa ni mapema sana kuanza kuzungumzia nani atakuwa rais au nani atagombea kwa chama gani lakini Watanzania wanayo haki ya kuanza kupima na kuchambua nani anaweza kuongoza taifa letu, hivyo ni rai yangu kwamba tukiwa tunafikiria nani atakuwa rais wa Tanzania pia tuwe tunafanya kazi ili kuweza kukuza kipato cha mtu mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla,
kimsingi Dr Slaa anaweza kugombea tena Urais kwa tiketi ya Chadema kwa kuwa hakuna kifungu chochote cha katiba ya chadema kinachomzuia kugombea Urasi kwa mara nyingine,,nimeisoma sana Katiba ya Chadema lakini sijapata kuona kifungu anacho kizungumzia ndugu Lukme, kwa maana hiyo napenda kuwatoa hofu Wanachadema na Watanzania kwamba hakuna kifungu chochote ambacho kinamzuia Dr Slaa kugombea tena Urais na pia ni haki yake ya Kikatiba. aidha kugombea au kutokugombea ni maamuzi binafsi ya mwanachama wa Chadema
Asanteni Wana Wa Nchi.
Kamanda Magoma Jr Magoma