Slaa: Ikulu imemdhalilisha Warioba

jme

JF-Expert Member
Aug 4, 2013
4,665
4,797
SIKU mbili baada ya Ikulu kutoa taarifa ya kejeli dhidi ya Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba, wanasiasa, wasomi, viongozi wa dini na wanaharakati wameitaka Ikulu ya Rais Jakaya Kikwete kumwomba radhi yeye pamoja na wajumbe wa tume yake.
Akizungumza na Tanzania Daima jana, Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa, alisema ukirejea kauli ya Rais Kikwete wakati akizindua Bunge la Katiba na kauli ya Ikulu juzi dhidi ya Warioba, utabaini kuwa kuna hila na chuki kubwa kati ya Ikulu, Warioba na tume yake.
Dk. Slaa alisema anaamini Jaji Warioba anasema ukweli kwani katika mazingira ya kawaida, isingewezekana baada ya kuwasilisha hotuba yake bungeni, usiku ule ule wakiwa mjini Dodoma, yeye na wajumbe wa tume yake wangekabidhi ofisi na kunyang'anywa magari.
"Nikirejea kauli ya Rais Kikwete bungeni ambapo jina la Jaji Warioba alilitaja zaidi ya mara sita, ukiunganisha na kauli ya Ikulu na msimamo wa CCM, utabaini kwamba kuna hasira kubwa dhidi ya Warioba kutokana na maoni aliyokusanya kutoka kwa wananchi. Rais na CCM wanaonyesha wazi kwamba hawaitaki katiba mpya," alisema Dk. Slaa.
Mhadhiri Mwandamizi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Dk. Benson Bana, alisema Ikulu ikubali kwamba ilitumia lugha ya kejeli na dharau kwa Jaji Warioba, hivyo iangalie namna ya kumuomba radhi.
"Kwa wananchi waliofuatilia majibishano ya Ikulu na Jaji Warioba, watakubaliana nami kwamba wamemdhalilisha mzee wetu Warioba, hivyo msemaji wake ni vyema akaangalia namna ya kuyamaliza kuliko kuendelea kulumbana hadharani," alisema Dk. Bana.
Alisema Ikulu ilipaswa itoe maelekezo ya makabidhiano kwa katibu mtendaji wa tume hiyo na siyo kuwadhalilisha wajumbe hao mjini Dodoma mara baada ya Mwenyekiti wao, Jaji Warioba kuwasilisha rasimu ya pili ya katiba mbele ya wajumbe wa Bunge hilo linaloendelea.
"Ikulu haikuwa na sababu ya kutoa kauli ya kashfa dhidi ya Jaji Warioba, hata kama alikosea. Wananchi wengi wanaofuatilia mchakato wa katiba, wanafahamu kazi yake nzuri akisaidiana na wajumbe wenzake. Kimsingi walistahili sifa na siyo kuwakejeli," alisema Dk. Bana.
Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dayosisi ya Karagwe, Dk. Benson Bagonza, alisema kitendo cha Ikulu kutoa taarifa yenye maneno ya kejeli kwa Jaji Warioba ni sawa na kumvua nguo za ndani hadharani.
"Nimejisikia vibaya niliposikia taarifa ya Ikulu, ni kama imemvua nguo za ndani hadharani… hakupaswa kufanyiwa hivyo. Ikulu ilipaswa kutumia burasa ya kufanya makabidhiano kutokana na kazi nzuri aliyoifanya kwa Watanzania," alisema Askofu Bagonza.
Askofu Bagonza alisema kama Ikulu ilivyomuamini, kumteua na kufanya hafla ya kumwapisha Warioba na wenzake 30, vivyo hivyo siku ya makabidhiano ya kuhitimisha kazi hiyo ingefanywa kulingana na umuhimu wa kazi yao.
"Hakuna jambo kubwa la historia linalomalizwa kwa kejeli ama malumbano, tumezoea kuona katika harusi na misiba baada ya kufanyika ama kumalizika, watu huvunja kamati zake kwa sherehe ndogo za kumalizia mabakia, ndivyo ambavyo tulitarajia Ikulu ifanye hivyo kwa Jaji Warioba. na kuongeza
"Nimesoma katika mitandao ya kijamii namna baadhi ya watu wakipinga hoja za Jaji Warioba kuhusu rasimu aliyoitoa, na hata malalamiko yake ya kutupiwa virago… hivi haiwezekani kupinga hoja zake bila ya kumtukana?" alihoji Askofu Bagonza.
Alisema Ikulu na Watanzania wanapaswa kufahamu kwamba hakuna mzalendo aliyebakia nchini zaidi ya Jaji Warioba, hata kama wapo wanaomkejeli.
"Sina shaka na uzalendo wa Jaji Warioba anaouonyesha katika nchi yake, tena ndiye mfano wa kuigwa kwa wote wanaotaka kuwa wazalendo," alisema Askofu Bagonza.
Katika hatua nyingine, Kaimu Mwenyekiti wa Jukwaa la Katiba (Jukata), Hebron Mwakagenda, alisema kinachofanyika sasa ni kuwatoa watu kwenye mawazo ya Bunge la Katiba.
Mwakagenda alisema kila kunapokuwa na jambo la msingi, kuna watu wanaingiza mambo yasiyofaa.
"Walianza na posho, mara kura ya wazi, mara saini imeghushiwa, sasa suala la Warioba na majibizano yasiyo na tija na Ikulu, mwacheni Warioba ameshamaliza kazi yake, lakini Salva akumbuke watu wazima hawapaswi kunenewa maneno yasiyo na msingi, Ikulu kutoa maneno makali sio uzalendo," alisema.
Jumuiya ya Wanafunzi wa Vyuo Vikuu (Tahliso), pia imeeleza kusikitishwa kwake na kauli za Ikulu za kumdhalilisha Jaji Warioba.
Rais wa Tahliso, Musa Mdede, alisema jana kuwa jumuiya hiyo haijafurahishwa na kilichosemwa na Ikulu dhidi ya Tume ya Jaji Warioba.
Mdede alisema kumdhalilisha Warioba kwa kazi aliyoifanya ni sawa na kumtusi, kwani hakufuata maoni ya chama, mtu, bali alifanya kazi kutokana na maoni ya wananchi.
Juzi, taarifa ya Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu iliyosainiwa na Salva Rweyemamu, ilisema Jaji Warioba ni mnafiki kwa kujifanya hajui ukomo wa tume yake.
Awali katika taarifa yake kwa vyombo vya habari jana, Jaji Warioba alisema ameiona taarifa ya serikali kuhusu Tume ya Mabadiliko ya Katiba, lakini ameshangazwa na maudhui na lugha iliyotumiwa na Ikulu dhidi yake.
Warioba alisema tume yake ilikuwa haijamaliza kazi wakati inakabidhi ripoti kwa Rais Kikwete kwani iliendelea na kazi ya kuandaa Randama ya Rasimu, Bango Kitita la Rasimu na maelezo aliyoyatoa kwenye Bunge Maalumu.
Alisema serikali ilijua tume ilikuwa inafanya kazi hiyo na nyaraka hizo zilikabidhiwa bungeni siku ya kuwasilisha rasimu.
Kuhusu madai kwamba wajumbe wa tume hiyo wanadai walipwe sh milioni 200 kila mmoja, Jaji Warioba alisema hakuna mjumbe aliyetoa dai kama hilo na serikali inajua.
Alisema alichozungumza ni muda wa kuandaa makabidhiano na kuandaa safari ya wajumbe kurudi makwao kwani aliwasilisha rasimu Machi 18, 2014, tume ilivunjwa Machi 19, 2014 wakati wajumbe wako Dodoma.
"Pamoja na lugha ya kejeli iliyotumiwa na serikali na kuniita mnafiki, busara ya kawaida ingeonyesha umuhimu wa serikali kujipa muda wa kufanya maandalizi ya kuwarudisha wajumbe nyumbani. Hata kama sheria ilitaja muda wa kuvunja tume, bado ilikuwa ni wajibu serikali kufanya mipango ya safari ya wajumbe baada ya kumaliza kazi. Sheria haikuizuia serikali kufanya hilo. Huo ni wajibu wa serikali na utaratibu wa kawaida unaotumiwa na serikali kwa tume zote inazoziunda," alisema.
source tanzania daima

Juzijuzi ilikuwa ccm wanasema Zito kadhalilishwa.....na huku chadomo na slaa wao wanasema Zito ni msaliti, Leo chadomo wanalia Warioba kadhalilishwa...tungoje ccm watasemaje.....
 
Wakuu kwa kweli baada ya nyerere mzalendo mwingine aliyebaki ndani ya ccm ni Warioba kwa kweli mzee huyu ni hazina
 
Dr. Slaa ameshapoteza mvuto kwa wananchi.

Kikwete na familia yake nao wanazidi kuidhalilisha na kuizamisha CCM ya Wakulima na Wafanyakazi iliyoasisiwa na Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kwa kuwabeba wezi, mafisadi, majangili, wauaji wa albino, walanguzi wa madawa ya kulevya na wahalifu wa kila aina ndani ya club yao wanayoiita CCM,
 
Wakuu kwa kweli baada ya nyerere mzalendo mwingine aliyebaki ndani ya ccm ni Warioba kwa kweli mzee huyu ni hazina

Uzalendo gani huo wa kuigawa Tanzania kupitia "Nchi 3/Serikali 3?" Tena usimlinganishe kabisa Warioba na Nyerere maana wako mbali kama mbingu na nchi esp kuhusu Muungano!
Halafu nilifikiri Tume imevunjwa kumbe pamoja na kuvunjwa huko Warioba bado ni "Mwenyekiti wa Tume?"
 
Porojo reeefu haijatolewa hata nukuu moja ya Kikwete inayomdhalilisha Warioba.

Amma kweli kuna watu wana viwanda vya uongo.
 
SIKU mbili baada ya Ikulu kutoa taarifa ya kejeli dhidi ya Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba, wanasiasa, wasomi, viongozi wa dini na wanaharakati wameitaka Ikulu ya Rais Jakaya Kikwete kumwomba radhi yeye pamoja na wajumbe wa tume yake.
Akizungumza na Tanzania Daima jana, Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa, alisema ukirejea kauli ya Rais Kikwete wakati akizindua Bunge la Katiba na kauli ya Ikulu juzi dhidi ya Warioba, utabaini kuwa kuna hila na chuki kubwa kati ya Ikulu, Warioba na tume yake.
Dk. Slaa alisema anaamini Jaji Warioba anasema ukweli kwani katika mazingira ya kawaida, isingewezekana baada ya kuwasilisha hotuba yake bungeni, usiku ule ule wakiwa mjini Dodoma, yeye na wajumbe wa tume yake wangekabidhi ofisi na kunyang’anywa magari.
“Nikirejea kauli ya Rais Kikwete bungeni ambapo jina la Jaji Warioba alilitaja zaidi ya mara sita, ukiunganisha na kauli ya Ikulu na msimamo wa CCM, utabaini kwamba kuna hasira kubwa dhidi ya Warioba kutokana na maoni aliyokusanya kutoka kwa wananchi. Rais na CCM wanaonyesha wazi kwamba hawaitaki katiba mpya,” alisema Dk. Slaa.
Mhadhiri Mwandamizi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Dk. Benson Bana, alisema Ikulu ikubali kwamba ilitumia lugha ya kejeli na dharau kwa Jaji Warioba, hivyo iangalie namna ya kumuomba radhi.
“Kwa wananchi waliofuatilia majibishano ya Ikulu na Jaji Warioba, watakubaliana nami kwamba wamemdhalilisha mzee wetu Warioba, hivyo msemaji wake ni vyema akaangalia namna ya kuyamaliza kuliko kuendelea kulumbana hadharani,” alisema Dk. Bana.
Alisema Ikulu ilipaswa itoe maelekezo ya makabidhiano kwa katibu mtendaji wa tume hiyo na siyo kuwadhalilisha wajumbe hao mjini Dodoma mara baada ya Mwenyekiti wao, Jaji Warioba kuwasilisha rasimu ya pili ya katiba mbele ya wajumbe wa Bunge hilo linaloendelea.
“Ikulu haikuwa na sababu ya kutoa kauli ya kashfa dhidi ya Jaji Warioba, hata kama alikosea. Wananchi wengi wanaofuatilia mchakato wa katiba, wanafahamu kazi yake nzuri akisaidiana na wajumbe wenzake. Kimsingi walistahili sifa na siyo kuwakejeli,” alisema Dk. Bana.
Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dayosisi ya Karagwe, Dk. Benson Bagonza, alisema kitendo cha Ikulu kutoa taarifa yenye maneno ya kejeli kwa Jaji Warioba ni sawa na kumvua nguo za ndani hadharani.
“Nimejisikia vibaya niliposikia taarifa ya Ikulu, ni kama imemvua nguo za ndani hadharani… hakupaswa kufanyiwa hivyo. Ikulu ilipaswa kutumia burasa ya kufanya makabidhiano kutokana na kazi nzuri aliyoifanya kwa Watanzania,” alisema Askofu Bagonza.
Askofu Bagonza alisema kama Ikulu ilivyomuamini, kumteua na kufanya hafla ya kumwapisha Warioba na wenzake 30, vivyo hivyo siku ya makabidhiano ya kuhitimisha kazi hiyo ingefanywa kulingana na umuhimu wa kazi yao.
“Hakuna jambo kubwa la historia linalomalizwa kwa kejeli ama malumbano, tumezoea kuona katika harusi na misiba baada ya kufanyika ama kumalizika, watu huvunja kamati zake kwa sherehe ndogo za kumalizia mabakia, ndivyo ambavyo tulitarajia Ikulu ifanye hivyo kwa Jaji Warioba. na kuongeza
“Nimesoma katika mitandao ya kijamii namna baadhi ya watu wakipinga hoja za Jaji Warioba kuhusu rasimu aliyoitoa, na hata malalamiko yake ya kutupiwa virago… hivi haiwezekani kupinga hoja zake bila ya kumtukana?” alihoji Askofu Bagonza.
Alisema Ikulu na Watanzania wanapaswa kufahamu kwamba hakuna mzalendo aliyebakia nchini zaidi ya Jaji Warioba, hata kama wapo wanaomkejeli.
“Sina shaka na uzalendo wa Jaji Warioba anaouonyesha katika nchi yake, tena ndiye mfano wa kuigwa kwa wote wanaotaka kuwa wazalendo,” alisema Askofu Bagonza.
Katika hatua nyingine, Kaimu Mwenyekiti wa Jukwaa la Katiba (Jukata), Hebron Mwakagenda, alisema kinachofanyika sasa ni kuwatoa watu kwenye mawazo ya Bunge la Katiba.
Mwakagenda alisema kila kunapokuwa na jambo la msingi, kuna watu wanaingiza mambo yasiyofaa.
“Walianza na posho, mara kura ya wazi, mara saini imeghushiwa, sasa suala la Warioba na majibizano yasiyo na tija na Ikulu, mwacheni Warioba ameshamaliza kazi yake, lakini Salva akumbuke watu wazima hawapaswi kunenewa maneno yasiyo na msingi, Ikulu kutoa maneno makali sio uzalendo,” alisema.
Jumuiya ya Wanafunzi wa Vyuo Vikuu (Tahliso), pia imeeleza kusikitishwa kwake na kauli za Ikulu za kumdhalilisha Jaji Warioba.
Rais wa Tahliso, Musa Mdede, alisema jana kuwa jumuiya hiyo haijafurahishwa na kilichosemwa na Ikulu dhidi ya Tume ya Jaji Warioba.
Mdede alisema kumdhalilisha Warioba kwa kazi aliyoifanya ni sawa na kumtusi, kwani hakufuata maoni ya chama, mtu, bali alifanya kazi kutokana na maoni ya wananchi.
Juzi, taarifa ya Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu iliyosainiwa na Salva Rweyemamu, ilisema Jaji Warioba ni mnafiki kwa kujifanya hajui ukomo wa tume yake.
Awali katika taarifa yake kwa vyombo vya habari jana, Jaji Warioba alisema ameiona taarifa ya serikali kuhusu Tume ya Mabadiliko ya Katiba, lakini ameshangazwa na maudhui na lugha iliyotumiwa na Ikulu dhidi yake.
Warioba alisema tume yake ilikuwa haijamaliza kazi wakati inakabidhi ripoti kwa Rais Kikwete kwani iliendelea na kazi ya kuandaa Randama ya Rasimu, Bango Kitita la Rasimu na maelezo aliyoyatoa kwenye Bunge Maalumu.
Alisema serikali ilijua tume ilikuwa inafanya kazi hiyo na nyaraka hizo zilikabidhiwa bungeni siku ya kuwasilisha rasimu.
Kuhusu madai kwamba wajumbe wa tume hiyo wanadai walipwe sh milioni 200 kila mmoja, Jaji Warioba alisema hakuna mjumbe aliyetoa dai kama hilo na serikali inajua.
Alisema alichozungumza ni muda wa kuandaa makabidhiano na kuandaa safari ya wajumbe kurudi makwao kwani aliwasilisha rasimu Machi 18, 2014, tume ilivunjwa Machi 19, 2014 wakati wajumbe wako Dodoma.
“Pamoja na lugha ya kejeli iliyotumiwa na serikali na kuniita mnafiki, busara ya kawaida ingeonyesha umuhimu wa serikali kujipa muda wa kufanya maandalizi ya kuwarudisha wajumbe nyumbani. Hata kama sheria ilitaja muda wa kuvunja tume, bado ilikuwa ni wajibu serikali kufanya mipango ya safari ya wajumbe baada ya kumaliza kazi. Sheria haikuizuia serikali kufanya hilo. Huo ni wajibu wa serikali na utaratibu wa kawaida unaotumiwa na serikali kwa tume zote inazoziunda,” alisema.
source tanzania daima

Kumbe source ni "Tanzania daima"...!!
 
Hasira za ccm ni kwa nini warioba hakuficha maoni ya wananchi? Ccm walipenda warioba awasilishe maoni ya ccm na sio wananchi!
 
Juzijuzi ilikuwa ccm wanasema Zito kadhalilishwa.....na huku chadomo na slaa wao wanasema Zito ni msaliti, Leo chadomo wanalia Warioba kadhalilishwa...tungoje ccm watasemaje.....
Wewe kweli FYATU!
 
Hasira za ccm ni kwa nini warioba hakuficha maoni ya wananchi? Ccm walipenda warioba awasilishe maoni ya ccm na sio wananchi!

Uko sawa mkuu huitaji kuwa na degree kujua Ikulu imemdhalilisha Warioba ni sababu wamezoea mawazo yao kupachikwa na si mawazo ya wananchi. Ndio matunda ya akili ndogo kutawala akili kubwa
 
Ingekuwa jina Warioba waliandika kinachokubaliwa na ccm tungeshuhudia kashfa kubwa ya mamilioni ya shilingi ikulu kuwapongeza tume. .
 
Ingekuwa jina Warioba waliandika kinachokubaliwa na ccm tungeshuhudia kashfa kubwa ya mamilioni ya shilingi ikulu kuwapongeza tume. .

Kaka mtu mwema kuliko wengine huwa ngumu sana kudhalilika!!!!!!
 
Porojo reeefu haijatolewa hata nukuu moja ya Kikwete inayomdhalilisha Warioba.

Amma kweli kuna watu wana viwanda vya uongo.

Mkuu kauli ya Ikulu ndiyo kauli ya Rais, huitaji uprofesa kutambua hilo.
 
Back
Top Bottom