Slaa ataja sababu za CCM kung’ang’ania madaraka

Kakke

JF-Expert Member
Dec 4, 2010
1,886
2,000
[h=1]Slaa ataja sababu za CCM kung’ang’ania madaraka[/h]

KATIBU Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa amesema kuwa Chama Cha Mapinduzi (CCM), kimeng’ang’ania madaraka kwa sababu kinajua kwamba wao wakiingia madarakani moja ya kazi yao ni kufagia mafisadi.
Akizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika Kijiji cha Kakola, mkoani hapa, Dk. Slaa alisema kuwa wizi na ufisadi na unyama unaofanywa na viongozi wa CCM ni wa kutisha, hivyo wanajua CHADEMA ikiingia madarakani, hawatapona.
“Ngoja leo niwaambie Watanzania siri kwanini CCM wanang’ang’ania madaraka kiasi cha kufikia hatua ya kuanza kutesa, kuteka na hata kuua watu wanaoonekana kuwa na mawazo mbadala yanayotishia uhai wa chama hicho madarakani. Wanaogopa nini itakuwa hatima yao iwapo CHADEMA ikishika nchi.
“CCM wanajua kuwa CHADEMA ikishika nchi, moja ya majukumu ya awali kabisa wakati tukiwatumikia watu ni kufagia ufisadi na mafisadi wenyewe. Hatutakubali kuvumilia mambo ya namna hii. Wakifika hapo wanaanza kujiuliza nani atapona. Tumewaambia hawawezi kukaa milele. Wananchi wameshaamua, wanaondoka,” alisema Dk. Slaa.
Katika mkutano huo, Dk. Slaa aliwapongeza Watanzania kwa kuiunga mkono CHADEMA dhidi ya ufisadi.
Alitoa kauli hiyo baada ya wanakijiji kumuuliza kwanini serikali inashindwa kushughulikia kashfa za ubadhirifu mkubwa wa rasilimali za umma.
Amelazimika kutoa pongezi hizo baada ya wanakijiji wa Kakola, kuhoji ukimya wa Serikali ya CCM katika kuchukua hatua dhidi ya wahusika wa kashfa nzito za ufisadi, wakitoa mfano wa wizi uliofanywa na Kampuni ya Kagoda Agriculture Ltd iliyokwapua sh bilioni 40 kutoka Benki Kuu (BoT), huku ikidaiwa kuwa fedha hizo zilitumika kwenye kampeni za CCM zilizomweka madarakani Rais Jakaya Kikwete mwaka 2005.
Pamoja na kuwepo kwa ushahidi wa nyaraka mbalimbali, ikiwemo hati ya kiapo cha wakili, serikali haijawahi kuchukua hatua kwa wahusika wa kashfa hiyo ya mabilioni ya fedha.
Mifano mingine ambayo wanakijiji hao waliitoa wakati wa kipindi cha maswali ambayo Dk. Slaa amekuwa akiruhusu katika mikutano yake yote kwenye ziara anayoendelea kufanya kuimarisha na kukagua uhai wa chama hicho mikoa ya Shinyanga, Kigoma, Tabora na Singida, wakisema ni ufisadi mkubwa kuachiwa, ni pamoja na;
Uuzwaji wa nyumba za umma uliofanyika wakati wa serikali ya awamu ya tatu na malipo ya wazee waliokuwa watumishi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kabla haijavunjika mwaka 1977, ambao wamekuwa wakipigwa danadana, wakati wenzao wa nchi za Kenya na Uganda walishalipwa na serikali zao.
“Ndugu zangu pamoja na kwamba maswali haya yanatia uchungu ukielewa namna ambavyo rasilimali za nchi yenu zinaliwa na hakuna anayewajibika, bado yamenipatia faraja na kunitia moyo zaidi kwa sababu wananchi mnafuatilia. Huko mijini CCM wanajigamba kwamba vita ya ufisadi ya akina Dk. Slaa inasikika mijini tu…eti vijijini hamna habari na mambo haya na hamuelewi.
“Nimefurahi sana mnajua ukweli kwamba fedha zinazokwapuliwa kwenye ufisadi wote mkubwa na mdogo, zingeweza kutumika kumaliza au kupunguza kero na matatizo mnayokabiliana nayo, mathalani ukosefu au upungufu wa huduma za msingi za jamii, ikiwemo maji, miundombinu, afya, elimu na nyingine nyingi.
“Hii inadhihirisha kwamba vita dhidi ya ufisadi inayolenga kutetea rasilimali za nchi tuliyoiasisi pale Viwanja vya Mwembeyanga imeendelea kuzaa matunda. Mzee wangu pale…Mzee Musa, ameuliza maswali muhimu sana, ameuliza kuhusu Kagoda, ameuliza kuhusu kuuzwa kwa nyumba za umma na kuhusu malipo ya wastaafu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki,” alisema Dk. Slaa.
Akijibu swali kuhusu ufisadi wa Kagoda kutochukuliwa hatua, Dk. Slaa alisema kuwa serikali inapata kigugumizi kwa sababu ukwapuaji wa fedha hizo unahusisha vigogo wakubwa akiwemo Rais mstaafu Benjamini Mkapa na kada mwandamizi wa CCM, Rostam Aziz huku fedha hizo zikitumika kwenye kampeni zilizomweka Rais Kikwete madarakani.
Aliongeza kusema kuwa wahusika wa wizi wa BoT uliofanywa na Kagoda wote wanajulikana na ushahidi upo, isipokuwa serikali haiwezi kuthubutu kuchukua hatua kwa sababu inaweza kuibua mlolongo wa kashfa na majina ya watu wazito na hata kufumua mtandao mkubwa wa ufisadi na mafisadi nchini, akidai CCM haiko tayari kuona hilo likitokea.
“Kwa CCM kuliko kuchukua hatua dhidi ya ufisadi na mafisadi wanaotafuna rasilimali za nchi, ni bora wananchi waendelee kukosa maji, dawa hakuna hospitali, shule ndizo hizi, elimu inadorora, watoto wa masikini hawana cha kurithi tena, wachache wanaendelea kutamba kwa kukwapua fedha za umma,” alisema.
Kuhusu nyumba za umma
Dk. Slaa alisema kuwa uuzwaji wa nyumba za umma uliofanywa na Serikali ya CCM wakati wa utawala wa Rais Mkapa ni moja ya ufisadi mkubwa kuwahi kutokea, huku akisema kuwa wanasheria wa CHADEMA wanalifanyia kazi suala hilo na siku za wahusika zinahesabika.
“Suala hili mzee wangu kama mwenyewe ulivyosema limetufanya tuonekane watu wa ajabu na limewafanya viongozi wa CCM wavuke viwango vya kuitwa mafisadi wakubwa. Hivi katika hali ya kawaida kiongozi anawezaje kuthubutu kupitisha uamuzi wa kuuza nyumba za umma, wakati serikali ipo.
“Tumepiga kelele sana kwenye suala hili. Sasa akina Profesa Abdallah Safari wanalifanyia kazi suala hilo, itafika mahali tutatua huu mzigo ambao tunajua umewaelemea wananchi kwa sababu nyumba zilizouzwa ni zenu. Kukosekana kwa nyumba hizo kumemgharimu mlipakodi Mtanzania masikini kuwalipia viongozi wao kukaa hotelini au nyumba za kupanga. Hatutakubali kunyamazia ufisadi,” alisema.
Aliwaeleza wananchi hao namna ambavyo viongozi wa serikali waliuziana mali hiyo ya umma kwa bei ya kutupa, huku wakiwa wametumia fedha za walipa kodi kuzifanyia ukarabati wa gharama kubwa hadi kwenye maeneo nyeti kama vile viwanja vya serikali na vituo vya polisi.
Wazee wa Jumuiya ya Afrika Mashariki
Dk. Slaa ambaye leo anaendelea na ziara yake katika Jimbo la Bukene baada ya msafara wake kutumia siku ya jana kufanya kikao cha ndani cha Kanda ya Magharibi ya chama hicho na kufanya matengenezo ya magari, alisema kuwa wastaafu wa EAC ‘wameingiliwa’ na Serikali ya CCM imewagawa makundi mawili ili wasifanikiwe.
Alisema kuwa kundi moja linaongozwa na mtu aliyedai ni tapeli na kwamba walioko upande huo tayari wameshalipwa fedha ‘nzuri’, hivyo sasa wanatumika kuwazunguka wenzao walioko kundi la pili ambao hawajalipwa stahili zao.
Aliongeza kusema kuwa serikali ilifanikiwa kushinda kesi ya wastaafu hao kwa sababu kuna nyaraka moja ilinyofolewa kutoka kwenye mkataba uliokuwa unalinda na kutambua haki za wastaafu hao, kigezo ambacho kinatumiwa na kundi la kwanza kuweka pingamizi mahakamani ili wastaafu wengine wasiweze kukata rufaa mahakama ya juu ili wapate fedha zao.
“Serikali imewagawa wastaafu wale katika makundi mawili. Walivyokuja kwangu kuomba msaada tuligundua kuwa kuna nyaraka imechomolewa kwenye mkataba ndiyo maana serikali ilishinda kesi. Sasa kundi moja limeanza kutumika kuweka pingamizi mahakamani ili wenzao walio wengi wasikate rufaa na kupata haki zao.
“Yote haya yanatokea kwa sababu serikali yenu ilipopokea fedha za wastaafu wale kutoka Uingereza, ilipanua mdomo na kuongeza ukubwa wa koo, ikabugia fedha zote. Wenzao wa Kenya na Uganda walilipwa stahili zao siku nyingi na serikali zao,” alisema Dk. Slaa.
 

cacico

JF-Expert Member
Mar 27, 2012
8,377
1,250
Ccm ni mashetani! Waondoke kwa style ya mabina! Puuuuuuuuuuuuuuuu!
 

utaifakwanza

JF-Expert Member
Feb 1, 2013
14,195
2,000
Hii PICHA NI YA MWAKA 2010 WAKATI wa uchaguzi mkuu. mleta mada anajaribu kuuhadaa umma
 

Nduka

JF-Expert Member
Dec 3, 2008
8,520
2,000
Mkono wa babu vipi? Au mmeshindwa qkupishwa picha hizo idara ya propaganda
 

utaifakwanza

JF-Expert Member
Feb 1, 2013
14,195
2,000
Dr. Slaa: Tukishika Dola tutaruhusu utengenezaji wa pombe ya gongo kisheria
Saturday, 14 December 2013 ·


Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimetoa mpya baada ya kueleza kuwa kitakapofanikiwa kushika dola kitaruhu Shirika la Viwanda Vidogo Vidogo (SIDO) kutengeneza mitambo ya kutengenezea pombe aina ya gongo. Katibu Mkuu wa Chadema, Dk.Willbroad Slaa, akizungumza na wananchi wa Jimbo la Kasulu Vijijini alisema kama gongo itatengenezwa kwa mitambo maalum itaondoa mianya ya rushwa kwa polisi ambao wamekuwa wakiwakamata wanaotengeneza kwa kificho na kuwafanya vitega uchumi vyao.


"Gongo sasa hivi ni haramu sababu inatengenezwa kwa kificho katika mazingira machafu, tukishika dola tutataka SIDO itengeneze mitambo ya kutengeneza gongo ili iwe katika hali ya usafi," alisema.


Mitambo hiyo itakayotengenezwa na SIDO itakapouzwa itaiingizia mapato serikali pia wauzaji wa gongo watafanya biashara hiyo kwa amani tofauti na sasa ambapo wanaifanya kwa kificho na wakikamatwa fedha zote wananufaika polisi.


Dk. Slaa alisema hata suala la kukamata watu wanaotengeneza silaha linapaswa kuangaliwa upya kwani wanaokamatwa wakifanya kazi hiyo wangekuwa wanashikiliwa kwa muda na baadaye wanapelekwa katika kiwanda cha serikali cha kutengenezea silaha ili watuhumiwa hao wapeleke ujuzi huo huko badala ya kuwafunga jela.


Dk. Slaa alisema matatizo yote yanatokana na wasomi kutofikiri namna ya kuisogea nchi mbele kimaendeleo.


"Nchi hii imelala, imechoka sababu waliopewa madaraka wamelala, wamejisahau hawatambui kuwa wamepewa nafasi hizo ili kuwatumikia wananchi," alisema.


CHANZO: NIPASHE
 

utaifakwanza

JF-Expert Member
Feb 1, 2013
14,195
2,000
Umesema ukweli, hiyo ndo dawa yao! hahahahaaa

acha hii inakuharibu ubongo
 

utaifakwanza

JF-Expert Member
Feb 1, 2013
14,195
2,000
unaakili sana we kijana hata mm nilikuwa najiuliza hii picha niliiona wapi?

tuko makini sana mkuu na huu uongo wa hawa walevi wa gongo. wanatumia picha za matukio ya mwaka 2010 kumpamba slaa baada ya kuona anadoda katika mikutano yake.
 

sawa

JF-Expert Member
Nov 22, 2010
2,750
2,000
tatizo lenu ni picha au ujumbe?mbona mandela alivyofariki amkutaka iwekwe picha ya wakati ana miaka 95?yaani ccm mpo kishabiki sana mpaka tuna hoji vichwa vyenu mnatumia kufikiri au kufugia nywele
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom