Slaa alalamikia bendera za CCM kwenye sehemu za biashara

Zak Malang

JF-Expert Member
Dec 30, 2008
5,404
233
Akiwa mkoani Arusha mgombea urais wa Chadema Dr W. Slaa amelalmikia jinsi chama tawala – CCM – kilivyoleta hali ya vitisho kwa wafanyabiashara pamoja na wale wadogo wadogo kwa kuwafanya wasimike bendera za CCM kwenye sehemu za biashara zao kwa kuogopa kubughudhiwa.

Amesema akiingia madarakani atapiga marufuku kusimika bendera za vyama vya siasa kwenye sehemu za biashara ili wafanyabiashara waendeshe shughuli zao kwa uhuru bila bughudha zozote.

Alishangaa jinsi CCM ilivyoileta hali hii miongoni mwa wafanyabiashara.

Unafiki wetu wa tanzania utatumaliza, na hili ndo jambo linalofanya CCM iendelee kutukandamiza na kufanya watakavyo, wakijua watawatisha wananchi na kweli tutatishika. Naanza kuamini kwamba watu wengi hawaipendi CCM lakini watu wataipigia kura CCM kwa sababu ya uoga unafiki na ubinafsi na kutokujali /kulithamini taifa letu. Tukiendelea na unafiki huu Vizazi vyetu vitapata taabu sana
 
Jaman jaman jaman ubunge mwanza kazi ipo masha hoi walijitokeza watu wachache mirongo da
 
Bendera za chama cha kikomunisti cha Nikolai Ceasescu wa Romania zilikuwa zimejaa kila mahali siku chache kabla hajadondoka. CCM thugs can force business owners to use their flag, but they cannot force them to vote for that disgraced party.

Idadi ya watu waliokuja wenyewe kumsikiliza Dr. Slaa na upendo walioonyesha kwake ni uthibitisho tosha kuwa wakati huu CCM haina kitu hapo Arusha. Hata wangesimika bendera kila choo mjini bado ni kazi bure.

Uchu wa CCM wa kuendelea kutawala, na kulewa kwao madaraka ndiko kunafanya walazimishe watu kupeperusha bendera zao. Hilo litakoma siku za karibuni.
 
Wafanyabiashara wengi hutundika HIRIZI ya chama mbele ya magari yao na kuning'iniza juu ya kioo cha ndani ya gari cha kuonea nyuma, iliyoadikwa neno CONGRESS.
 
yataka moyo sana kushuhudia upuuzi huu wa ccm na jinsi wafanyabiashara wanavyoiogopa na kuharibu maeneo yao ya biashara.........lakini kilichonifurahisha sana ni pale waliposema kuwa mabango wanaweka lakini kura zote kwa SLAA.
 
Huyo Slaa, bendera za CCM zinamwashia nini? Kaishiwa cha kusema kwenye kampeni zake nini?
 
Huyo Slaa, bendera za CCM zinamwashia nini? Kaishiwa cha kusema kwenye kampeni zake nini?
Naona umefika mwisho wa kufikiria.

Mnatoa vitisho kwamba kama mfanyabiashara yupo nje ya ccm hatokuwa salama. mna tofauti gani na jamii ya SICILY kule Italy enzi za GODFATHER
 
Jaman jaman jaman ubunge mwanza kazi ipo masha hoi walijitokeza watu wachache mirongo da

ni mmoja wa mawaziri ambao hata sura zao hunichefua ninapoona. I will be happy to see him gone.
 
MMESAHAU waziri Mkuu wa awamu ya TATU MH. SUMAYE aliwambia UKITAKA BIASHARA YAKO ISIBUGUZIWE peperusha bendera ya CCM.
 
Naona umefika mwisho wa kufikiria.
Mkuu, sijui huyo Slaa akiona hili kama hatolia...!
KATIBU%20MWENEZI%20WA%20CHADEMA%20MORO..JPG
 
wakuu tuwe sirias jamani

we have bigger problems kama njaa, afya, vifo vya wazazi, elimu, barabara nk.

i advice Dr. Slaa to remain focused kuliko kuanza kwenda mrama... you are missing your target by allowing to be carried aways that easily
 
Bendera za chama cha kikomunisti cha Nikolai Ceasescu wa Romania zilikuwa zimejaa kila mahali siku chache kabla hajadondoka. CCM thugs can force business owners to use their flag, but they cannot force them to vote for that disgraced party.

Idadi ya watu waliokuja wenyewe kumsikiliza Dr. Slaa na upendo walioonyesha kwake ni uthibitisho tosha kuwa wakati huu CCM haina kitu hapo Arusha. Hata wangesimika bendera kila choo mjini bado ni kazi bure.

Uchu wa CCM wa kuendelea kutawala, na kulewa kwao madaraka ndiko kunafanya walazimishe watu kupeperusha bendera zao. Hilo litakoma siku za karibuni.

Na hapa Tanzania tulitolewa shuleni na kupangwa kwenye mitaa ya Dar es salaam kumngojea Nyerere na swahiba wake Ceausescu wapite kutupungia mkono. Hii ilikuwa safari yake ya mwisho Ceausescu nje ya nchi. Ndani ya mwezi mmoja baada ya kutupungia mkono na swahiba wake Nyerere, alipinduliwa huko kwao Romania.
 
Huyo Slaa, bendera za CCM zinamwashia nini? Kaishiwa cha kusema kwenye kampeni zake nini?

Hizo pesa kama CCM mngezipeleka kununulia magodoro ya wagonjwa, au madeski mashuleni tungewaona mna akili kidogo. Lakini ubinafsi na kunogewa na utamu wa madaraka mmesahau na kufikiri kuwa maisha ya m-Tanzania ni miezi mitatu tu (wakati wa kampeni tu) baada ya hapo kula mbele mtindo mmoja.

Can't wait for the 31st of October 2010.

2010: ........It's time for Africa!!!!!! (Shakira). It's time for Tanzania too!!
 
wakuu tuwe sirias jamani

we have bigger problems kama njaa, afya, vifo vya wazazi, elimu, barabara nk.

i advice Dr. Slaa to remain focused kuliko kuanza kwenda mrama... you are missing your target by allowing to be carried aways that easily
Kampeni za mwaka huu huko bara ni za vituko na vioja, nakumbuka kampeni aina hii zilikuwepo sana katika chaguzi za mwaka 1995 na 2000 huko visiwani, na matokeo yake kila mtu anayajua.

Ni vema huko bara mkaangalia visiwani mwaka huu wanakampeni kwa namna gani. Msione haya kujifunza toka kwao.

Ama kama upinzani utaendelea na kampeni zisizo na tija kwa wananchi wake, wasitegee kufanikiwa kwa lolote lile.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom