Wegr
JF-Expert Member
- Apr 27, 2022
- 226
- 579
Wakuu nina kisa hapa naomba kuwashirikisha mnishauri namna ya kuamua au kufanya,
Sio mwandishi mzuri na maelezo ni marefu usichoke kusoma pengine unaweza jifunza kitu, twende,
Miaka 5 iliyoisha nilikutana na binti huko moja ya mikoa ya kanda ya ziwa tukaanzisha mahusiano yaliopelekea kapata mtoto wa kiume wakati nilikuwa nafanya kazi huko baadaye nikahamishwa kikazi nikaletwa moja mikoa Nyanda za juu kusini ndo nilipo mpaka sasa.
Wakati niko huku nikapokea simu yake kuwa anajisikia vibaya na mambo mengine mengi nikamshauri akapime na nikamtumia pesa maana mara ya mwisho wakati nataka kuondoka tulikunatana kimapenzi akaenda kupima akanitumia majibu ikaonesha ana mimba,
Tangu hapo nikaanza kulea mimba ni binti ambaye nilimpenda na hakuonesha mwenye mambo mengi ndo maana sikusita kulea mimba, hatimaye mtoto akazaliwa zoezi la kulea likaendelea bila shida nilijitahidi kwa kweli bila kuchoka mtoto akakua na akafika hatua ya kwenda shule mwaka huu mwanzoni tukashauriana na mzazi mwenzangu tukaona ni bora aanze hizi shule za watoto kwa sababu mamaake alikuwa anajishughulisha ikawa shida kumlea ikabidi aende huko kindagaten wanaita
Kama kaiwada nikaandaa mahitaji muhimu ya mtoto kwa ajili kuanza na ada nikawa nalipa kadri inavyotakiwa.
Sasa wakuu kinachoniumiza kichwa mpaka mda huu nisikose cha kufanya ni hiki na kichwa kupata moto mpaka mda mwingine nakosa hata hamu ya kula ni kuwa wakati wanataka kufungua hii likizo fupi ya juzi hii ya wiki mbili nikampigia mwalimu wake kutaka kulipa Ada kwa mshangao mkubwa kabisa mwalimu akaniambia mtoto amahamishwa shule aisee nilitaka kugongwa na gari barabarani nilijihisi vibaya sana ilibidi nikae sehemu nitulie kwanza, maswali yaliokuwa yanakuja kichwa ni Sababu za kumhamisha ni zipi? Kwa nini hakuniambia wakati mwezi wa 8 tarehe 16 tulikuwa pamoja na mzazi mwenzangu na mtoto? aisee mpaka sasa sielewi nikampigia simu ndo ananiambia ni kweli kamhamisha shule aliyohamia hasemi namba za shule husika napewa namba ambazo hazitumiki kichwa kinauma nikamtuma ndugu yangu afatilie shule alipo mtoto hata jina aliloniambia awali kwamba kahamia hicho kishule hakipo, maumivu mara mbili
Mpaka hivi ninavyoandika hapa ameshani block namba zangu zote
Nikipiga simu inatumika.
Wadau naombeni msaada tena ni hatua gani nichukue au kwa uzoefu ni nini kipo hapa, mbona ni wa kwangu kabisa na anafanana na Mimi!