Siyaelewi makato ya benki ya CRDB

Pole mpendwa kwa usumbufu uliopata, makato kwa mwenzi ni Tshs 1888 kwa akaunti inayoendeshwa kwa sarafu ya Tanzania mfano akaunti ya akiba, mwanafunzi.


Makato kwa njia ya simbanking kuangalia salio ni shs 354 na kutoa pesa kuanzia 0 -- 200,000 ni shs 2594 inapanda kulingana na kiasi unachotoa

kutoa pesa katika ATM gharama ni shs 944 kwa kila muamala utakaokua unaufanya na kutoa pesa kwa cashier dirishani ni 2594, mpka kwa kiwango kisichozidi mil 10
Wamepandisha tena mwaka huu!! Yeleuwiiiiii
 
Nilikuwa natumia CRDB kipindi nipo chuo kupokelea boom na kufanya saving, walikuwa wanaikata makato makubwa bila huruma niliwafuata mara kadhaa majibu yao ni makato ya kawaida tu, nilipoachana na masuala ya boom ikawa mwanzo na mwisho kukanyaga CRDB.
Afadhali nitumie international bankers huduma yao ni ya kueleweka
international bank ipi unayotumia?
 
Equity, BankABC na FNB
nilisikia FNB imefungasha virago..
Equity nasikia sifa nzuri juu yake...nitajarribu ifuatilia..
BankABC sina taarifa kamili kuihusu zaidi ya kwamba nimesikia Equity atainunua hivi karibuni
 
Mmh FNB amelala mbele mkuu?
nilisikia FNB imefungasha virago..
Equity nasikia sifa nzuri juu yake...nitajarribu ifuatilia..
BankABC sina taarifa kamili kuihusu zaidi ya kwamba nimesikia Equity atainunua hivi karibuni
 
La haulah hawa jamaa ndio maana wanapata hela sana na faida kubwa sijuagi kama wanakata hizi huwa nachukua tu basi, nilikuwa na current account na savings account, ila current account wanakata sh 10,000 kwa mwezi huduma zingine sijawahi kukagua na sijui labda nichukue statement ya miezi 2 ndio ntajua, ila tatizo lingine nikiwekewa hela kutoka nje ya nchi exchange rate wanayoitumia ni mbovu sana haifai kabisa isitoshe wanakata sh 10,000. nikiwekewa hapa nchini yani ktoka mikoani kiwango mara nyingi ni mil 2 kwenda juu wanakata sh 10,000 yan nakatwa mimi kwa kuingiziwa huwa sielewi hii pesa kwa nini wasisubiri nitoe ndio wakate kweli nitahama nimewasoma sasa ntakuwa nimeshakatwa hela nyingi sana mpaka sasa hivi.
Hapa kuna kitu mnaficha au haukijui kama una card ya visa mastercad kuna hela mnakata sijui ya nini kama 6000 hivi
Dah, hivi vitu wanavificha sana, sijui kwa nini kutoka 1882 kwa kadi ya tembo card Hadi 6000 kwa card ya Visa !! . Inabidi wawe wawaz kidogo bhana.
 
Back
Top Bottom