Siungi mkono Rais kutukanwa!

Wewe jingaaaa sana, na kwa taarifa yako wale wote wanaomchangia huyo kijana wanafuatiliwa, na lazima wote wakomeshwe
 
"Ninafikiri ni vyema na muhimu tukaendel, lakini k
Godbless Lema (Mp)
Hapo kamanda Lema umeteleza kabisa. Ulipaswa ukae kimya kabisa na siyo kuja na hoja ya kumponda ama kujifanya unamshauri huyo kijana mwenzetu. Jamii bado inaamini kaonewa na ana sababu zake za kuacha kukata rufaa kama hakukata. Mtu unapewa sifa katika jamii kulingana na tabia yako! Mimi pia nasema kaonewa na namshauri aendelee na mahakama za juu kudai haki yake. Kinachonikwaza hapo ni wewe kuuona umuhimu wa kutoa tamko kwa jambo lisilo na maana kama hilo na kusahau kabisa kwamba, alipouawa KAMANDA ALPHONCE MAWAZO hakuna tamko lolote lililotolewa na Magufuli, wala kiongozi yeyote wa serikali, au CCM. Na mbaya zaidi unalitoa tamko hili kati kati ya ukandamizaji mkubwa wa demokaria na haki za binadamu katika taifa. Mikutano imezuiliwa pamoja na makongamano ya vyama. Bunge kukosa usawa. Nk. Kubalance mambo tamko kama hili halifai. UMETELEZA KAMANDA.
 
Na mimi pia siungi mkono rais kutuitwa BWEGE.

Siungi mkonon wananchi/wapigioa kura upande wa pili kuitwa MALOFA na WAPUMBAVU.

Siungi mkono aliyepata "division Four" kuitwa KI.LA.ZA.

Kwa kutaja machache, yapo mengi siungi mkono....
 
Wewe jingaaaa sana, na kwa taarifa yako wale wote wanaomchangia huyo kijana wanafuatiliwa, na lazima wote wakomeshwe
hahaha, kama hii nchi ni ya wanasiasa pekee tutakomeshwa........ kutesa kwa zamu tu.
 

Hizi dhana za kuwatukuza viongozi na kuwaona na super beings ndo maaana wanatuibia kila siku . Uongozi ni dhamana tu haumu elevate mtu kuwa above other human beings. Kwenye nchi kama North Korea, China, Rwanda etc huko ndio kuna tamaduni kama hizo za kidikteta Kiongozi anakuwa Mungu wa pili sababu inaeleweka inaongozwa kwenye hiyo misingi ya kidikteta.Sasa nchi yetu ni ya kidemokrasia,,,huu utukufu wa viongozi tunaokuza gafla kwenye Awamu ya tano unatuweka kwenye same periscope na nchi kama Rwanda na North Korea
 
Nani huyu alietumia jina la Mheshimiwa humu ndo maana baada ya (Mb) ameandika (Mp)
 
Ulivyokuwa unamtukana batilda burian ulikuwa unaona sawa tu au kwa sababu ni muislamu
 
Lema ameshawachoka CHADEMA.. anataka kurudi nyumbani CCM
 
Ahsante mh lema kwa mara ya kwanza nakuunga mkono
Huu ni ukomavu mkubwa wa kisiasa uliouonyesha.
Hongera lema.
 
Lema mbunge wangu hilo neno linaeleza uhalisia uliopo. Pole kama huelewi lakini ndiyo sifa pekee ya mtu wako.
 
K
Ni Kweli, Lakini Busara Ya Kumkanya Na Kumsaidia Ni Bora Zaidi Kuliko Kumwacha Akaozee Jela Wakati Inawezekana Kumrekebisha Mtaani.
Je, Huyo Hakuwa Mmoja Kati Ya Vijana Walioitwa Wapumbavu Kisa Wanataka Mabadiliko?
Kwamba wamejitokeza watu kumchangia yapo mawili 1 wanaunga mkono 2 wanashiriki kwenye adhabu ya Isaac. Mimi namtia moyo asikatishwe tamaa na adhabu kwa kusimamia anachokiamini na tunachokiamini baadhi yetu.

Sikuelewa mlalamikaji kama aliathiriwa na cho chote; ndiyo maana vimbele mbele tu wamepeleka kesi mahamakamani.
 


I love this....
 
Kemea kwanza tendo linalofanywa na vijana na madiwani wenu. Kitendo cha kumchangia fedha mtuhumiwa kinatoa taswira mbaya kwa chama chenu japo wengine wanaona ni kitendo cha kishujaa lakini huwezi kuenzi ushujaa katika mambo ya kijinga.
Kaguswa malaika asiyetakiwa kukosolewa
 
Tulia Atkson amepewa adhabu gani na bunge baada ya kumwita mbunge mwenzake bwege❔
 
Lem
Asante Lema,

Lakini mbona kama alichangiwa 4.5m za faini na viongozi wa chama chako mkoa, au mlimchangia baadae mkamwambia lakini kijana umekosea au ulinyamaza kimya.
Lema Lema usisahau ujasiri unaotuhubiria mimi naongeza mchango wangu kwa Isaac na nimekumind sana
 
Kwa akili za watanzania huyo kijana angeachwa kwa kuonywa au kumrekebishua mtaani ange/wangesema mbona flani hakufungwa au kupigwa faini?.

So kwa muktadha uluochukua nafasi na kumpa adhabu ile ni funzo sana kwa watz wenzangu ambao mna tabia ya kujikweza na kusahau sahau.
 
Halafu wee ujue unatutafutia balaa? Poa tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…