Siungi Mkono hoja ya Zitto

Mnufaikaji wa wizi wa hela za serikali atakuwa mtu wa ajabu sana akiunga mkno hoja ya Zitto, Lakini wote ambao tumeibiwa tunamuunga mkono Zitto na kumsaidia kupata sahihi za kutosha alianzishe na tutapiga kampeni zipatikane kura za kutosha kutokuwa na imani. Hii ni hatua muhimu sana kuondoa udhalimu na wizi wa mchana
 

check hii kutoka kwenye katiba.....

53A.-(1) Bila ya kujali masharti ya ibara ya 51 ya Katiba hii,
Bunge linaweza kupitisha azimio la kura ya kutokuwa na imani na
Waziri Mkuu endapo itatolewa hoja kupendekeza hivyo na
ikapitishwa kwa mujibuwa wa masharti ya ibara hii.

(2) Bila ya kuathiri masharti mengineyo ya ibara hii, hoja
yoyote ya kutaka kupitisha kura ya kutokuwa na imani na Waziri
Mkuu haitatolewa Bungeni endapo-

(a) haina uhusiano na utekelezaji wa majukumu ya Waziri
Mkuu kwa mujibu wa ibara ya 52 ya Katiba hii, wala
hakuna madai kwamba Waziri Mkuu amevunja Sheria
ya Maadili ya Viongozi wa Umma;


Hivi mawaziri wanawajibika kwa waziri mkuu au kwa rais?
 
Tusubiri tuone mazingaumbwe.

Yawezekana lisifanikiwe kama unavyoomba, lkn majority will never alter the fact. Kutokutosha kwa kura za kumkosea imani PM ni zao la unafiki wa watu fulani lkn hata wao ndani ya mioyo yao wanajua kuwa anastahili kutoka. Pinda ni legelege, bora mwizi Lowassa kuliko Pinda anayemwogopa Jairo. Mbona Nyoni alisimamishwa na Pinda huyo huyo kama sio ulegelege tu unamsumbua.

Kwanza kwa taarifa yako, hakuna jambo litakalomnyoosha JK kama kumtoa Pinda kwa kura
 
SinaJina1 hajagundua hilo ni rahisi kupiga kura ya kutokuwa na imani na PM kuliko uraisi kutokana na ukweli baadhi ya wabunge wengi wa CCM wanajua hii ndiyo awamu yao ya mwisho kwenda bungeni kutokana na kutoendana na kasi ya mageuzi.

Hapo nimekusoma Kamanda
 
Mimi pia nilijiuliza hilo but kwa kuwa sheria ndivyo isemavyo nadhani hakuna jinsi BUT swali langu, kama Waziri Mkuu anawajibishwa na wabunge kwa kushindwa kumshawishi au kumshauri Rais juu ya maamuzi muhimu, hata akiondolewa/akijiuzulu akawekwa mwingine what if issues zinazohusika ni zile zinazomkwaza Rais au what if Rais hashauriki, watawajibishwa mawaziri wakuu wangapi??

Nakubaliana na sheria but ingerekebishwa kidogo kwa Rais kupunguziwa madaraka aliyonayo. Iwekwe kuwa pale ambapo Rais anastahili kumuwajibisha waziri flani basi BUNGE nalo liwe na mamlaka flani katika kushinikiza hilo ili Rais naye ajue kuwa yeye si mwenye madaraka ya mwisho na kama itatokea atashindwa na nguvu ya BUNGE juu ya jambo flani basi akubali kutekeleza. Mf. Kumwajibisha Pinda kwa kushindwa kumshauri Rais au kumshawishi Mkuu kumfukuza kazi Mkulo (ambaye tuseme kwa mfano ni swahiba au Mkwe wa Rais) ni kama kumwonea kwa kuwa hata Waziri Mkuu ajaye akileta same allegations za Mkulo kwa Rais (Swahiba au Mkwe wake) bado reaction zitakuwa the same.............sasa tutavote no confidence kwa Mawaziri wakuu wangapi?

Mwajibisheni Pinda kwa mujibu wa Sheria but hata madaraka ya Rais katika maamuzi pia yapunguzwe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…