Sitti Mtemvu kuburuzwa Mahakamani

Sitti Mtemvu kuburuzwa Mahakamani

rpg

JF-Expert Member
Joined
Oct 10, 2007
Posts
3,620
Reaction score
1,478
Huku akiwa ametangaza kuvua taji la urembo la Taifa 'Redd's Miss Tanzania 2014', Sitti Mtemvu, anadaiwa kuandaliwa hati ya mashtaka kuhusiana na tuhuma za kudanganya umri wake ili kutimiza sifa za kushiriki shindano hilo ambalo fainali zake kitaifa zilifanyika Oktoba 11, mwaka huu kwenye Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa habari NIPASHE ilizozipata jijini jana zinadai kuwa Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (Rita) tayari wameshabaini kwamba Sitti alipata cheti kipya kwa njia ya udanganyifu na sasa wanaendelea kuchunguza ili kuwabaini wale waliohusika katika kukipata cheti hicho ili wote waweze kushtakiwa pamoja.

Chanzo chetu kiliendelea kueleza kwamba taasisi hiyo imechukizwa na sakata hilo na inataka kuchukua hatua zinazostahili ili iwe fundisho kwa wote ambao wanania ya kufanya kosa la aina hiyo.

"Imebainika kuwa watu wengi wanatoa taarifa zisizo sahihi ili kupata vyeti vipya vya kuzaliwa kwa lengo la kuwasaidia katika kupata ajira, nafasi za masomo au kurahisisha mambo yao mengine, sasa hatutaki taasisi yetu iendelee kuchafuliwa jina, kuna tamko litatolewa hivi karibuni, hatutakaa kimya," kiliongeza chanzo chetu.

WANASHERIA WALONGA
Alex Mgongolwa, wa jijini aliliambia gazeti hili kuwa kosa la kughushi limegawanyika katika sehemu mbili na kila moja lina adhabu yake tofauti.

Mgongolwa alisema kuwa kosa la kwanza la kughushi nyaraka adhabu yake ni miaka saba jela kama ilivyoainishwa katika kifungu cha kanuni cha adhabu namba 333.

Mwanasheria huyo ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya Yanga, alisema katika kifungu cha 337 endapo mtu atapatikana na hatia ya kutumia hati iliyoghushiwa, hukumu yake itakuwa ni kwenda jela kwa muda wa miaka mitatu.

"Kama mtuhumiwa atakuwa amekutwa na hati hiyo ya kughushi na alishiriki pia katika kuitengeneza atakumbana na adhabu zote mbili," alisema mwanasheria huyo maarufu na mwanachama wa Klabu ya Yanga na Mwenyekiti wa zamani wa Kamati ya Sheria, Maadili na Hadhi za Wanachama wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).

Katibu Mkuu wa zamani wa Simba na aliyekuwa Mkurugenzi wa Vyama na Masuala ya Sheria wa TFF, Evodius Mtawala, alisema kuwa kifungu cha 339 kinaeleza kwamba mtu atakayebainika amedanganya kwa kughushi atatakiwa kwenda jela kwa muda wa miaka saba.

"Ila kifungu cha 338 ambacho kinaeleza makosa ya kughushi wosia, hati za ardhi, hukumu ya mahakama, hundi, nyaraka za benki, fedha au malipo yoyote, adhabu yake ni kifungo cha maisha," alisema Mtawala.

Naye Wakili, Damas Ndumbaro, alisema kuwa kwanza mtu atakayebainika na kosa hilo anatakiwa kukamatwa na kufikishwa mahakamani mara moja na hukumu yake itatolewa ya kwenda jela na haina faini.

"Uthibitisho ukishapatikana mtu huyo anafikishwa mahakamani moja kwa moja," Ndumbaro aliongeza.Kifungu namba 28 (3) cha Sheria ya Kuandikisha Vizazi na Vifo ya Rita kimeweka wazi kuwa atakayebainika ametoa taarifa za uongo ili kupata cheti cha kuzaliwa adhabu yake ni kwenda jela kwa muda usiopungua miaka mitatu.

Cheti ambacho Rita inakifanyia uchunguzi ni kile kilichotolewa Septemba 9, mwaka huu chenye namba 1000580309 ambacho kinataja jina la baba wa Sitti ni Abbas Mtemvu Zuberi (Mbunge-Temeke) na mama yake ni Mariam Nassor Juma ambaye ni diwani wa Temeke, jijini Dar es Salaam.

Cheti hicho kinaonesha Sitti amezaliwa Mei 31, 1991.Moja ya taarifa za awali zilizoonekana kwenye mitandao ya kijamii siku moja baada ya mrembo huyo kushinda taji ni hati ya kusafiria inayoonesha ilitolewa Februari 15, 2007 na muda wake wa kutumika mwisho ukiwa ni Februari 14, 2017, huku zikitaja tarehe ya kuzaliwa Sitti ni Mei 31, 1989.

CHANZO:
NIPASHE
 
ataburuzwa mahakamani wapi? ya kimataifa au ya taifa? maana kama ni ya taifa, ni changa la macho tu hapa, hakuna mpya. ziko issue kubwa kuliko ya huyo alogushi cheti lakini zimeishia hewani. ngoja tusubiri tuone.
 
Sasa mtu ashajulikana kuwa ni miss bibi BOMBA , iweje waendelee kumfuga fuga mtaani? kama vipi atiwe nguvuni kama makanjanja wengine wanao ghushi nyaraka nyeti ili kujipatia ulaji . Chonde chonde Rita tunaomba mrudishe hadhi na heshima yenu kama hapo zamani.
 
Last edited by a moderator:
mimi nataka kuona kawekwa sero na wale wa rita wote ... uhuni mwisho umefika
 
ataburuzwa mahakamani wapi? ya kimataifa au ya taifa? maana kama ni ya taifa, ni changa la macho tu hapa, hakuna mpya. ziko issue kubwa kuliko ya huyo alogushi cheti lakini zimeishia hewani. ngoja tusubiri tuone.

Labda mahakama ya mbuzi a.k.a VINGUNGUTI.
 
Sasa mtu ashajulikana kuwa ni miss bibi BOMBA , iweje waendelee kumfuga fuga mtaani? kama vipi atiwe nguvuni kama makanjanja wengine wanao ghushi nyaraka nyeti ili kujipatia ulaji . Chonde chonde Rita tunaomba mrudishe hadhi na heshima yenu kama hapo zamani.

kama hawasikii mwakani tunawazika wote waache wanafoji foji tu utakuta yalipewa laki mbili tu
 
89 na 91 Sioni sababu ya huyu Sitti kilaza kughushi, matatizo mengine ya kujitakia.

Kuna uwezekano alipoteza cheti cha kuzaliwa na kwenda kuchukuwa kipya wakakosea mwaka?

Maana mpaka sasa siioni sababu ya huyu mkosa adabu kughushi tofauti ya miaka miwili tu!
 
Kwahiyo hicho cheti chake kinapotea tu siku 30 kabla ya shindani la mlimbwende wa miss Tanzania?
Mwizi ni mwizi tu mkuu FaizaFoxy hata aibe kalamu ni mwizi tu.
 
Last edited by a moderator:
89 na 91 Sioni sababu ya huyu Sitti kilaza kughushi, matatizo mengine ya kujitakia.

Kuna uwezekano alipoteza cheti cha kuzaliwa na kwenda kuchukuwa kipya wakakosea mwaka?

Maana mpaka sasa siioni sababu ya huyu mkosa adabu kughushi tofauti ya miaka miwili tu!

Unazeeka vibaya,,, sababu ya kufoji Ni kupata cheti chenye umri unaoendana na sifa za kushiriki miss Tanzania, hivyo ikabidi wa-adjust miaka miwili. Sasa inakula kwake, mtoto WA kiislam na kuacha mapaja nje wapi na wapi? Au na wewe uliacha Sana vyombo nje enzi zako!
 
Eti siti ata buruzwa makamani!!ktk nchi hii hii?labda kwa msaada wa wahisani!
 
Unazeeka vibaya,,, sababu ya kufoji Ni kupata cheti chenye umri unaoendana na sifa za kushiriki miss Tanzania, hivyo ikabidi wa-adjust miaka miwili. Sasa inakula kwake, mtoto WA kiislam na kuacha mapaja nje wapi na wapi? Au na wewe uliacha Sana vyombo nje enzi zako!

Astaghafirullah, akutukanae hakuchagulii tusi.

Mama'ko angekuwa hajaacha nje vyombo vyake ungezaliwa wewe?
 
Taasisi za serikali kama RITA na NIDA zinatakiwa ziendeshwe na watu wazalendo, werevu, wenye weledi na waadilifu katika majukumu yake.
Hawatakiwi watu wanaofanya mambo kwa mtindo wa bora liende (business as usual) kutokana na umuhimu wake kwa taifa.
Ukifanya utafiti kidogo tu utaona uwepo wa watu ambao wana vyeti, vitambulisho kutoka taasisi hizo vyenye taarifa ambazo siyo sahihi na hata wengine siyo raia wa Tanzania!
Hali hii haikubaliki na haitakiwi iendelee.
 
Back
Top Bottom