Aliyekuwa Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba Samwel Sitta amesema kilichomkuta aliyekuwa Mwenyekiti wa tume ya mabadiliko ya Katiba jana ni sawa na kujitakia mwenyewe.
Akihojiwa muda mfupi uliopita na Redio Voice of Tabora kuhusu maoni yake kwa vurugu kubwa iliyoongozwa na Paul Makonda jana, Mzee Sitta amesema kimsingi wananchi walio wengi wanaunga mkono Katiba pendekezwa.
Mzee Sitta amesema Jaji Warioba anapaswa kutulia kwani akiendelea anaweza kuaibishwa kuliko aliyofanyiwa jana pale Ubungo blue pearl.
Mzee Sitta amemtaka Warioba awaachie wananchi Katiba pendekezwa waamue wenyewe kwa njia ya kura.Sitta ameendelea kusema watanzania wa sasa siyo wajinga na wakikuona unawadanganya watakuvamia hapohapo.Amedai uelewa wa wananchi kwa sasa ni mkubwa kuliko wakati mwingine wowote.
Alipoulizwa swali kuhusu Uvumi kwamba yeye ndiye anamfadhili na kumtuma Paul Makonda kupambana na yeyote anayempinga Mzee Sitta amecheka na kusema hatajibu hilo swali.
samwel sitta amepoteza sifa za kuwa kiongozi wa kuaminiwa na umma kwa nafasi yoyote na huu ndo mwaka wake wa mwisho kuwa kiongozi wa umma. Nina uhakika hata akigombea ubunge Paul Andrew Maganga atamshinda mapema asubuhi na akigombea uraisi kura za maoni hazitafika hata 30.
Ile laana ya watumishi wa Mungu imemmaliza ameungana na wahuni kina paul makonda na kuanzia sasa ntakuwa naandika jina lake kwa herufi ndogo
Nawewe umeingizwa town?,habari ya kupika hiyoKwa maelezo yake Sitta, inawezekana kabisa kuwa ndiye aliyemtuma, kugharamia na kuratibu mpango wa Makonda!
Aliyekuwa Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba Samwel Sitta amesema kilichomkuta aliyekuwa Mwenyekiti wa tume ya mabadiliko ya Katiba jana ni sawa na kujitakia mwenyewe.
Akihojiwa muda mfupi uliopita na Redio Voice of Tabora kuhusu maoni yake kwa vurugu kubwa iliyoongozwa na Paul Makonda jana, Mzee Sitta amesema kimsingi wananchi walio wengi wanaunga mkono Katiba pendekezwa.
Mzee Sitta amesema Jaji Warioba anapaswa kutulia kwani akiendelea anaweza kuaibishwa kuliko aliyofanyiwa jana pale Ubungo blue pearl.
Mzee Sitta amemtaka Warioba awaachie wananchi Katiba pendekezwa waamue wenyewe kwa njia ya kura.Sitta ameendelea kusema watanzania wa sasa siyo wajinga na wakikuona unawadanganya watakuvamia hapohapo.Amedai uelewa wa wananchi kwa sasa ni mkubwa kuliko wakati mwingine wowote.
Alipoulizwa swali kuhusu Uvumi kwamba yeye ndiye anamfadhili na kumtuma Paul Makonda kupambana na yeyote anayempinga Mzee Sitta amecheka na kusema hatajibu hilo swali.
Kilichomkuta jana Warioba ni msiba wa kujitakia
Kuna siri gani hawataki midahalo. Wananchi wananataka kujua
Kwa maelezo yake Sitta, inawezekana kabisa kuwa ndiye aliyemtuma, kugharamia na kuratibu mpango wa Makonda!