G Sam
JF-Expert Member
- Apr 20, 2013
- 12,279
- 38,855
Kwa mara ya kwanza hapa Dodoma, Samwel Sitta kiongozi wa bunge maalum la katiba amekiri kwamba wana wakati mgumu.
Hayo ameyaongea wakati akiwa na kikao na kamati ya uongozi pamoja na ile iliyoandaa rasimu ya tatu ya katiba, nimethibitisha.
"Kwa kweli muda unavyozidi kwenda na kila jambo tunalofanya tunakumbana na upinzani mkali kinyume kabisa na matarajio yetu" alisema Sitta.
Sitta pia katika kikao hicho amesema kuwa anajiuliza sana ni kwa nini upepo unawabadilikia hivyo na anaonekana kukata tamaa kama rais Kikwete ataridhia rasimu ipigiwe kura mapema.
Sitta kwa mara ya kwanza tangu aanze mchakato huu wa katiba amesikika akisema kuwa ana wasiwasi huenda akageukwa siku za usoni na mahasimu wake kisiasa ndani ya CCM kwa lengo la kulipa kisasi ingawa hakugusia ni kisasi cha aina gani.
Ni ukweli usiopingika kuwa Samwel Sitta amejikuta akipoteza kabisa mvuto aliokuwa nao kisiasa baada ya kulingoza bunge la katiba na kujikuta akikosolewa na kutupiwa shutuma nzito waziwazi kama msaliti mkubwa wa wananchi kwa sasa.