Sitta pengo lako halizibiki lakini unaweza kushauri | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sitta pengo lako halizibiki lakini unaweza kushauri

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Burigi, Jul 3, 2012.

 1. B

  Burigi Member

  #1
  Jul 3, 2012
  Joined: Jan 11, 2011
  Messages: 45
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 15
  Nimekuwa nikifuatilia sana mjadala wa kikao cha bunge kinachoendelea hivi sasa bungeni kwa kweli inatia huzuni kubwa kwa spika,naibu spika mwenyekiti Jenista muhagama na bwana mabumba kweli nyote ni janga kwa taifa na msipoangalia mnakaribisha vurugu na nyinyi ndiyo chanzo cha kelele bungeni mmeshindwa na ninadiriki kusema nafasi hizo haziwafai hata kidogo. Kiti hicho ni sawa refa ambaye anatakiwa aone makosa ya kila mchezaji na atoe adhabu bila kupendelea hata kama yeye ni shabiki wa timu mojawapo humo ndani inasikitosha kuona kiti kinafikia hata kushabikia maneno ya hovyo yanayotupwa upande wa pili ni sawa refa kati kati ya mchezo na yeye arukeruke kushangilia bao limelofungwa lazima vurugu zitatokea tu na mchezo utaisha vibaya tu.

  sisi wana ccm wenzenu bado tuna waamini lakini myafanyayo si kichefuchefu kwa wapinzani na wasio na chama bali hata wana ccm waadilifu na wapenda haki wapendezwi na uwezo wenu huo na hiyo imekuwa ikileta hisia kama chama chetu kimeshindwa na kinatumia mabavu kizima hoja.

  Wana ccm wabunge wetu hivi mnafikiria yasemwayo na wapinzani hayatugusi sisi kwa kuwa tu ni wanachama wa ccm la hasha nafikiri mu vipofu wakubwa kama hamtambui hil?

  i bunge la jana wapinzani wameongea mambo ya maana sana kuhusu utawala bora kuanzia wabunge
  wa cuf ,chadema nccr lakini wabunge wetu wa ccm hakuna hata mmoja alieweza kukemea hali ya nchi ya mauaji dhuruma utawala bora uwajiikaji hata mmoja ni aibu bado spika amekuwa akiwaeleza ukweli kweli kama wananchi wana waangalia kwa mfanyayo bungeni na wanawapima mfanyayo bungeni ukweli ni kwamba wapinzani wanakonga nyoyo za wananchi wote bila itkadi hata wana ccm tuna wa admire kwani wanafanya kazi ya wananchi siyo wagongameza na wenye kuuna mkono kisha wanaeleza udhaifu kama kuna udhaifu utaungaje mkono mia kwa mia wananchi tuna washangaa sana tunawaona kama nyinyi ni wasanii na hamtuwakilishi sisi wananchi bali ni maslahi binafsi kwani haiwezekani kitu kiwe sawa kwa asilimia 100 halafu ukitoe kasoro kwa asilimia 60 hivi mpo serious kweli.

  Ninasikitishwa na wabunge vijana wa CCM kuwa na uwezo mdogo sana wa uelewa nakuendekeza siasa za kina mzee wetu kingunge hawaelewi kama siasa hizo hazipo tena na wananchi ni waelewa kabisa namshangaa mbunge machachari eti ndiyo machachari wetu wana ccm na tumempa safu ya kushambulia maadui wetu yaani opposition parties ni aibu na hawa ndiyo wachimba kaburi na washona sanda wa chama chetu hawa ni kina MWIGULU MCHEMBA ni janga la chama chetu ni aibu kuitangazia chadema ni chama cha kikabila na undugu na ukanda wakati akijua bungeni hapo yupo VITA KAWAWA NA ZAINABU KAWAWA pia alikuwepo ANNA KILANGO MALECELA NA SAMUEL MALECELA walikuwepo PIUS MSEKWA NA ANNA ABDALLAH alikuwepo DR ABDALLAH KIGODA NA DR AISHA KIGODA ALIKUWEPO MAMA BEATRICE SHERUKINDO NA MZEE SHERUKINDO wapo UVCCM RIZIWANI KIKWETE NA MA RAFIKI ZAKE WOTE Sisi wananchi haya hayatuhusu na wala hayana tija kwetu tunachoangalia ni uwezo wao wa kufanya kazi au ndiyo mnataka kutuaminisha kama wasemavyo Wapinzani wetu kama tuko tunakata roho na hatujui tusemalo tunatatapa wakati wapinzani wakipigania haki na uporaji wa rasilimali za taifa wakiteka pesa za UMMA ZA EPA KAGODA NA MMEZOWEKA USWISI ZIRUDI nyie mnakejeli eti takukuru na usalama wa taifa unafanya kazi ya kutosha kweli bwana mwigulu unaeza tetea jambo hili wewe kama kijana wa taifa hili na TV zote zikikuonyesha ukitoka mapovu mdomoni ukijua watanzania ni wajinga hawaelewi ninakusikitia sana nina wasikitikia wabunge wa ccm ninaiskitikia ccm yangu kweli tumefika hali ambayo mwanandani kisha chimbwa tukisubiri safari yetu ya
  Milele

  Utamdanganyaje mwanachi wa iringa mbeya kigoma biharamulo shinyanga mwanza kigoma,maswa mbozi kuwa chadema ni chama cha wachaga wakati wanawabunge waliowachagua wao wasio wachaga au wakati wabunge wachaga ni wachache kuliko makabila mengine je sisi tunataka propaganda kweli.

  USHAURI WANGU KWA WANA CCM NYIE NI CHAMA TAWALA HAMUWEZI KUPAKA MATOPE CHAMA PINZANI WAKATI NYIE MMEJIPAKA MAVI POPOTE PALE CHAMA TAWALA KINA KASHFA NYINGI KWA HIYO UKIRUSHAKASHFA KWA CHAMA PINZANI UTAKUWA UNAJIMALIZA MWENYEWE BADILISHENI MTAZAMO KILA LITOKALO UPINZANI LIWE NI CHALLENGE KWENU KULIREKEBISHA NA SIO KULITETEA HUKO NI KUVUNJA IMANI KWA WANANCHI PROPAGANDA NA MABAVU HAVINA NAFASI TENA KUMBUKA MANENO HA HEKIMA YA SUGU JANA NYINYI VIJANA WA CCM MNAPOKAA NA WAZEE VIONGOZI WENU MUWAAMBIE HALI HALISI KUHUSU URAIANI NA KUJIPENDEKEZA KWENU KUTOKUSEMA UKWELI NI KIFO KWA CHAMA CHETU UKWELI NI KWAMBA CCM TUMECHOKWA NCHI NZIMA SIO SIRI HAKUNA CHA KUJIFARIJI TUSEME UKWELI HATA KAMA NI MCHUNGU KIASI GANI MH SPIKA MAKINDA JUZI ALIZUNGUMZA HUKO MTAANI WANANCHI WANAWAANGALIA TUTAFANYAYO BUNGENI WABUNGE WENGI WA CHAMA TAWALA WALIPIGA MAKOFI YA KINAFIKI LAKINI UKWELI NI KWAMBA WANANCHI WANAPIMA MUYASEMAYO YANAWAGUSA KIASI GANI NA HUKO MTAANI UKWELI NI KWAMBA CHADEMA CUF NCCR KOMBAINI TIMU YAO INA IDADI SAWA NA MABAO YA SPAIN NA CCM INA KIPIGO SAWA NA CHA ITALY TUWENI MACHO HIKI KIPIGO SI KIDOGO.
   
 2. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #2
  Jul 3, 2012
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  Inapofikia point ya kuitetea ccm, Sheria Kanuni na Taratibu zinawekwa kapuni.
  Mjomba waache wote hao waandae kaburi la chama chao, kwa kilipofikishwa sasa naamini hakuna tena U-TURN!
   
 3. brazilian

  brazilian JF-Expert Member

  #3
  Jul 3, 2012
  Joined: Feb 10, 2012
  Messages: 607
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Hivi huyu Mabumba kweli anastahili kuwa mwenyekiti. yaani hoja kabisa ni afadhali hata ya Jenista ingawa naye ni kilaza sana. Mabumba kweli amebumbwa kwa udongo wa kichuguu
   
 4. GeniusBrain

  GeniusBrain JF-Expert Member

  #4
  Jul 3, 2012
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 4,321
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Washwa washwa ni ugonjwa mbaya sana na umeanza kuwakumba wabunge wa cdm, na sasa unaelekea kwa wanachama na wapenzi wao km mtoa mada na wengine. Na dawa ya ugonjwa wa washwa washwa hakuna zaidi ya kukunwa pale panapowasha.
   
 5. k

  kbhoke Member

  #5
  Jul 3, 2012
  Joined: Apr 20, 2011
  Messages: 84
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 15
  Viongozi wa CCM wamefikia ukomo wa kufikiri. Hatutegemei cha ajabu. Elimu pia inawaangusha.
   
 6. mtotowamjini

  mtotowamjini JF-Expert Member

  #6
  Jul 3, 2012
  Joined: Apr 23, 2012
  Messages: 4,540
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  sasa hivi kuangalia bunge ni sawa na unaangalia ze comedy
   
 7. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #7
  Jul 3, 2012
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,765
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  tatizo lako mkuu umekaa kutetea kila kitu cha ccm. Huo ndo ujinga unadhani ccm wewe ni mwanachama pekee!??
   
 8. Lenja

  Lenja Senior Member

  #8
  Jul 3, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 132
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Nakubaliana na wewe kuwa noi Heri Jen kuliko Mabu ila bunge la leo asubuhi , huyu Mama kachemsha vibaya sana; Miongozo , Taarifa na Kuhusu utaratibu vimemtoa nokuauti......nae sio tu Mr, hana tofauti nahuyo Mabu
   
 9. Ruttashobolwa

  Ruttashobolwa JF-Expert Member

  #9
  Jul 3, 2012
  Joined: Feb 22, 2012
  Messages: 43,699
  Likes Received: 12,750
  Trophy Points: 280
  Umetoa ushauri mzuri sana kwa wana ccm wenzio.

  Hongera sana kwa busara ulizonazo! You have my like.

  Watanzania tunataka maendeleo sio matusi!

  Kweli sitta kiti kita ku miss
  spika ana ongea kama mvuta bangi! Ina sikitisha sana.
   
 10. Rogie

  Rogie JF-Expert Member

  #10
  Jul 3, 2012
  Joined: Nov 22, 2010
  Messages: 6,277
  Likes Received: 3,008
  Trophy Points: 280
  Mimi si mwanachama wa Chama chochote,mleta mada nikupongeze sn kwa kuweka ukweli wazi japo CCM wenzio wataona km umeweka wazi madhaifu yao. Huu ni ukweli mtupu sisi wananchi tunaelewana kinachofanyika bungeni ni kukutetea ujinga tu..MB akisema kitu cha msingi kinachogusa CCM kaa chini zitamwandama na kuzomea. Mwisho wa siku sisi tutamjua mbaya wetu nani na tutatumia haki zetu za msingi.
  CCM mmeishiwa..
   
 11. m

  mwinukai JF-Expert Member

  #11
  Jul 3, 2012
  Joined: May 3, 2011
  Messages: 1,448
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145
  Bunge ni kioo saiakinaonesha udhaifu wa CCM
   
 12. Q

  Q600 Member

  #12
  Jul 3, 2012
  Joined: Jul 1, 2012
  Messages: 6
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Michembe ndo jembe la ccm!! walio baki ni vilaza!! Sa kama jembe nalo kilaza zaidi ya vilaza wenzake ogopa sn iyo organization! Ina tia uruma kuona Ccm wana ongeza Majanga kwa kuwa na watu kama uyo bwana!
   
Loading...