Sitta: Nchi imebaki mifupa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sitta: Nchi imebaki mifupa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by ketwas, Aug 25, 2011.

 1. ketwas

  ketwas JF-Expert Member

  #1
  Aug 25, 2011
  Joined: Dec 27, 2010
  Messages: 213
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Happy Lazaro, Arusha
  WAZIRI wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta amezitaka mamlaka za dola kuwafukuza kazi, viongozi wakiwamo mawaziri wenzake waliojilimbikizia mali kwenye biashara kupitia nafasi zao.

  “Nchi imebaki mifupa mitupu huku wananchi wake wakiteseka kwa kushindia mlo mmoja na wengine wakiishi kwa kuokota vyakula majalalani, wakati huo baadhi ya watu wachafu wakiwamo viongozi wao wanaendelea kuneemeka bila kujali maisha duni ya mwananchi,” alisema mjini hapa katika ufunguzi wa Kongamano Vijana wa Kikristo kutoka nchi za Afrika Mashariki.

  Sitta alisema kama mamlaka hizo hazitachukua uamuzi mgumu kwa kuwakabili watendaji wake wenye utajiri wa kutisha, nchi itaendelea kuwa maskini na wananchi watabaki na maisha magumu.

  Kauli ya Waziri Sitta inakuja kipindi kifupi baada ya kuingia kwenye mjadala na baadhi ya makada wa chama chake cha CCM wakiwamo mawaziri alipoitaka Serikali iwaombe radhi wananchi kutokana na tatizo la umeme.

  Akizungumza katika kongamano hilo, Sitta alisema anakerwa kuona kiongozi wa Serikali akipigana vikumbo na wafanyabiashara wadogo kwenye zabuni mbalimbali zinapotangazwa.

  Sitta alisema haiwezekani kiongozi kama waziri serikalini ajiingize kwenye biashara ndogondogo za vioski akishindana na wafanyabiashara wadogo kwenye maeneo yao maalumu ambao mitaji yao ni midogo inayohitaji kuongezewa nguvu.

  Alizitaka mamlaka hizo husika kufuatilia kwa makini vyanzo vya mapato vya viongozi hao ikiwa ni pamoja na kuchunguza akaunti zao mara kwa mara ili kuona kama zinaendana na vipato vyao, hali ambayo itasaidia kubaini ubadhirifu wa fedha za umma.

  Alisema wapo baadhi ya viongozi wanaofanya biashara ambao wamekuwa wakidiriki hata kuingiza majina mengi ya watu kwenye mikopo ya fedha kwa maendeleo ya vijana na kuacha vijana walengwa kukosa mitaji.

  "Inakera kumwona mtu ni waziri lakini inapotokea mikopo ya fedha za maendeleo kwa vijana na yeye anaingiza mkono wake anaweka majina kama 10. Kwa hiyo kama mkopo ni Sh5milioni yeye anazoa Sh50milioni vijana wengine walengwa wanakosa," alisema Sitta.

  Alisema Tanzania siyo nchi ya kuwa maskini kutokana na rasilimali nyingi zilizopo lakini hali hiyo imekua kutokana na baadhi ya viongozi waliopo madarakani kutozingatia maslahi ya wananchi na kukumbatia wajanja wachache wanaojilimbikizia mali huku wakiwa huru pasipo kuchukuliwa hatua na mtu yeyote.

  "Mimi ninachoishauri mamlaka husika za dola ni kwamba, iwachukulie hatua kali viongozi watakaobainika kukutwa na fedha nyingi zisizoeleweka na sheria ichukue mkondo wake kwani watu hawa ndiyo wanaifanya nchi na wananchi kwa ujumla kubakia maskini siku hadi siku huku wao wakizidi kufaidika tu," alisema Sitta.

  Sitta alisema kwamba kuna watu wanaopenda kujilimbikizia mali bila kuangalia tabaka dogo la wanyonge wakiwamo vijana kitu ambacho ni cha hatari, kwani vijana wamekuwa wakitajwa kuwa mhimili wa nguvukazi ya taifa lakini yanapokuja maslahi yao wapo wakubwa wanaojaribu kuyapora.

  Hata viongozi wa Afrika

  Alisema hata baadhi ya viongozi wa Afrika wamekuwa wakijilimbikizia mali wanapokuwa madarakani na wanapokuja kuachia madaraka wamekuwa wakigundulika kuwa na utajiri wa kutisha, kitu ambacho kimekuwa kikichangia nchi za bara hili kuendelea kuwa maskini.

  Alisema viongozi wa aina hiyo ni vyema wakaumbuliwa mapema kabla hawajaitafuna nchi na kuiacha ikiwa na umaskini wa kutupwa huku wananchi wake wakiendelea kuteseka siku hadi siku.

  Awali, Askofu wa Kanisa la Spiritual Transformation la mjini hapa ambao ndiyo waandaaji wa kongamano hilo, Askofu Francis Mnkande alisema lengo lake ni kuwajenga vijana kiroho na kimaisha hasa ya kiuchumi ili waweze kujikwamua na hali ngumu.

  Askofu Mnkande alisema kongamano hilo la wiki moja linalenga pia kuwajengea uwezo vijana hao kuwa viongozi waadilifu na wenye kumcha Mungu katika maisha yao watakapokuwa viongozi hali itakayosaidia kuondokana na changamoto mbalimbali za uadilifu zinazowakabili viongozi walio wengi madarakani.

  Kongamano kama hilo linalokutanisha mamia ya vijana hufanyika mara moja kwa mwaka na tayari limekwishafanyika Uganda na Kenya na mwakani linatarajiwa kufanyika nchini Rwanda.

  Mwaka huu, zaidi ya vijana 500 walihudhuria wakitokea nchi za Kenya, Rwanda, Uganda, Burundi, Tanzania na Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo (DRC) ambao waliomba kushiriki.
   
 2. Amiliki

  Amiliki JF-Expert Member

  #2
  Aug 25, 2011
  Joined: May 6, 2011
  Messages: 2,087
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Maamuzi gani magumu anayoyataka huyu Mnafiki! Kuna maamuzi magumu yaliyofanywa na serikali yake kama yale ya kuvaa uso wa mbuzi na kumrudisha Jairo kazini jana kabla Bunge kuingilia kati!
  Kwa serikali hii kuchukua maamuzi ya maana hilo asahau! Hii serikali ni kama tu mwanaume wa Kihindi, lazima kwanza aingizwe kitu ili kitu kinyanyuke!
   
 3. Mess

  Mess JF-Expert Member

  #3
  Aug 25, 2011
  Joined: Mar 2, 2009
  Messages: 667
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Sita ni mnafiki wa kutupwa na huyu jamaa ameimaliza reputation ambayo angekufa nayo na watu wakamkumbuka nayo ya kuwa spika mzuri. sasa hivi anaharibu tu.
   
 4. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #4
  Aug 25, 2011
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,762
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  ukiona watu tumeanza kuona rangi za sitta ukombozi unakalibia HUYU NI MNAFIKI MKUBWA WA NCHI HII NI HATARI KULIKO LOWASA!
   
 5. Mwita25

  Mwita25 JF-Expert Member

  #5
  Aug 25, 2011
  Joined: Apr 15, 2011
  Messages: 3,840
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Huyu mzee ni maiti inayotembea, hata CCM wenyewe tumemshtukia!
   
 6. S

  SEAL Team 6 JF-Expert Member

  #6
  Aug 25, 2011
  Joined: Jun 10, 2011
  Messages: 655
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Anaandaa mikakati ya kuwanasa baadhi ya wapiganaji wa chadema ili wajiunge na CCK.
   
 7. tatanyengo

  tatanyengo JF-Expert Member

  #7
  Aug 25, 2011
  Joined: Mar 30, 2011
  Messages: 1,140
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  Mbona anawatetea wanyonge wa nchi hii, kwanini kumwita mnafiki?
   
 8. mmbangifingi

  mmbangifingi JF-Expert Member

  #8
  Aug 25, 2011
  Joined: Mar 9, 2011
  Messages: 2,855
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Mkuu angalau leo umejipambanua kuwa wewe ni CCM, kuna post yako moja ulikanusha kuwa si mmoja wao,,just a neutral observer. safi mkuu. Sasa mzee huyu Sitta mtamchukulia hatua gani au mpaka mumzike tu?
   
 9. samirnasri

  samirnasri JF-Expert Member

  #9
  Aug 25, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 1,377
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Zote hizo ni mbio za kuwania urais mwaka 2015. Sitta anajaribu kujijenga ili aonekane ana huruma na watanzania.
   
 10. majata

  majata JF-Expert Member

  #10
  Aug 25, 2011
  Joined: Oct 7, 2010
  Messages: 385
  Likes Received: 54
  Trophy Points: 45
  <br />
  <br />
  Unakumbuka alivyosimamia shughuli za selikali bungeni wakati pinda kasafiri, mnafiki mkubwa huyu mzee, amepoteza sifa, alikuwa wapi kurekebisha alipokuwa spika, yeye pia nifisadi tu kama rostam.
   
 11. Angel Msoffe

  Angel Msoffe JF-Expert Member

  #11
  Aug 25, 2011
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 6,797
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  <br /> <br / kwa sababu alishawah kusema kuwa wapinzani hasa chadema ni wanafiki.
   
 12. samirnasri

  samirnasri JF-Expert Member

  #12
  Aug 25, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 1,377
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Zote hizo ni mbio za kuwania urais mwaka 2015. Sitta anajaribu kujijenga ili aonekane ana huruma na watanzania.
   
 13. Domhome

  Domhome JF-Expert Member

  #13
  Aug 25, 2011
  Joined: Jun 28, 2010
  Messages: 1,986
  Likes Received: 1,043
  Trophy Points: 280
  Wote mpo mochwari ndo maana hakuna wa kumzika mwenzie!
   
 14. Bishop Hiluka

  Bishop Hiluka Verified User

  #14
  Aug 25, 2011
  Joined: Aug 12, 2011
  Messages: 4,100
  Likes Received: 1,424
  Trophy Points: 280
  Inawezekana usemayo lakini hata wewe umeonesha rangi yako kwenye suala hili...
   
 15. Najijua

  Najijua JF-Expert Member

  #15
  Aug 25, 2011
  Joined: Nov 5, 2010
  Messages: 1,029
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Ila nae si tuna mashaka naye!!kuna hoja kuwa nae ni msaliti na mnafiki mbona mpaka leo anakaa nyumba ya Spika na sio uwaziri na serikali inaingia gharama za kumlipia spika wa sasa mahali kwingine?nae si wanasema ana skendo ya kuumiza vijana wetu na madawa ya kulevya japo kaacha siku hizi baada ya kuneemeka
   
 16. MVUMBUZI

  MVUMBUZI JF-Expert Member

  #16
  Aug 25, 2011
  Joined: Jan 8, 2011
  Messages: 4,970
  Likes Received: 666
  Trophy Points: 280
  Hilo ni changa la macho mkuu we msikilize uondoke zako usanii mtupu huo
   
 17. L

  Lua JF-Expert Member

  #17
  Aug 25, 2011
  Joined: May 19, 2011
  Messages: 704
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Huyo ni mnafiki tu, mbona yeye anaishi kwenye nyumba masaki ya sh. 12b na kajenga jengo la spika kwao tbr huo c mfumo wa kujilimbikizia mali. Au haoni hilo.
   
 18. Mentee

  Mentee Senior Member

  #18
  Aug 25, 2011
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 142
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  anaitwa mnafiki kwa sababu ni opportunist! Mi nilimsamehe pale wakati ni Waziri wa Sheria alipopindisha Sheria iliyosababisha Ladwa kupewa kiwanja kile cha Golden Tulip Hotel. Nikamheshimu pale alipokuwa Spika wa Bunge.... lakini kumbe nilikosea. Si msafi katu na ana kamtimanyonyo kwa wenzie pale anapoona wanampiku. Baada ya kuona mifupa... je, umechukua hatua gani za kuchimba kaburi???
   
 19. pangalashaba

  pangalashaba JF-Expert Member

  #19
  Aug 25, 2011
  Joined: Jan 10, 2011
  Messages: 1,078
  Likes Received: 858
  Trophy Points: 280
  tumbaku mbaya sana...... kumbe vingereza vigumu unavyotuleteaga hapa jf ni magamba pure. nimegundua!!!!
   
 20. RAU

  RAU Member

  #20
  Aug 25, 2011
  Joined: Jul 6, 2011
  Messages: 61
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Katika mambo yanayoendelea sasa hivi ndani na nje ya bunge, ni kielelezo cha wazi kunatatizo katika mfumo mzima wa CCM.
  1. Viongozi hawaeshimiani tena,
  2. Mwenye fedha anafanya anavyotaka

  Hii ni 2011, mpaka ifike 2013 kitaeleweka
   
Loading...