Sitta: Nafaa kuwa Rais wa Tanzania!

Sitta: Nafaa kuwa Rais wa Tanzania!

mnyonge mnyongen haki yake mpeni. aliongoza bunge lenye viwango, ni shupavu. anajiamini. naona anafaa 100%.
Toa pumba hapa,kuongoza Bunge ndio kuongoza Taifa?
 
anastairi kuwa rais nampongeza kwa ujasili alionao
 
"Waliopo hatuwataki, tunaotaka kuwapa hatuwaamini" By Mrisho mpoto.
 
Hana jipya ni walewale magamba tunataka chama kingine kikamate dola [cdm] "Babu we pumzika ule matunda yako kama unashamba"
 
Sitta ni miongoni mwa viongozi ninaowakubali sana ndani ya CCM. Huyu anafaa sana kwani ana uthubutu na anapenda maendeleo. Wengine ambao ninawakubali CCM ni Mwakyembe na Magufuli.
 
Bado Magufuri na Mwakyembe nao nasikia wanautamani, dah, 2014 kuna mambo!
 
Ile nyumba ya spka Urambo vp sasa akiwa Rais ni Nyumba ya Rais Urambo kweli kila mtu ana Malengo yake.
 
Dr Slaa Tosha Urais 2015

we nae na slaa unatisha mkuu.mm sita aliniudhi kusema cdm ni slaa pekee anayeweza kuongoza na kufunga mjadala wa richmond kabla ya maazimio ya tume ya mwakyembe hayaja pata majibu.akae mbali
 
atajenga ikulu urambo kama alivyo jenga jengo la spika.kazi yake ndogo tu .ccm wakisema wanataka rais mwanamke
 
........Kama kutakuwa hakuna wagombea wa maana afadhali ya Mzee 6 achukue nafasi hiyo kuliko wengine wanaojitokeza.. Hapa duniani kuna wakati mwanadamu anaangalia kipi ni afadhali ya kingine katika kila jambo.... kipi au nini au nani atafaa au atamsaida...
 
Samwel John Sita a.k.a STANDARD AND SPEED huyu mtu sio kiongozi hata kidogo kwanza ogopa kabisa mwanaume mwenye maneno ya jikoni kama mwanamke hafai nasema hivi kwani namfahamu vyema na mm ni mpiga kura wake, anapenda sana kutukuzwa na kujisifia yeye ni mtawala na ogopa sana mtu wa ngenga za namna hii, Hana upendo hata kidogo kwa wapiga kura wake, kwa nyazifa alizowahi kushika katika taifa hili Urambo isingekuwa namna hii pamoja na kuwa Halmashauri hii kuwa ya pili kitaifa kuingiza fedha za kigeni ukiiondoa wilaya ya Temeke yenye Bandari, huyu jamaa hata nyumba ya familia aliyojenga kwao na mama yake mzazi kukoswa koswa kuangukiwa na nyumba ya nyasi na watoto wa mdogo Paul Sita alikataa kabisa kuwapeleka shule ikabidi waombe Halmashauri iwasoshe mithili ya yatima hii ni pamoja na watoto wa Mzee Simwanza kaka yake na mke wake ambae nae mtu mkubwa ktk serkali miaka mingi kama mnavyojua Magreth Sita watoto wa kaka yake wasingeathirika mpaka Simwanza ambaye ni mzee asiye na kipato chochote mpaka kuomba watoto wake walioko Ukombozi Sec kuomba wasomeshwe na Halmashauri na wakati dada yake Magreth yupo na ana kipato kikubwa sana, sasa je hawa ni viongozi watakaolifaa taifa? Na maneno ya mungu katika Biblia yanasema asiyeijali familia na ndg zake ni sawa na muuaji. Kama wao wana dini mbona hawayatii haya maneno ya mungu? zaidi ya yote Sita anajulikana kama mwenye Siasa za majungu Urambo hata watumishi wa serkali ukisalimiana na Kapuya tu umehamishwa hii imetokea kwa wengi tu na majina ni Bwana Kiyungi, Bw Ngangaji na wengine wengi walikuwa wakuu wa idara mbalimbali wa Halmashauri ya wilaya ya Urambo ambao walisambazwa mikoa mingine kwa sababu wanasaliana na mbunge mwenzake wa Urambo magharibi Pr Juma Athmani Kapuya sasa huyu ndie awe kiongozi wa kuijenga Tanzania na wakati nyumbani kwao tu ameshindwa kuweka hata msingi baada ya nyumba ya miti ya mama yake kuanguka hivi karibuni mwaka 2007?
 
Jamani kumbukumbu zangu zinaonesha kuwa Mzee 6 ni mwanzirishi wa CCJ wakiwa na mlopokaji Nape. Sasa iweje aseme CCM wakichagua mtu asiyekubalika upinzani utachukua nchi kiurahisi au asipochaguliwa kuwa mpeperushaji wa bendera ya CCM atakimbilia CCJ kupeperusha? Huyu Mzee anazeeka vibaya sijui tatizo lake lilitokana na walipomletea mizengwe ya kuwa mgombea wa Uspika lazima awe mwanamke hivyo kwa kuwa muda ulikuwa mdogo kwa yeye kujibadilisha anaona ni bora kuwavuruga tu sasa ili tukose wote...
umesema vema
 
Kugombea sawa, kuwa rais NOOOO.

Six akiibomoa CCM atakuwa ametoa mchango mkubwa zaidi kwa Tanzania.
 
Kwani CCJ aliyoianzisha imefutiwa usajili na Tendwa? Si aende huko? Chama chenye kutoa Rais wa TZ ni CHADEMA tu wengine hawana mpango.
 
Kumbe hawa watu wana hamu sana ya kutangaza nia sema tu wanaoneana aibu. Bado Membe
 
Back
Top Bottom